bongo united fc

Timu kabambe ya Bongo United jumamosi april 11 iliipa kipigo cha mbwa mwizi mabao 3-2 timu ngumu ya Liberia ya North Carolina mbele ya mashabiki wao kwenye uwanja wa Scott King uliopo mji wa Durham.
 
Mchezo uliaza kwa kasi huku wenyeji wakifanya mashambulizi mfulululizo yaliozaa goli katika dakika ya 23 ya mchezo goli llilofungwa  na mshambuliaji mkali Denis Jonson kwa shuti kali mita 40 na kumfanya golikipa wa bongo united Luke akigala gala bila mafanikio.
 
Bao hilo lilimfanya kocha msaidizi wa timu ya Bogo United Fc Aligo Sachi(Dedy Luba)alieambatana na timu badala ya kocha mkuu supa kochi Gharib Latto kua na dharula kwa mwajili wake kufanya mabadiliko ya kumtoa Ray Abraham na Hussein na nafasi zao kuchukuliwa na Haji Helper na Elvis Dotto Mnyamuru.
 
Mabadiliko hayo licha ya kuleta uhai kwa bongo united yalibalibadilisha sura ya mchezo na kuifanya Bongo United kutandaza kabumbu la kitabuni  na kumfanya golikipa wa bongo united kua likizo isiokua na malipo,huku ikipendeza kwa uzi wa Chelse utafikiri wapo wanja la darajani.
 
Mpaka mapunziko Liberia walikua wanaongoza kwa bao 1-0,kipindi cha pili Bogo united fc ilikianza kwa kulishambulia goli la liberia kama nyuki huku ikimuacha mlinda mlango George Taylor wa Liberia kuokoa mshambulizi yaliokua yakiongozwa na mshambuliaji machachali Vicent Ndusilo akisadiana na winga wa kulia mwenye kasi ya ajabu Ebra Nyagaly.
 
Kunako dakika ya 67 mchezaji wa kiungo Elvs Dotto Mnyamuru aliipatia Bongo United bao la kusawazia kwa shuki kali lilomuacha golikipa wa Liberia akidaka hewa huku nyavu zikitikisika,bao hilo liichanganya beki ya Liberia na kua inatoa mipira onyo ya kona ambazo ziliipatia Bongo united Fc mabao mawili ya haraka haraka katika dakia ya 79 na 83 yalio fungwa na Vicent Ndusilo moja kwa kichwa na lingine kwa kifua.
 
mabao hayo yaiamsha timu ya Liberia ambayo washambuliaji wake waliwekwa kapuni muda karibuni wote wa kipindi cha pili na safu ya ulinzi ya Bongo united fc iliokua ikiongonzwa Kheri Yahaya akisaidiwa na David jua kali huku kulia Steave Majumbo akifanya kazi yaziada akisidiwa na Beki wa kushoto Libe Mwang'ombe (Germany Defence).
 
Kunako dakika ya 90 Liberia walipata bao la pili lilifungwa na Denis Jonson na kufanya mpira uishe kwa Bongo united kushinda kwa bao 3-2 na kuwasubiri Houston stars may 24 kwa mpambano unaosubiriwa kwa hamu na washabiki wa kabumbu Washington Metro Area na Jirani zao na habari tulizo zipata Radio mbao Houston jumamosi april 11 ilishindwa kufurukuta dhidi ya timu zaifu ya Sudan ilipochapwa bao 4-2 kipigo kichopelekea washindwe hata kuleta matokea kwenye glob ya jamii,poleni sana Houston

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. When i was born, I heard Man Utd's Song.
    When I slept in my cot, i had a dream,
    "Man Utd Was The Dream"
    FOREVER MANCHESTER UNITED

    ReplyDelete
  2. Manchester United = Joy of English Football
    Manchester United = Joy of European Football
    Manchester United = Joy of World Football
    Manchester United = Joy of Modern Football
    Manchester United = Joy of Entertainment and Attacking Football
    Manchester United = Joy of the Fans

    ReplyDelete
  3. When you’re in the tunnel and you hear on the speakers, “Please welcome the champions of England, the champions of Europe and the champions of the world,” you just believe that you are going to crush anybody that is in your way. I get goosebumps every time I walk out at Old Trafford. It’s great.

    HAHAHAHAHAHAAAAAA

    ReplyDelete
  4. BADO HOUSTON.

    ReplyDelete
  5. Bongo united Fc na jezi ya chelsea wapi na wapi? nitafuteni niwatumie jezi ya Tanzania mtawakilisha safi zaidi!
    email: liwang57@yahoo.com

    ReplyDelete
  6. HYMN of REAL MADRID

    Of the sport glories
    that they graze in the fields by Spain
    Madrid with its flag goes
    clean and white that does not dim


    Pure-blooded and generous club,
    all nerve and heart,
    veterans and noveles,
    veterans and noveles,
    your laurels watch always
    with respect and emotion


    Hala Madrid! , Hala Madrid!
    Nobleman and warlike leader,
    horseman of the honor.
    Hala Madrid! , Hala Madrid!
    To prevail in good combat,
    being defended your color


    Hala Madrid! , He hauls Madrid! , He hauls Madrid!
    Enemy in the fight,
    when he loses gives the hand
    without you envy nor resentments,
    like good and faithful brother


    Sundays in the evening,
    walking to Chamartìn,
    the Madrilenian mocitas,
    the Madrilenian mocitas
    go glad and smiling
    because today its Madrid plays


    Hala Madrid! , Hala Madrid!
    Nobleman and warlike leader,
    horseman of the honor.
    Hala Madrid! , Hala Madrid!
    To prevail in good combat,
    being defended your color
    Hala Madrid! , Hala Madrid! , Hala Madrid!

    ReplyDelete
  7. hao bongo united nawatamani tucheze nao...kama vipi mje wichita kucheza na sisi.wenzenu hao houston walikula goli tano.

    ReplyDelete
  8. Huyo wa kwanza waliosimama(shoto) naye anacheza soka au anacheza American Football?Jamaa ana bonge la kitambi kukimbia atawezaje?

    ReplyDelete
  9. hawa Bongo Yunaitedi kweli hamnazo.yani kwa kuwa mna matumbo makubwa basi hiyo 3-2 mnaita kipigo cha "mbwa mwizi".yani mna haki ya kusema hivyo kwani wengi wenu mko "out of shape".mngeshinda 1-0 mngesema "mauaji".

    ReplyDelete
  10. huyo Haji Helper na Elvis Doto ni wachezaji wa Tanzanite FC,ina maana mlichukua majeshi?hahaha

    ReplyDelete
  11. Bro Michu hebu nifikishie salamu zangu kwa Rais wa TFF.. Mbona chama hiki kinaongoza soka kwa mtindo wa kizamani sana? Hivi ni kwa nini hawajifunzi na kubadilika? Mi nimesikia suala la kuvunjwa kwa mechi la ligi ya bara. mara mbili sasa kisa eti ni mvua kubwa iliyonyesha. Mechi kama ya Yanga na Polisi Dodoma mwamuzi aliivunja dakika ya 75! huku wachezaji wote wakiamini wanaweza kucheza hadi mwisho, Mechi ya Simba na Azam waliivunja vivyohivyo kwa sababu zilezile. Inakuaje TFF?
    Sasa kuna kastory ka Mgosi na Kado kufungiwa. Jamaa wallipewa kadi nyekundu wameshatumikia mechi tatu lakini jamaa wanawazuia wasicheze eti kamati bado haijakaa! TFF acheni upuuzi huo, mbona mnakaa na Yanga na Simba kujabili kuhusu uwanja na viingilio inonekana mnajali sana pesa kuiko maendeleo ya soka nchini. Kumbuka watu walikuchagua ili uskukume gurudumu la soka la bongo na si kujinufaisha kama mfanyavyo sasa.
    Michuzi hata usipoitoa hii comment naomba nifikishia ujumbe kwa Tenga tunataka marekebisho ya kanuni za soka
    hatutaki mechi kurudiwa hovyohovyo kama mechi ya Yanga na Polosi au Simba na Azam kwani ikumbukwe kwamba timu zinazoingia gharama ya maadalizi ya mechi ndizo zinazoumia,si wao.
    Then hatukaki kusikia mchezaji amanfungiwa miezi sita kwa kosa la kijinga,kumfungia mchezaji anayetumua miguu kupata kula yake kwa miezi sita sio utu ni sawa na uuaji.
    Pia masuala kama haya ya Mgosi na Kado ni utoto na kukomoa vilabu, kwani je ikionekana kama jamaa hawakustahili adhabu zile je mtalipa fidia?
    Na maamuzi ya TFF kuwanyanganya timu points ni upuuzi mtupu,ni mambo yanayoonesha uongozi wa ubabaishaji. Huwezi kupoka points kwa timu hii haipo kwenye soka la kisasa katika dunia hii eti kisa timu ilikata rufaa kwa kutumia wachezaji walio kwenye adhabu. Kwani ni nani anayetunza ripoti ya match commissioner kati ya klabu na TFF? mbona nyie TFF mlitumiwa waraka na FIFA kuhusu kutomtumia Nsajigwa kwenye WC match? si kwa sababu wanatunza kumbukumbu za kila mechi.
    Ni hayo tu bwana Michu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...