
HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE
1938-1984
KESHO APRILI 12, 2009 ITAKUWA IMETIMU MIAKA 25 KAMILI TOKEA WAZIRI MKUU WA ZAMANI HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI HUKO DAKAWA KATIKA NJIA KUU YA MOROGORO-DODOMA.
KWA MUJIBU WA TAARIFA YA FAMILIA YA HAYATI SOKOINE, KESHO HAKUTAKUWA NA HAFLA RASMI YA KUKUMBUKA MIAKA 25 YA KUFA KWAKE BALI SALA MAALUMU ZITAFANYIKA KATIKA MAKANISA YA ST. PETER NA ST. JOSEPH JIJINI DAR NA PIA KATIKA KANISA LA ROMAN CATHOLIC MONDULI JUU WAKATI WA IBADA YA PASAKA HIYO KESHO.
TAARIFA HIYO IMESEMA KWAMBA HAFLA MAALUMU YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA KIFO CHA SOKOINE IMEPANGWA KUFANYIKA AGOSTI 1, 2009 HUKO MONDULI JUU, NA KWAMBA TAREHE YA HAFLA HIYO IMESOGEZWA MBELE KWA KUWA KESHO NI PASAKA NA WENGI WANAOTEGEMEWA KUHUDHURIA WATAKUWA KATIKA MAJUKUMU YA SIKUKUU YA PASAKA.
AGOSTI 1, 2009 NDIYO SIKU YA KUZALIWA KWAKE HAYATI SOKOINE NA FAMILIA IMEONA ITAKUWA VYEMA HAFLA MAALUMU YA KUMKUMBUKA IFANYIKE SIKU HIYO.
PAMOJA NA MAMBO MENGINE HAYATI SOKOINE ATAKUMBUKWA KWA UCHAPAKAZI ULIOTUKUKA PAMOJA NA KUCHUKIA NA KUKEMEA UFISADI WA AINA YOYOTE KIASI HATA RAIS WA WAKATI HUO MWALIMU NYERERE ALIMTEUA MARA MBILI KUWA WAZIRI MKUU. NA KWELI MAFISADI WALIKIONA CHA MOTO. HAKUKUWA NA MASIHARA KABISA ENZI ZAKE.
JIKUMBUSHE MAMBO YA HAYATI SOKOINE
NA
those minbuses were called daladala because were charging 5sh coin which was equivalent to 1us dolla by that time. hence daladala emerged as a nickname.
ReplyDeleteTunammisi sana, alikua waziri wa watu na sio waziri wa ufisadi.
ReplyDeleteEdward na Amina Chifupa mkae mahali pema peponi.
EDWARD MORINGE SOKOINE,HOLLASI KORIMBA VIFO VYAO VIMEILAANI TANZANIA WAO WALIKEMEA RUSHWA
ReplyDeleteWATU WAKAWATENDA MAMBO BASI TOKEA HAPO HII NCHI NI RUSHWA MTINDO MMOJA KWANI MTU AKISEMA WANA MFANYA MAMBO KUMBE KILA MTU NI KUKAA KIMYA NA KULA VYA WAVUJA JASHO
HALAFU UKIICHUKIA NCHI WANAANZA KUSEMA ETI MKAATAA KWAO NI MTUMWA BORA NIKAWE MTUMWA KWA WATU KULIKO KUWA MTUMWA NYUMBANI KWENU.
TANZANIA INABIDI IHUNGAME KWA MAMBO ILIYOWAFANYIA VIONGOZI WALIOKUWA NA MOYO NA NCHI NASEMA HAYA KWA UCHUNGU TOKA MOYONI MWANGU
ReplyDeleteLEO TUNAKUMBUKA YESU ALITUFIA MSARABANI JANA SASA BASI
KAMA KWELI MNATAKA KUITOA RUSHWA TANZANIA INABIDI IHUNGAME KWA VIONGOZI WAPINGA RUSHWA WALIOKUFA KWA VIFO VYA AJABU AJABU SISI WOTE SI WATOTO TUNAJUWA YALIYOPITA ILA KUFANYA HIVYO HUENDA WALE WATU KULE WALIKO WATAISAMEHE NCHI NA MAMBO YAKATUENDEA VIZURI.
MR.MICHUZI NAOMBA USIYABANIE MAONI YANGU HAYA NI MAONI TU.
TUSIENDELEE KUFANYA UNAFIKI NA WALIOTUTANGULIA WANAONA NA TENA TUNAVITA KUBWA YA KUPIGANA NA RUSHWA HATA RAIS WETU INAMPA TABU KUONGOZA NCHI ILIYO JAA RUHWA IMEKUWA VIGUMU KUITOA RUHWA NA IKITOKEA RAIS KIKWETE MIAKA KUMI YAKE IKAISHA BILA RUSHWA KUISHA SIDHANI KAMA KUNA RAISI ATAKUJA KUITOA RUSHWA TANZANIA
alikuwa mzuri wa sura,tabia,roho,na mchapakazi we real miss you
ReplyDeletesiamini kama hatunaye mtu mzuri vile jamani ama kweli wema hauna maisha
ReplyDeleteMungu ampe raha ya milele mpiganaji huyu shupavu bila mfano hapa Tanzania.
ReplyDeleteKumi na mbili tarehe, aprili nane nne,
ReplyDeleteilikuwa si sherehe, kufariki sokoine,
mkemea walanguzi, waangushao uchumi.
Kiongozi mshiriki, nchi kuitembelea,
mtatua kila dhiki, nchi ipate pendeza.
bado tunaomboleza, kifo chake sokoine.
Wa bara na visiwani, nisikieni jamani,
kupitia redioni, niliona kama ndoto,
na katu sikuamini, nikauliza jirani.
Kiongozi mshiriki, nchi kuitembelea,
mtatua kila dhiki, nchi ipate pendeza.
bado tunaomboleza, kifo chake sokoine.
alitokea dodoma, kwenye bunge kujadili,
sheria zenye hekima, pia kujibu maswali,
akija daresalama, akapatwa na ajali.
Kiongozi mshiriki, nchi kuitembelea,
mtatua kila dhiki, nchi ipate pendeza.
bado tunaomboleza, kifo chake sokoine
Yaani nilikua mdogo sana lakini bado nakumbuka nilikua wapi alivyofariki huyu waziri....First time kumwona mama yangu analia....
ReplyDeleteNakumbuka nilikuwa na miaka 10 wakati ule ilikuwa nadra kusikia msiba.
ReplyDeleteTulimpoteza kiongozi shupavu na kamwe hatutapata kama yeye. Waliopo ni mafisadi tupu!
Eee Bwana Mungu mpe pumziko la aman MTanzania shupavu mpenda ukweli asiyekuwa na majungu wala tamaa ya madaraka wala pesa..... Moringe, waTanzania tutakukumbuka!!! Pumzika Baba!!
ReplyDeleteNyie ni washenzi sanaaaaaaaaaaaaaaa, Nimetuma comments yangu jana hamjaiweka watu wakaisoma wakaona kuwa tunajua waziri ni mafisadi # 1. Basi na nyie mnahusika. Ningekuwa nimeongelea mambo ya ngono hapo mgeiweka sasa kwa vile najua siri za viongozi wenu jinsi wali mafisadi mmezitoa. Lakini tutaandamana hadi Ikulu.
ReplyDeleteViongozi wenyewe wanatuchafulia nchi yetu.
Tena mkome kabisa.
Huyu alipigania nchi yetu kwa kila jasho lake uhakikisha kila mtanzania anapata haki yake.
Yaani ungelikuwepo kila mtanzania angelikuwa anatapata haki yake. Tunakulilia sana. GUSA vilio vyetu.
ReplyDeleteMalaika wa Bwana akulinde na uendelee kupumzika milele. Amini
Nikitaka kukumbuka Marehemu Sokoine alifariki lini huwa naimba mwanzo wa wimbo huu, maana enzi zile huwa hii ilikuwa inatoka ktk mtihani wa Siasa, nilipoona hii post nikauimba ili nijue kama tushafika au tumeipita siku hii, nimeuimba tu na mara nnaouona wimbo, big up mdau uliyetukumbusha wimbo huu. Nilikuwa la tatu A pale muhimbili primary , dah.
ReplyDeleteYule dereva yupo wapi aliyesababisha ile ajali???
Nilikuwa Masange JKT wakati huo. Nilikuwa najiandaa kwenda kwenye zamu ya ulinzi, halafu tuliitwa mbele ya ofisi kuu. Tukaambiwa hiyo habari ya kusikitisha.
ReplyDeleteNa kweli yule dereva Dumisane sijui yuko wapi?