Marehemu Rashid Lema

Koplo Rashid Lema, mshtakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi, jijini Dar amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Ocean Road jijini, alikohamishiwa baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa muda.

Marehemu Koplo Lema ni mmoja wa washtakiwa tisa katika kesi hiyo, akiwemo mshtakiwa namba moja, Abdallah Zombe, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa Dar es Salaam na ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam.

Koplo Lema, ambaye ni shahidi muhimu wa utetezi kulingana na maelezo yake ya awali katika kesi hiyo, alilazimika kulazwa Muhimbili akitokea katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke alikokuwa amelazwa tangu kiasi cha wiki tatu zilizopita, baada ya uvumi kuenea wkamba ameshavuta.
Mengi zaidi baadaye

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hiyo fulana karibu ifanane na ile fulana ya jamii

    ReplyDelete
  2. Yesu, Maria na Yosefu! Ote lanyo! Kuorye kindu aho! Yeeeeeleeeeeuuuuuwiiiiiii! Ulalu kitewe wamrestisha in peace Lema wa watu jamani! Shahidi namba 1 jamani! Nyaaaanyiii, ngalewa! Kuorye kindu iho! Wachaga tunalia jamani!

    ReplyDelete
  3. Mr ShabbbanApril 03, 2009

    Eeeee..!!!!.Mambo ya GODFATHER. Tumeendelea.

    ReplyDelete
  4. huuu wizi mtupu

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa na pia pole taifa kwa ujumla maana sasa longolongo zitaanza....mara wameachiwa huru hakuna ushahidi... DOH jamani ...

    Poleni sana wafiwa poleni sana mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

    Natunaomba sheria ichukue mkondo wake.

    ReplyDelete
  6. daa....hamna tofauti na mambo ya Balali kuondoka na ushahidi.....Anyways, he suffered maskini, Mungu amlaze mahali pema...

    ReplyDelete
  7. Hapo sasa ndo mnanichanganya,hebu wataalamu nambieni hapa ndo kesi inakuwa imeisha au hukumu inaweza kuendelea kwa kina zombe!

    ReplyDelete
  8. plse tell us more kakufa na nini na mbona wakiwekwa humo jela za bongo washtakiwa wana dedi ama there is something goin on? i think
    wanafanyiwa vimambo kama vya guantanamo bay??? michuzi ebu investigate and tell us the secret xx

    ReplyDelete
  9. wewe ulieandika kichaga umenichekesha sana, hamna kitu hapo ni maradhi tu yalikuwa yana msumbua huyo, nasikia ugonjwa wa kisasa.

    ReplyDelete
  10. Anon wa April 03, 2009 4:16PM kama ugonjwa wa kisasa huwa unapamba moto mtu akiwa mahabusu basi "Mzee wa katoweka" muda ni mrefu naye tuasikia chali...

    ReplyDelete
  11. Poleni wafiwa wote, pamoja na sisi sote tuliokuwa tunasubiri muelekeo wa kesi nzito ya akina Zombe.
    Sina nia mbaya, lakini mimi nina wasiwasi kuwa huyu marehemu aidha "wamemKolimba au
    wamemBalali".

    ReplyDelete
  12. Kweli ile fulana aliyovaa marehemu inafanana na fulana ya jamii...rangi tu ndiyo tofauti!! Michuzi nani kakutafsiria hicho kichaga au umepost tu hiyo comment?kama ni lugha ya kuchafua hali ya hewa je? Utajuuuuuuta..... Sasa Koplo Lema kwanini kafa? itakuwa vigumu kuamini kifo chake kama hakina mkono wa mtu...Duh!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...