Marehemu Koplo Lema ni mmoja wa washtakiwa tisa katika kesi hiyo, akiwemo mshtakiwa namba moja, Abdallah Zombe, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa Dar es Salaam na ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akikaimu nafasi ya Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam.
Koplo Rashid Lema, mshtakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi, jijini Dar amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Ocean Road jijini, alikohamishiwa baada ya kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa muda.
Koplo Lema, ambaye ni shahidi muhimu wa utetezi kulingana na maelezo yake ya awali katika kesi hiyo, alilazimika kulazwa Muhimbili akitokea katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke alikokuwa amelazwa tangu kiasi cha wiki tatu zilizopita, baada ya uvumi kuenea wkamba ameshavuta.
Mengi zaidi baadaye
Hiyo fulana karibu ifanane na ile fulana ya jamii
ReplyDeleteYesu, Maria na Yosefu! Ote lanyo! Kuorye kindu aho! Yeeeeeleeeeeuuuuuwiiiiiii! Ulalu kitewe wamrestisha in peace Lema wa watu jamani! Shahidi namba 1 jamani! Nyaaaanyiii, ngalewa! Kuorye kindu iho! Wachaga tunalia jamani!
ReplyDeleteEeeee..!!!!.Mambo ya GODFATHER. Tumeendelea.
ReplyDeletehuuu wizi mtupu
ReplyDeletePoleni wafiwa na pia pole taifa kwa ujumla maana sasa longolongo zitaanza....mara wameachiwa huru hakuna ushahidi... DOH jamani ...
ReplyDeletePoleni sana wafiwa poleni sana mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Natunaomba sheria ichukue mkondo wake.
daa....hamna tofauti na mambo ya Balali kuondoka na ushahidi.....Anyways, he suffered maskini, Mungu amlaze mahali pema...
ReplyDeleteHapo sasa ndo mnanichanganya,hebu wataalamu nambieni hapa ndo kesi inakuwa imeisha au hukumu inaweza kuendelea kwa kina zombe!
ReplyDeleteplse tell us more kakufa na nini na mbona wakiwekwa humo jela za bongo washtakiwa wana dedi ama there is something goin on? i think
ReplyDeletewanafanyiwa vimambo kama vya guantanamo bay??? michuzi ebu investigate and tell us the secret xx
wewe ulieandika kichaga umenichekesha sana, hamna kitu hapo ni maradhi tu yalikuwa yana msumbua huyo, nasikia ugonjwa wa kisasa.
ReplyDeleteAnon wa April 03, 2009 4:16PM kama ugonjwa wa kisasa huwa unapamba moto mtu akiwa mahabusu basi "Mzee wa katoweka" muda ni mrefu naye tuasikia chali...
ReplyDeletePoleni wafiwa wote, pamoja na sisi sote tuliokuwa tunasubiri muelekeo wa kesi nzito ya akina Zombe.
ReplyDeleteSina nia mbaya, lakini mimi nina wasiwasi kuwa huyu marehemu aidha "wamemKolimba au
wamemBalali".
Kweli ile fulana aliyovaa marehemu inafanana na fulana ya jamii...rangi tu ndiyo tofauti!! Michuzi nani kakutafsiria hicho kichaga au umepost tu hiyo comment?kama ni lugha ya kuchafua hali ya hewa je? Utajuuuuuuta..... Sasa Koplo Lema kwanini kafa? itakuwa vigumu kuamini kifo chake kama hakina mkono wa mtu...Duh!!
ReplyDelete