
Wakazi wa eneo la Misheni, nje kidogo ya mji wa morogoro, wakigombea mafuta yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye tenki lililoanguka mahali hapo wikiendi ilopita. Pamoja na kuwepo polisi wa usalama barabarani mmoja aliyekuwa akijitahidi kuwafukuza wakazi hao, wananchi walikuwa wabishi na kutoogopa lolote ambalo lingetokea pale.

Baada ya lori la mafuta kuacha tela lake likijiendesha lenyewe baada ya kuchomoka na kuingia porini, al manusra ifinyange finyage hii Escudo ilioacha njia kwa kulikwepa lile tela lililokuwa limesheheni mafuta ya taa

wadau wakiwahi mafuta ya dezo katika ajali hiyo!

Escudo lillilopone chupuchupu kusombwa na roli la mafuta lilolokuwa likienda adijojo
Polisi wa usalama barabarani akijaribu kukabiliana na na mmoja wa wakazi sehemu ya tukio tena kwa kwa usalama wao lakin walikuwa wabishi ile mbaya! Picha na habari na Michuzi Jnr
Ama kwa hakika "Sikio la kufa huwa halisikii dawa".
ReplyDeleteNi mara ngapi matukio ya ajali zinazotokana na moto wa mafuta ya gari zimeripotiwa Tanzania, Kenya na Nigeria na bado watu hawajifunzi?
Ni dharau ama habari haziwafikii ama maisha magumu haina haja ya kujali uhai tena?
Jameni, cheese ya bure ipo ktk mtego wa panya! Likilipuka hilo majeruhi na wafu kibao. Tuache kupenda vitu vya dezo
ReplyDeleteBlackmpingo
NI UGUMU WA MAISHA AU WANANCHI WAMEKATA TAMAA NA MAISHA?
ReplyDeleteAh ah ahhh mwenye kidumu haya mwenye kidebe haya hii ilikuwa taarifa ya masako baada ya tukio la watu kuungua na moto ktk staili kama hiyo kule mbeya,Watanzania tuepuke kukaribia maeneo kama hayo kwani ni hatari sana,halafu mkubwa hiyo gari ni PAJEO io sio ESCUDO BABA.
ReplyDeleteMdau JP
salama yao wote pamoja na askari wa usalama mara hii hakuwepo juha aliekimbilia mafuta huku akiwa na sigara mdomoni!!!!!!!!
ReplyDeleteHiyo ni dalili tosha ya maisha duni wanafahamu madhara yake ila wakale nini? maisha ya mtu masikini ni sawa na kifo kwa hiyo hawezi kufikiria ya kesho wakati ya sasa hayajui.
ReplyDeleteE bwana hiyo picha ya chini kabisa ya askari na msela imeniacha hoi sana.
ReplyDeleteUtafikiri muvi fulani vile.
Duh wabongo wabishi look the last pic haha itz not a funny but lazima utacheka..anyw hongera Michuzi Jr nimeona kipaji mkubwa hapo nimekupa CREDIT....
ReplyDeleteJAMANI VIJIJINI LAZIMA KUWEKA ELIMU KUHUSU GARI LIKIPINDUKA, NI MSAADA HASA PIA KUKAA NAKO MBALI INAWEZA KURIPUKA IKAUWA WATU WENGI KWANI, PIMBI MMOJA HANA AKILI ANAWEZA KUJA NA SIGARA HAPO HUKU NA DUMU LAKE. ELIMU SIO LAZIMA DARASANI KUONGELEA TU VIWANJANI. SIO LAZIMA MPAKA UONGEE KIENGEREZA.
ReplyDeletewakishaungua utasikia ooooh serikali haitujali!!!
ReplyDeleteserikali itakujali vip wakati mwenyewe hujijali????
si kwamba hawajui madhara yake,lkn hali ngumu ya maisha ndiyo inayofanya wananchi hao kutojali uhai wao.na kwa staili hiyo hata Mungu yuko tayari kuwasamehe.
ReplyDeleteinasikitisha sana kuona ni jinsi gani hali ya maisha ilivyo ngumu.there's no hope for tomorrow.
AFANDE MIDAKO
ReplyDeleteNI UGUMU WA MAISHA AU WANANCHI WAMEKATA TAMAA NA MAISHA?
Afande Midako,
Hapo hakuna ugumu wa maisha wala kukataa tamaa, bali ni ujinga uliokithiri.
Halafu maafa yakitokea tunailaumu serikali.
Ninawalaani vikali wale wote walikwenda pale kuchota mafuta kwani walihatarisha maisha yao. Ikibidi ninaziomba mamlaka husika ziwachukulie hatua kali wale wote ambao ushahidi wa wazi umeonekana wakiwa katika eneo la hatari.
Nadhani hii itasaidia kurudisha nidhani.
kufa kufaana
ReplyDeleteKwa hiyo Baba Ubaya kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu, tuhalalishe vibaka, wakabaji, wezi na wavunja sheria wengine?
ReplyDeleteMimi sikubaliani na wewe hata kidogo. Zamani tulikuwa tunasimuliwa kuwa enzi za ukoloni, wakoloni wakiwachapa watu bakora, nadhani ni watu kama hao. Sasa hivi hatuwezi kuwachapa bakora lakini ni muhimu hawa waliokwenda pale wakaadhibiwa vya kutosha ili iwe funzo kwa wengine.
Nidhamu hakuna kabisa!
Tanzania hiyo watu kama wanyama,kweli umasikini ni ushetani.
ReplyDeleteyaani roho za kufa bwana,hivi wamesahau ya kule mbeya jinsi walivyokufa shauri ya kufata mafuta? wanajua sana madhara yake basi tu ROHO ZA KUFA HIZO
ReplyDeleteUMASKINI GANI HUO WA KUHATARISHA MAISHA?
yaani roho za kufa bwana,hivi wamesahau ya kule mbeya jinsi walivyokufa shauri ya kufata mafuta? wanajua sana madhara yake basi tu ROHO ZA KUFA HIZO
ReplyDeleteUMASKINI GANI HUO WA KUHATARISHA MAISHA?
Suala sio umasikini. ni ujinga, ukosefu wa elimu na kutojitambua na mwisho kufuata mkondo. kama umasikini ndio unafanya uwe hivyo si tungesikia kila siku malori yanakwenda kuwamwaga watu baharini waliokata tamaa? au kwenye ajali za moto si ndio watu wangekuwa wanajitupa ili wafe? ni ujinga tu watu na wala serikali wasilaumiwe kwa jambo hili.
ReplyDelete