Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania wote waishio katika jiji la Dallas na vitongoji vyake katika ibada maalumu ya PASAKA.
Hii ibada hii itafanyika katika ukumbi wa kanisa la Umoja International Outreach,kanisa linalosimamiwa na kuendesha na watanzania waishio hapa Dallas.Hii ni siku muhimu ambayo tungependa kuwaona ndugu zetu wote wakija kwa pamoja na kusherekea kufufuka kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Shughuli mbali mbali zitafanyika siku hiyo ikiwa ni pamoja na kuwabariki viongozi mbali mbali wa kanisa,kuwaombea watoto wote watakao kuwepo ibadani,kubariki couples,kupokea shukrani mbali mbali,na mambo mengine mengi.Baada ya ibada kutakuwa na kuburudika kwa chakula pamoja na vinywaji huku waimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili wakiwa wanamwimbia Mungu kwa shangwe na sifa.
Tunaomba kila moja atakae soma tangazo hili amkaribishe mwenzake.
Ibada itaanza saa kumi na moja na nusu.
Anuani;12727 Hillcrest Road
Dallas Texas,75230
simu ni 214 554 7381
Mungu awabariki sana.
Pastor Absalom Nasuwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...