
madaraka selemani 'mzee wa kiminyio'
UONGOZI WA FANJA SPORTS CLUB HAPA OMAN UNAPENDA KUTOA SALAMU ZA DHATI KWA MCHEZAJI WAKE WA ZAMANI MADARAKA. MADARAKA SELEIMANI ALIKUWA NI MCHEZAJI ALIEPATIA SIFA SANA TIMU YA FANJA YA HAPA OMAN.
MECHI YAKE YA MWANZO ALIPOICHEZEA FANJA - INAKUMBUKWA NA WATU WENGI - KWANI GOLI ALILOFUNGA ILIKUWA KARIBU UMBALI WA METER 35. ITAKUMBUKWA MWAKA HUO ALIWEZA FANJA KUCHUKUWA UBINGWA WA OMAN. YEYE NA MAREHEMU RAMADHAN LENI WALING'ARA SANA KATIKA TIMU HII.
WENGINE WALIOKUWA PAMOJA NA MADA NI AHMED AMASHA, HILALI HEMEDI, TALIB HILAL, ZAHOR SALIM , ABDUL WAKATI NA BAADAE WACHEZAJI ATHUMANI CHINA, YUSUF TIGANA, SHAABANI RAMADHANI, RAJABU SHAMTE WALIWAKA SANA KATIKA KUIENDELEZA FANJA.
ALIKUWAS MFUNGAJI BORA WA LIGI - NA KWA NIABA YA WAPENZI NA VIONGOZI WA FANJA SPORTS CLUB YA OMAN - TUNATOA SALAMU ZETU ZA DHATI KWA VETERANI HUYO AMBAYE SASA AMESTAAFU SOKA.
Hawa Fanja walikuwa hawanunui wakristo ?
ReplyDeleteJamaa kweli alikuwa moto, hata Yanga wanamuota hadi leo alikuwa akichukua mpira anawakusanya anavyotaka. Nadhani hata sasa pamoja na umri mkubwa akipewa wingi ya kulia sioni mtu wa kumzuia pale yebo yebo!!
ReplyDeleteMdau wa kwanza usilete udini. inaonekana umetawaliwa na udini, hata hao wachezaji wenyewe watakushangaa. Kila jambo unatanguliza dini mbele wewe si mpenzi wa mpira, labda mlokole. Kwani hao wachezaji walikuwa wabovu?
ReplyDeleteWalitakiwa wamtumie BARUA ama wampigie simu. Kama haingii katika 'Blogu ya Jamii" atapataje ujumbe. Pia wasimuenzi kwa maneno tu, wanaweza hata kuitisha mechi ya "Veterani" mapato wamkabidhi na wengineo.
ReplyDeletekalaghabaho, FANJA hujawahi kumsikia INNOCENT HAULE aliyekuwa akiichezea small simba? acheni udini.
ReplyDeleteMzee wa Kiminyio alikuwa noma. Anastahili pongezi zaidi kwa kuweza kucheza soka la kiwango cha juu katika umri mkubwa. Kuna mechi alienda kuichezea Taifa Stars huko Botswana au Swaziland nafikiri, mwandishi wa habari alipomwona akashangaa kwamba bado anachezea timu ya taifa. Aliendelea kushangaa zaidi alipomwona akifanya vitu uwanjani.
ReplyDeleteMastriker wa kibongo, nendeni kwa mzee wa kiminyio mkachote hazina ya maarifa kwake. Huyu alikuwa akiwepo uwanjani mashabiki tunajua kuna bao.
TOENI HELA BASI IL TIMU TUIFUFUE TENA,WACHEZAJI BADO WAPO WA UHAKIKA NA KUWEZA KUIREJESHEA TIMU YENU JINA LAKE LA ZAMANI,KAMA MUKO OK WEKA ADRESS YAKO ILI TUWASILIANE NA WEWE TUKULETEENI VIFAA VYA UHAKIKA ,ILA TU MLIPE KWANI SOKA NI HELA,MUKISHINDA UBINGWA NA KUFIKA MBALI KOMBE LA ASIA,HELA KIBAO MUTAINGIZA,FUFUENI TIMU KWANI HELA MNAYO ILA UBAHIRI TU NDIO UNAKUSUMBUENI,ANYENI SASA HISTORIA HIO HISTORIA INATAKIWA IZIDIWE NA KITU CHA LEO,WACHEZAJI WAPO WENI WAZURI TU,HERA MNAYO KWANINI MUDORORE HADI LEO.
ReplyDeleteHAPO MBONA UMEMSAHAU GAGA RHINO,NA METHOD MOGELLA,NA WENGINEO
ReplyDeleteMNAMKUMBUKA JINSI ALIVYOWASAIDIA. JE NYIE MLIMFANYIA NINI CHA MAANA KWASABABU NAMUONA MECHOKA KISHENZI?
ReplyDelete