Mkuu wa udhamini na mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(katikati) akiongea na waandishi wa habari leo wakati wa kumuaga nyota wa Vodacom Globbal Soccer star Francis Castor(kulia) anayekwenda Ubelgiji kujiunga na shule maalumu ya soka Cercle Brugge na kugharamiwa na Vodacom Tanzania,(kushoto)Meneja udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna.
Hatimaye nyota mmoja wa Vodacom Global Soccer Star, Francis Casto anaondoka leo kwenda nchini Ubelgiji kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza aliwaambia Waandishi wa Habari jana Jijini kwenye hafla ya kumuaga mchezaji huyo kwamba nyota huyo akiwa nchini Ubbelgiji atajiunga na shule maalum ya soka/timu iitwayo Cercle Brugge na atakuwa nchini humo kwa wikli mbili.

Alisema kijana huyo anakwenda Ubelgiji ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya kuwatafutia nyota hao shule ama timu za kujiendeleza kisoka barani Ulaya.

Sanjari na Casto nyota wengine ni Salum Saad (Zanzibar) na Cosmas Mwazembe (Mbeya), ambao alisema kampuni yake iko kwenye hatua za mwisho mwisho za kuwapeleka barani humo.


Alifafanua Casto alipatikana ndani ya kundi kubwa la vijana 11,000 waliojaribiwa kote nchini na waalimu mahiri wa soka kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na nchini Uingereza na mwisho kuchaguliwa kwa kura na maelfu za Watanzania,.


“Hivyo mtaona ni jinsi gani Casto na wenzake wawili walivyopigana ili kupata nafasi, hii kwa kweli wanastahili pongezi,” alisema.

Rwehumbiza alisema Vodacom Tanzania itaendelea kudhamini soka na michezo kwa ujumla ili kulipatia taifa wawakilishi bora kwenya anga za kimataifa.

Mpango wa kusaka nyota VGSS ulianza mwezi Mei mwaka jana na kufikia tamati tarehe Mosi mwezi Novemba mwaka huo huo, ambapo Vodacom Tanzania kama mdhamini Mkuu kwa kushirikiana na wadau wengine wa soka iliendesha mpango maalum wa kusaka vipaji vya soka kwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 16 na 22.

Kati ya mwezi Mei na Juni mwaka jana vijana walikusanyika kwenye kambi maalum za usaili zilizogawanywa kikanda ili kutoa nafasi kwa vijana kutoka mikoa yote kushiriki, kanda hizo zilikuwa katika Mikoa ya Zanzibar, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya

Baadaye mwezi Oktoba mwaka jana vijana 34 waliong’ara katika Kanda hizo waliweka kambi jijini Dar es Salaam lengo kuu likiwa ni kuwapata nyota watatu ambao miongoni ni Casto.


Mbali na Soka Vodacom Tanzania inadhamini michezo mbalimbali kama vile Tenisi, Riadha, Mbio za basikeli, Kuogelea, Golfu na Shindano la Vodacom Miss Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. umalize shughuli iliyokupeleka mdogo wangu urudi, usije kujilipua kama akina sie tuko tu huku tunalolifanya halieleweki, ilimradi tu kuwabana wazungu kwenye matrain yao...
    urudi chonde chonde,,sio ghafla tusikie uko sweden, mara umeonekana Holland, maana na huu muungano wa Schengen huu, ni balaaa..

    ReplyDelete
  2. Wow, welcome back the FULANAZ. Kumbe ziko nyingi tu niliona kwenye mnuso mmoja ze fulanaz ya rangi nyekundu.

    ReplyDelete
  3. MICHUZI YVONNE CHAKACHAKA YUPO TANZANIA MJINI MTWARA,WABANDIKIE WADAU MAMBO ALIO YAKUTA,YAPO KWENYE BLOG NYINGINE.

    ReplyDelete
  4. Ubelgiji kuna mpira gani jamani?
    Si wangempeleka Holland?

    ReplyDelete
  5. aisee vodacom kuna "position" za kazi adi rahaaaaaa

    safi sana tngenezeni ajira ya wabongo-naja muda si mrefu voda

    ReplyDelete
  6. Nawapongeza vodacom, lakini wiki mbili ni chache sana kwa kijana kujifunza, siku za usoni walau kijana akae miezi sita hadi mwaka hapo ndipo atakuwa ameiva kisawasawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...