Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Sema kp sema, usiogope sema!!! kila siku watawala wetu wanazunguka dunia nzima kuomba misaada, na wakirejea tukawatumbulia mimacho tu wanashangaa kwa nini hatuwapigii makofi kuwasifu kwa kazi nzuri wanayoifanya!!!!!

    ReplyDelete
  2. Mungu amuhurumie JK.
    Eti hatma ya nchi yetu iko mikononi mwa nchi za G20?

    Nina imani Mungu anajuta kutupa akili za kibinadamu na rasilimali zote tulizo nazo, ndo maana anatunyang'anya bila hata sisi wenyewe kujua. Kwani tunaowakaribisha wawekezaji ni sisi wenyewe na mikataba tunasaini wenyewe, wanachukua pesa zetu kisha tunaenda kuwaomba tena misaada. KUFRU.
    Naamini kuwa HATMA YA TANZANIA IKO MIKONONI MWA MWENYENZI MUNGU nasi tuna wajibu wa kuyatumia mawazo yetu vyema kujikomboa wenyewe, TUWE NA PLANS ZETU JINSI YA KUJIKWAMUA. ACHA KABISA KUTEGEMEA MWENZAKO MWENYE MATATIZO AKUPANGIE MIPANGO YAKO YA MAENDELEO.

    ReplyDelete
  3. KP hii imesimama sana tu. Mnase hicho kibao tena kiwe kikali kuliko kile kingine anaboa sana huyo jamani hata sijuwi Mungu anamwangaliaje?

    ReplyDelete
  4. Yani inatia hasira sana sana. Juzi ktk dr 1 Denmark walimuonyesha Ali Mfuruki akihojiwa na mwandishi wa Kidenish. Eti huyu Ali mfuruki anasema anaamini kwamba watanzania ipo siku watawauwa matajiri kwaajili ya corruption.Na yeye ni mshauri wa Jk kama sikosei.
    Mimi nadhani kama kweli ni mshauri basi wachukue tahadhari mapema kuwanusuru watanzania na janga la umasikini.
    1. Wapunguze bei/ushuru wa utalii ili kuvutia watalii nchini.
    2. Wapitie upya mikataba ya uwekezaji hasa ktk sekta ya madini.
    Tuna utajiri mwingi mno ila hatuufaidi wanaufaidi wageni na matokeo yake tunakuwa Matonya na tunasimangwa mno. Maana hiyo misaada tunapewa na kusimangwa.

    ReplyDelete
  5. Ajabu kabisa, `yabidi tujipige kibao' kwani macho tunayo, akili tunayo na mikono tunayo, lakini tumelala.
    Oh, labda Kipanya ungeongeza bomba kutoka kwenye bokisi la maliasili lielekealo kwa tunaowaomba misaada.
    M3

    ReplyDelete
  6. KAZI KWENU NDIO KWANZA RAIS WENU ANASEMA HATIMA YA WATANZANIA KUJIKWAMUA KIUCHUMI IKO MIKONONI MWA WA-WEST? NILIVYOSIKIA HIVYO NIKASEMA AMA KWELI NGOZI NYEUSI NI NYEUSI TU, KUOMBA MPAKA LINI, KWELI RAIS MZIMA UNASEMA HATIMA YA WANANCHI YAKO IKO MIKONONI MWA WENGINE! nO HATIMA YA WATANZANIA IKO MIKONONI MWA WATANZANIA FULL STOP.

    ReplyDelete
  7. Hata mimi sipendi utoaji wa Hutuba wa Mh. Rais hasa inapofika wakati anazungumzia hao Wazungu. Inaonekana kabisa anawanyenyeke sasa kama yeye ndio hivyo je huyo mwnanchi wa kawaida huko Ngara na Bariadi si atawaona hawa jamaa wazungu. Jiwe Jiwe tu bwana lazima tuwe maskini jehuri kwani hata wao walipitia huku na wakatoka bila msaada wa mtu. Kilichowatoa ni mali amabazo nyingi zilitoka kwetu sasa kama mali tunazo na watu wapo wa kufanya kazi kwanini tusikae tufikiria mipango madhubuti ta kujikwamua bila kuwajali hawa? Nchi kama Saudi Arabia na Africa Kusini ni mifano mizuri. Ipo hajaya kubadilika mh. Rais!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...