ripota wa globu ya jamii leo katembelea ilipo kip-lefti iliyo karibu na twin tawazzz ya benki kuu na kukuta bado utepe haujakatwa na siku ya kufanya hivyo bado haijajulikana. akamsaka mhusika na mazungumzo yalikuwa hivi:

ripota: sh'kamoo mzee...

mhusika: marahaba kijana.  je, tukusaidie nini?

ripota: natoka globu ya jamii. ningependa kujua hii kip-lefti itafunguliwa lini?

mhusika: kwani vipi?

ripota: ah, nilitaka kujua tu ili nikaripoti maendeleo yake. maana redio mbao zimeshaanza kutoa ripoti za ajabu ajabu. zingine zinadai eti hili ni dili la kutaka kuingia nanihii kwa chini chini....

mhusika:  dah! mmeshaanza. sikiliza kijana. nyie msitake kuingilia kazi za watu. unajua hii sehemu si rahisi kuifanyia kazi kama unavyodhania. chini kuna mkondo wa maji, na inahitaaji utaalamu wa hali ya juu. hapa kwa saa moja tunatoa ndoo 56 za maji. hivi sasa inasubiriwa tume maalumu iliyoundwa itoe mwongozo kabla kazi haijakamilika. tumekonsalti mainjinia wa kijapani, kichina na wa kimatumbi, wote wametoa mapendekezo ambayo tume inayafanyia kazi. pendekezo litalofaa ndio litatekelezwa.

ripota: kwa hiyo tutegemee lini kazi hii itaisha?

mhusika: eeeeh, yu noo, hii kitu kinahitaji umakini wa hali ya juu maana sehemu hii ni nyeti sana sana kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi. hivyo haraka haraka haina baraka. njoo mwezi ujao tarehe kama ya leo utapata jibu.

ripota: yaani mkuu una maana nitapata jibu ya nini kitafanyika ama kazi itakuwa imemalizika?

mhusika: huna masikio nini wewe???? nimekwambia utapata jibu!!

ripota: sawa mkuu. nimekusikia. nitafika hapa mwezi ujao tarehe kama hii kupata jibu.....samahani kwa usumbufu.

mhusika: wasalimie. waambie libeneke linaendelea bado....


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ciao I write from Italy: it's really a pity that I don't understand kiswahili, I didn't have the opportunity to learn it, I was about to merry with a Zanzibarian... I love your country in fact my blog now talks about my trip in Tanzania and Zanzibar some years ago. It is written also in english if you want to have a look. Try to make some post in english too if you can!
    Many Greetings from Muzungumalaika!

    ReplyDelete
  2. heeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    1."mkondo wa maji??",
    2."wataalamu wa kijapan,kichina,kimatumbi?",
    3."mustakabali wa taifa?"
    4."tume husika?"

    siamini jicho langu,,,sijaelewa

    ReplyDelete
  3. JK kabadili wakuu wa wilaya Mikoa kwa madai ya kuchochea Maendeleo, Bongo TAMBARARE .

    ReplyDelete
  4. Bongo tupimwe ALCOHOL kabla ya kuanza kazi.Uhu ni ULEVI wa pombe.

    ReplyDelete
  5. Fransesca, I visited your blog and definetly you fell in love with Zanzibar and thank you for being an ambassador to that extent. However I do not get it when you wrote "I was about to merry with a zanzibarian ... " my guess is a typo mistake. Do visit zanibar again. Grazie segnorita

    ReplyDelete
  6. Hehehe
    funny lakini ndio majibu ya watumishi mawizarani yanavyokua. Kwa spidi hii mboni hizo flyovers zitatuangukia kwa wingi tu!!

    ReplyDelete
  7. Michuzi leo umenikwaza sana kaka. Yaani milipuko yote ile hujatushtua wenzako ni nini, sasa umefanya nimehangaika sana kupata habari. Nakushauri uweke namba yako ya simu ya kiganjani BAYANA ili tuweze kukupigia ili UTUHABARISHE au TUKUHABARISHE.

    Ahsante sana kaka

    ReplyDelete
  8. Wow, what a joke! Tume inaundwa ili kuziba pot hole? Kwa maana hiyo hawa watu wana maana kwamba wanautaalamu wa kuweza kujenga majengo makubwa namna hiyo juu ya mkondo wa maji bali kuziba shimo barabarani ni kazi ngumu inayotakiwa kuundiwa tume!! Guys, Tanzania is finished! Kwisha kabisa.

    ReplyDelete
  9. A HII NDIYO ARI MPYA KASI MPYA NA NGUVU MPYA
    ALUTA CONTINUA

    ReplyDelete
  10. Mzee wa KimaraApril 29, 2009

    Hapo ndipo watu tunaamua kutorudi bongo coz issue ndogo kama hiyo watu wanaweka usiku kinoma si bora mtu utumie ma high way ya Obama tu mitaa hii huku ukicheki ustaarabu mwingine!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...