katibu mkuu wa klabu ya michezo ya break point, mzee mwawanda, akiwa ameongozana na wanachama waandamizi wa klabu hiyo, akimkabidhi kadi na ubani mjane wa marehemu hamidu bisanga, mwandishi mkongwe aliyefariki katika ajali ya gari wiki iliyopita jijini dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Maskini Mama yangu Tunu, Mungu akupe uvumilivu na maisha yenye amani na utulivu na naomba Mungu akutangulie sana kwenye wakati huu wa majonzi. Hali kadhalika ndugu zangu Issa na dada yangu Khadija Mungu awape baraka zake na awape uvumilivu kwenye WAKATI HUU wa kuondokewa na Baba yetu Hamidu.

    Mungu awatangulie wote Inshallah kwa kila jambo.

    Mdau Issa D

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa kutoa ubani wote waliotoa Mungu awajalie zaidi lakini mpelekaji kavaa kaptura haikunifurahisha au kwa sababu ni mwanamichezo?

    ReplyDelete
  3. Aisee roho yaniuma kupita mfano kuhusiana kifo cha mpendwa wetu Hamidu Bisanga, lakini hakuna jinsi nakuombea upata moyo wa faraja my dia sister tunu na wanangu wote Khadija, Ahmed, Hawa, Issa na Mdogo wenu nadya

    ReplyDelete
  4. Wafiwa nawapa pole, mungu ndie aliepanga,
    lakini huyo mtoa ubani vipi?
    ni mtu mzima ila etiquette hana kabisa, au anadharau.
    sijapenda!!!!!!
    Wanaume wengine kama huyo mjirekebishe, IT MATTERS A LOT

    ReplyDelete
  5. Mama Pole na ndugu zangu wote, mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu kwani kuondokewa na mzazi ni pigo, lakini kila nafsi itaonja umauti tunachotakiwa kujiweka tayari kwa safari. Poleni ndugu zangu wote,Hawa, Ahmed, Hadija, Issa, Nadya na Ahmed mdogo.
    M.

    ReplyDelete
  6. Kaka rekebisha anaitwa Radislaus Mwamanga .. Wafiwa poleni sana.

    ReplyDelete
  7. Marehemu alikuwa mwanachama wa klabu hiyo ya michezo na hapa wanamichezo wenzake ndio wanatoa ubani, nadhani ndio sababu ya kuvaa kaptura. Poleni sana wafiwa mwenyezi Mungu wape nguvu pia ninawapongeza club brake point kwa kuwafariji wafiwa.

    ReplyDelete
  8. Poleni sana wafiwa na mungu awape moyo wa subila na uvumilivu katika kipindi iki. lakini huyo ndugu aliyevaa kaptula ndio kachafua kabisa. hata kama ni uana michezo lakini si sahii kwamtu mzima kwenda sehemu kama hiyo uku umevaa kaptula ni aibu. mambo ya kuiga yatatufikisha pabaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...