Kaka michuzi hapa kwetu hali ya uchumi ni mbaya tunajaribu kushukuru Nyama nayo imeshuka ila duka la nyama spellings zake hasa ni zipi?butcher au bucher naomba msaada pengine mimi ubongo umekaa mguu wa kushoto.
Mdau Musoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. mh! nyama bei ubwete hivyo. i wish ningekuwa naishi huko musoma

    ReplyDelete
  2. Mimi ninamsifu huyu aliyeandika kwakua amefikisha ujumbe kwa wanaofahamu English na Kiswahili!
    Watu kama hawa wanahitaji support.

    Nilikutana na mwandishi wa habari anaetoka Denmark, alinisimulia safari yake ya Tanzania miaka takriban 10 iliyopita, hakuwa anajua Kiswahili kabisa,alikua Posta Mpya na alitaka kula chips omlet kwa vijana wa mtaani. Alimuendea muuzaji na yule jamaa alichangamkia tenda na kwa uwezo wake wa lugha alimuuliza mzungu "chips egg far far or comfuse" yule mzungu alielewa na akamjibu "just mix all together". Yule mwandishi alimsifu yule kijana alivyoweza kutumia uwezo wake mdogo wa lugha ya kigeni katika biashara yake!

    ReplyDelete
  3. Spellings za duka la nyama kwa kiinglishi ni butcher tatizo ni kuwa huyu tajiri mwenye hili duka la nyama ameishi sana china ndio maana ameandika kiinglishi kwa kichina bucher
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  4. NENO BUCHER BINAFSI NALIONA HALINA TATIZO JAMANI, MANENO YALIONICHANGANYA NI "LOBO" NA "STECK"

    ReplyDelete
  5. KULINGANA NA KIWANGO CHA ELIMU ALIYOTUACHIA CHIFU WENU, HII NI SAWA TU. ZAIDI YA ROBO TATU YA KISWAHILI TUNACHOANDIKA NA KUONGEA NI MAKOSA MATUPU SASA TUKIANZA KUSAHIHISHA HILI HATUTAFANYA KAZI NYINGINE MWAKA MZIMA, TUKUBALIANE TU KUWA KILICHOANDIKWA HAPO NI SAHIHI KULINGANA NA ELIMU YETU. ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI, IDUMU CCM.

    ReplyDelete
  6. "Bucher" "Steck" "Lobo". Hii safi sana

    ReplyDelete
  7. yUKO SAWA TU

    ReplyDelete
  8. hii ndo bongo bwana kakosea sana tu baada ya robo kaandika lobo, even instead of steak yeye kaandika steck kaazi kwelikweli.

    ReplyDelete
  9. Bucher,steck ,lobo na trei. we anonymous wa April 01,2009 3:00PM naona kama vile ulisahau kidogo hiyo trei

    ReplyDelete
  10. pengine alitaka kuandika neno buthcer kama mdau mmoja alivyo sema. lakini hata hivyo neno butcher manake ni mtu anaye chinja wanyama (waliwao, mara nyingi mbuzi ng'ombe au kondoo, kukatakata, na kuuza.Hivyo butcher ni 'mtu' na si 'kitu'Kwa hali hiyo, haitakuwa sahihi kusema butcher ni duka la nyama.

    Pengine neno Butchery lingefaa zaidi katika muktadha huo.

    ReplyDelete
  11. Jina sahihi ni BUTCHERY, ukisema BUTCHER, huyo ni muuzaji ndani ya BUTCHERY.

    ReplyDelete
  12. HAhahahaha, Kuna mtu kanipasua mbavu hapa.... Ebwana asante kwa kichekecho mwanana... "chips egg far far or comfuse"....

    ReplyDelete
  13. JAMANI WADAU HII IKIWA NDIYO BEI YA NYAMA MSOMA KWA WAFUGAJI JE DAR NI KIASI GANI?
    NAOMBA MNIJIBU JAMANI KUMBE NYUMBANI VITU VIMEPANDA KIASI HIKI?
    KWELI HII IMENISIKITISHA

    ReplyDelete
  14. sisi ndiyo wa tz bwana mtizamo wetu siku zote ni kukosoa,kama uliona mapungufu hayo ya lugha uliweza, kupiga picha je ulifanya jitihada kuingia hapo na kumshauri kuandika lugha iliyo sahihi.

    ReplyDelete
  15. HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAAA.......aisee, saa zingine humu ni vichekesho tupu. Namfagilia Anony wa pili (2:35PM)...umenichekesha ile mbaya mwana..eti "chips egg far far or comfuse"..kazi kweli kweli!!!!

    ReplyDelete
  16. jamani wadau bei ya nyama dar ni kiassi gani??samahani kwa usumbufu ila nitashukuru sana

    ReplyDelete
  17. Anon wa April 01, 2009 4:45 PM

    Bei za nyama ya ng'ombe Dar es Salaam on average ziko hivi:

    Steak (yaani nyama isiyo na mifupa) ni Tshs. 6,000/- kilo moja.

    Mchanganyiko (yaani nyama yenye mifupa) ni Tshs. 5,000/- kilo.

    Utumbo ni Tshs. 4,000/- kwa kilo.

    Bei zinatofautiana kutegemea na eneo iliko bucha. Hii ni kwa sababu kodi za jengo zinatofautiana pia kutokana na eneo.

    Hizo nilizokupa ni bei za Magomeni. Ila ukienda Manzese au Kimara bei ni pungufu kwa Tshs. 1,000. Na ukienda Namanga, au Masaki utakuta bei ziko juu kwa Tshs. 1,000/- hadi 3,000/-

    Bei zilipanda haraka sana wakati ule mafuta yalipopanda maana gharama za kusafirisha ng'ombe zilipanda na kodi za majengo nazo zilipanda.

    ReplyDelete
  18. I like that far far or confused. Nimecheka saana. Jamani wabongo we are very smart basi tu

    ReplyDelete
  19. that wos really funny! 1/3 init spodse to be robo and not lobo lol, wot does myana mchanganyiko means? does it mean its veal , pork, goat lamd all mixed in 1?pls enlighten m e as im buffled!

    ReplyDelete
  20. ANONY WA APRIL 01,2009 9:37 PM.

    Aisee nashukuru sana kwa msaada wako, huwa naambiwa vitu vimepanda sikuelewa sasa nimeelewa

    ReplyDelete
  21. Da kweli tanzania bado sana. Ila sasa mashaka yangu yanakuja pale anaposema PAMOJA NA VIUNGO sijui ana maana gani? Na ni viungo vya hao wanyama ama? Maana sasa hivi tupo kwenye hali tata sana ndani ya nchi na ukizingatia Kura za Albino zinaendelea kule Mwanza.

    Naomba kuwasilisha ni mawazo tuu.

    Mdau Davey

    ReplyDelete
  22. NAKUBALIANA NA MDAU WA HAPO JUU KWAMBA BUTCHER SIO DUKA LA NNYAMA BALI MAANA YAKE NI MCHINJAJI, MUUZAJI AU MKATA NYAMA. PIA NENO BUTCHERY LINASIMAMA KAMA NOMINO YA KUCHINJA, YAANI UCHINJAJI. KWA KIINGEREZA SANIFU, DUKA LA NYAMA LAFAA KUITWA BUTCHER'S SHOP. KAMA KUNA MWENYE MAONI TOFAUTI ASEME.

    ReplyDelete
  23. hili ni duka la nyama la mbunge wa Musoma mjini(vedastus Mathayo Manyinyi)c c m tena ni msomi wa chuo kikuu na ndiye aliyeniandikia kikaratasi ili nimpe muandishi wa Kibao anakili sasa shida iko wapi Hapo na ukizingatia Ni Msomi mie ningefanyaje.

    ReplyDelete
  24. Naamini huyu mjasiriamali amefikisha ujumbe wake kwa wateja wake. Tumakosa tudogo tudogo huto hakampi hasara yeyote. Baada ya kubandika bango lake aligeuka nyuma na kujisemea kimoyomoyo "msg delivered" Vijiji vingine wanapiga ngoma tu, mbinja au makelele ili watu wafahamu leo wamechinja. Kwa hiyo huyu amepiga hatua kubwa sana. Iwapo akirekebisha spelling na grammer hakumwongezei kitu, bora aache hivyo hivyo. MSG DELIVERED & UNDERSTOOD.

    ReplyDelete
  25. naomba ufafanuzi tafadhali ati ni lobo au robo?

    ReplyDelete
  26. tanzania maisha ni magumu kweli, yaani nyama ni karibu dolllar 6 ,kwa kilo na watu wanalipwa kiasi gani cha mshahara ?niambie jamani nimetoka huko miaka 18 iliyopita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...