
Reginald Mengi

Yusuf Manji
A City businessman, Yusuf Manji has sued his long-time protagonist, IPP Executive Chairman Reginald Mengi and his Independent Television (ITV) Limited, demanding one shilling (1/-) compensation and apology for libel for brandishing him a ‘shark of corruption’ along with four other local businessmen.
Manji has filed his suit through Muganda, Kamugisha and Bwana Advocates’ law firm, ostensibly designed against the defendants at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar es Salaam.
Read more
Wana-Yanga wawili wameingia kuchegama.
ReplyDeleteHapo mtu ameshavuka mstari, ameputa mchanga na kutia dole. Tunausubiri mtanange kortini.
Hawa ni mahasimu wa jadi na wana makundi ya kishabiki ya kidni.
ReplyDeleteTegemeeni comenti za kidni au kikaburu(ubaguzi wa rangi) hapa.
1 Shilling! TZ ni corrupt, sio Asians tu. Tuache ubaguzi.
ReplyDeleteHaya aje mie nnayo.Mmh hili suala ni zito.Ukiliangalia kijuujuu utaona ni dogo ila ni kubwa.Siko upande wowote ila naona Mengi sio mwendawazimu kwenda kuropoka mbele ya waandishi wa habari ilhali anajua kama hana ushahidi ingemgharimu sana.Ila sijui inawezekana akawa anamuharibia but I dont think so.Langu jicho nasubiria machweo manake naona tumetoka mawio
ReplyDeleteBwana mdogo Manji kachemsha,pesa wanazogawa kwa wadau wake kwenye chaguzi sasa zinajionyesha .Utawajua kwa matamshi yao.
ReplyDeleteUsiibie maskini utaumbuka
How nice, he is fighting for principle and not the money.
ReplyDeleteHivi kwanini swala lolote linalohusu wa-TZ wenye asili ya Asia, ubaguzi hutumika kuua hoja! hivi huyo Mengi alisema neno lolote kuhusu rangi ya hao jamaa? je alisema hao jamaa si Wa-TZ? hiyi siasa za nchi hii zinaenda kubaya niliposikia Prof. Mapumba anasema ubaguzi sidhani kama ninaweza nikamuelewa tena kwake yeye kashfa itangazwe naye tu sio wengine swala la Rada, ndege ya raisi vilikuwa danganya toto nini leo hii mwingine anaongelea hilohilo anaambiwa anajipendekeza!
ReplyDeleteANGALIENI UFISADI MPAKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI,MENGI AMEKUA AKITUMIA VYOMBO VYAKE KUJITANGAZA NA KULINDA MASLAHI YAKE.
ReplyDeleteMAFISADI MENGI NA WAHINDI WANAGOMBA NIA KITOWEO(MNOFU) CHA WATANZANIA MASKINI WENYE NJAA.MUNGU WANGU TUTAKULA WAPI SISI WALALA HOI MAANA MIFISADI HAITOSHEKI TU.
MENGI ANATUDANGANYA WATANZANIA HOHE HAE KULINDA MASLAHI BINAFSI KWA KUTUMIA UZALENDO HIVI SISI WAZALENDO WA KWELI AMBAO NI MASKINI TUKIAMBIA KEMPISKY INAUZWA TUTAWEZA KWELI KUINUNUA?ZAIDI YA YEYE KUFAIDIKA PEKE YAKE?
MENGI NA WAHINDI MSITUZINGUE
Suala la Mengi na Rostamu laibukia bungeni
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuwa makini katika matumizi ya vyombo vya habari pamoja na mambo yao, akisema matumizi mabaya yataiingiza nchi katika migogoro.
Pinda alisema hayo jana wakati kipindi cha maswali ya papo kwa papo cha kila Alhamisi ambacho msimamizi huyo mkuu wa shughuli za serikali Bungeni hukitumia kujibu maswali mbalimbali ya wawakilishi hao wa wananchi.
Alikuwa akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Hamad Rashidi Mohamed, aliyetaka kujua ni hatua zipi zitachukuliwa kwa mtu anayetumia vyombo vya habari kwa manufaa yake binafsi.
“Mheshimiwa waziri mkuu, naomba kuuliza. Katika kutekeleza sera ya utawala bora, je ni halali kwa mmiliki wa chombo cha habari kutumia chombo chake kwa ajili ya kuwashutumu watu wengine,” aliuliza Rashidi na kutaka kujua msimamo wa serikali.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema jukumu la mtu aliyekashifiwa kupitia vyombo vya habari kuamua cha kufanya ni lake mwenyewe na kwamba anaweza kwenda mahakamani au anaweza kunyamaza na kusamehe.
Alisema Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeshaliona hilo na itachukua hatua stahiki kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo.
Waziri Mkuu pia alisema suala la mtu kumiliki vyombo vya habari na kutumia vyombo hivyo kwa kuwakashifu watu wengine halipendezi na halitavumiliwa hata kidogo.
Suala hilo la matumizi mabaya ya vyombo vya habari limetinga Bungeni wakati kukiwa na mjadala mkali juu ya kitendo cha mfanyabiashara Regnald Mengi kutangaza hadharani watu watano aliowatuhumu kuwa ni mafisadi, akiwabatiza jina la 'mafisadi papa' na kuitaka serikali iwachukulie hatua.
Kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki magazeti, television na radio, kimetafsiriwa na aliowatuhumu na watu wengine kuwa ni kutumia vibaya vyombo vyake vya habari, baadhi wakihoji sababu za kutowapa fursa watuhumiwa hao kujibu kama maadili ya uandishi yanavyotaka.
Tayari watu wawili kati ya watano waliotajwa wamechukua hatua dhidi ya kitendo cha Mengi, baada ya mfanyabiashara Yusuf Manji kufungua kesi akidai fidia ya Sh1 kwa kukashifiwa na Rostam Aziz kutoa saa 24 kwa Mengi ili amsafishe kabla ya kuchukua hatua za kisheria.
Mjadala huo wa kitendo cha Mengi pia uliendelea nje ya Bunge, baada ya viongozi wa umoja wa vijana wa CCM mkoani Tabora kujitokeza jijini Dar es salaam na kumtaka mfanyabiashara huyo awaombe radhi kwa kumchafua mbunge wao wa jimbo la Igunga, Rostam.
Nora Damian anaripoti kuwa mwenyekiti wa umoja huo, Robert Kamoga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) Mengi alipaswa kupeleka ushahidi, kushtaki au kufungua kesi dhidi ya mtu yeyote anayehujumu taifa na si kuwahukumu watu hadharani.
Alidai kuwa Rostam ni msafi kwa kuwa hajafikishwa kwenye chochote cha sheria na kwamba bado ni mtuhumiwa.
“Tunaiomba serikali iangilie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kusababisha mtikisiko mkubwa kwenye nchi,” alisema Kamoga.
Alidai kuwa kauli za Mengi zinatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza
Maneno ya Mengi ni matusi ya hadharani. Ametumia media yake kusambaza chuki kwa kikundi fulani achohisi yeye binafsi na washirika wake hakiwapendezi.
ReplyDeleteHaiingii akilini mtu kama yeye kuongelea watu wenye kesi mahakamani na kuwahukumu. Tusipoangalia tutazidi kuwa na utawala wa majungu na fitna kuliko utawala wa sheria. Mengi amechemsha na sheria ni msumeno. Kwanini haukati? Nini adhabu ya "Contempt Of Court"? Nini adhabu ya kutukana hadharani?
Hawa watani wa jadi, Lakini mimi nahisi Bwana Mengi anakaroho ka kwa nini? Kwa sababu in most cases yeye huwa anaanzisha hizo chokochoko! Manji si mwanasiasa na wala hatuna haja ya kujua pesa zake anapata wapi! Kama anatumiwa na mafisadi walioko serikalini bila shaka tukishawadhibiti wao hata yeye utakuwa mwisho wako! Ila huyu Mengi ni too much pride, He always want to be the last man standing! Una bore!
ReplyDeleteHAKUNA MJADALA
ReplyDeleteMAFISADI WADOGO, WAKUBWA WOTE WAACHE.
MENGI SIO MSAFI NA ASIWE WA KWANZA KURUSHA JIWE
NA HAO TUMEWASIKIA KILA LEO KATIKA KESI ZA UFISADI
ACHENI RUSHWA KWA KILA LEVEL HADI POLISI NK
Manji is very smart man 1/= Tanzania shilling ni matusi makubwa kwa mengi ....but apology is what he wanted not money from Mangi.
ReplyDeleteKitendo cha Manji kudemand shilling moja ya kitanzania kutoka kwa mengi ni tusi kubwa kuliko tusi la mapapa, ni kumfanya mengi kuwa kama mlala hoi, na maskini wa mawazo (kumbuka hata wewe unaweza kutoa shilling moja) he made mengi to look stupid mbele ya publicity
Sikilizeni Hapo Mengi Lazima apelekwe mahakamani Sababu yeye akiambiwa FIsadi anakuja Juu Ilawenzake amewasema kama ni Mafisadi-PAPA Sio Kitu cha busara kabisa Pesa Sio kitu anataka kumuonesha tu alichofanya ni Kosa. Mengi kuwa na Busara au utakuja kujiharibia Jina.
ReplyDeleteBwana mengi angeshauriwa kuacha siasa kwa wanasiasa vinginevyo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wake.
ReplyDeleteHUU NI UKWELI KABISA ,MENGI NDIO ANAHAANZISHA UGOMVI NA HAWA WATU ALIEWATAJA ,KWANZA TUANZE NA MANJI .YEYE MWENYEWE MENGI ALIAAZISHA SWALA LA NSSF,HAA HUYU MWIZI KAAIBA HELA ZA NSSF,POLISI WAKONA HAKUNA HAJA ZA UPELEZI KWA MANJI, MAANA MANJI HAWEZI KWENDA KWENYE MAJENGO YA NSSF KUIBA HATI NA KUHAMISHA JINA LAKE, NIKITU HAKIWEZIKANI KABISA ILA KUNA UTARATIBU WA KIABIASHARA, HALAFU HAWA JAMAA WENGINE ALIOWATAJA PAMOJA NA MANJI UTAKUTA NDIO WAFADHILI WA CCM WENGINE WAPO BUNGENI ,NDIO WANAOJULIKANA SANA KWENYE FANI YA SIASA NA MICHEZO, HUYU MENGI YEYE KWENYE MISIBA, PARTY, MAHARUSI NA MIALIKO YA WAGENI WA KISERIKALI. SASA UTAKUTA WATU WANAFWATILIA SANA MICHEZO NA SIASA YA VYAMA. YEYE MENGI HAJIUSHISHI NDIO UTAKUTA HAJULIKANI KAMA HAWA NDIO MAANA INAMUMA SANA
ReplyDeletemengi wala hajakosea kama mtanzania aliyeguswa na jambo lolote ana haki ya kuliongea kama katiba inavyosema sasa ni juu ya hao walioguswa ama kujibu ama kutojibu ama kusamehe lakini pia ni kwenda mahakamani kushtaki sasa hapo ubaya wa mengi upo wapi. wengi mnamhukumu eti anatumia vyombo vyake vibaya si kweli mlitegemea akatumie vyombo vya habari vya rostam? mbona hata rostam anatumia vibaya vyombo vyake mfano jinsi alivyomuandika vibaya mwakyembe. angalieni mambo yanaendaje
ReplyDeletewe unaesema lipumba ameingiza ubaguzi unakichaa,kwani hadi mengi ataje rangi ndo utajua mbaguzi,wewe huoni statement za mengi ni za kibaguzi,kasema mafisadi papa tz ni kumi,lakini kataja watano tu,na wote wahindi,tena wafanyabiashara enzake,wewe unategemea nini,mengi ni mbinafsi,na anatumiwa na chadema kwa upande wa pili,wewe tangu umjue mengi umeshasikia amegombana na watu wangapi,ngoja nikutajie wachache tu kuanzia 2005,manji,adam malima,ramadhan dau wa nssf,masha,rostam,jetuu patel,acha huko nyuma ndo usiseme.na saa hivi amanfisia kikwete na kumkandia mkapa,kama sio unafiki ni nini,2015 si atarudi kumtukana tena JK.sema watz tumeamka atawadanganya hao hao wajinga.
ReplyDeleteMimi siko upande wowote ktk issue hii kwa kuwa sina ushahidi wowote ila naona Mengi hajafanya kosa kuwataja hao aliowataja kuwa ni mafisadi papa, hayo ni mawazo na mtazamo wake na sidhani kuwa ameamua tu kuropoka eti kwa kuwa ametumia vyombo vyake kwani bila shaka alijua kuwa atapata reaction toka upande wa hao aliowataja kwani nao si watu wadogo. Wote tunajua kuwa nchi yetu ina mafisadi wengi tu kwa sasa, yeye ameamua kuwataja baadhi yao (kwa jinsi ajuavyo yeye) kwa kuwa ana nafasi ya kufanya hivyo. Sisi walala hoi hatuna sauti, nani atatusikia? Nafikiri hao waliotajwa watachukua hatua za kisheria kama wanaona iko haja ya kufanya hivyo.
ReplyDeleteIVI NYIE APO JUU???
ReplyDeleteMTU AKIONGEA OOOH NA YEYEY ANA MADHAMBI,AKINYAMAZA OOH MICHUZI MBBONA HABARI ZA MAFISADI ZIMEPOA?
IVI TUTAKUA WAOGA NA WANAFIKI,WAZINDIKI IVI ADI LINI NYIE WADANGANYIKA?NCHI INALIWA SAAAANA NA TUNAJUA,NA WANAOKULA NI NANI?MCHWA?WADUDU?? SII WATU NDO WANAKULA TENA WACHACHE SANA!!
IVI SEMENI MWANASIASA GANI (walio wengi)ATASIMAMA KUSEMEA ILI SUALA LA MAFISADI?MANA WEEENGI "wamefadhiliwa na ufisadi" MANA NAPO ISINGEKUA MAGAZETI YALIPOKOMALIA TOKA KITAMBO HUU WIZI SI YANGEPITA TU TUNGEPATA WAPI??????mengi kasema lake na ni sahihi kabisaaaa usahidi atatoa!!ni heri kuliko nyie mnaolowa tuuu afu mwapiga kelele pembeni weee na bado mwaliwa.ata mama kilango anasema sana tu kwa uchungu mwingi ila afanyeje yupo ktk hilo CHAMA!!
KUNA WATU WASHENZI SANA KTK HII NCHI,YAN KUNA MAJANGILI ASWAA WANATAFUNA HII NCHI.
yani adi kieleweke kabisa,msituletee upupu "\\|>&&#**& wenu apa MAPAPA
michu bandika hii
ona comments za wengi hapa, halafu mkiambiwa kuwa watanzania niwabaguzi mnalalama!!!!
ReplyDeleteMENGI NAYE, SIMUELEWI KWANI YEYE NI NANI MPAKA ANAROPOKA HIVYO, DOLA SI IPO ITAFANYA KAZI YAKE, SHIDA YA MENGI NI MASWALA YA PESA/BIASHARA AKIPIGWA GOLI LA KISIGINO BASI TABU.
ReplyDeletewatanzania inasikitisha mgali mmelala kutokana na mamneno hayo juu.
ReplyDeleteukweli ni kwamba rushwa tanzania inamkabili kila mmoja na viongozi hawana mapenzi na nchi.
cha msingi wananchi muwe watu wa kufikiria sana na kuto nunuliwa na pesa. watanzania wengi ni watu wa kununuliwa kwa pesa na hii ndio inaipa nguvu rushwa na wengi kupata taabu.
watanzania tufauate mwendo wa usa tuchague kiongozi mwenye uchungu na siyo kwa ajili ya pesa.
chukulia vyama vingi vya siasa kiongozi anachaguliwa na chama hii ni kosa kubwa na ndio maana kiongozi anakuwa hajali maslihi ya wananchi badala yake anajali maslahi ya chama.
chukulia CCM NEC ndiyo inampitisha diwani au mbunge na siyo wananchi sasa hapa haki itapatikana wapi jamani?.
wananchi ni muhimu kuamka na kupiga mambo kama haya na kubadilisha kiongozi achaguliwe na wanachi.hiki kiwe kitu cha kwanza.
utumizi wa magazeti binafsi hakika hii inafanywa na viongozi wote wa serikali maana wote wamo katika biashara na siyo rostom pekee.
wafanya biashara na serikali wanatumia mbinu za kutoa habari dhidi ya adui yake na hii hakika siyo mangi wala rostom ni mtindo unaotumika tanzania.
kukomesha hayo ni watanzania kuamka na kubadilika.
rushwa tanzania imekuwa ndio biashara kubwa kuanzia chini hadi juu.
ushauri wangu tusiwe na kasumba za chama tuchague watu watakao leta maendeleo na sheria nyingi zibadilishwe ili zilete watu wa maana, maana kwa sasa pesa ndiyo inachagua viongozi hii ipigwe vita watanzania.
jamani tusiwe na tamaa za kidunia kwa muda maana tukipata kiongozi mzuri yote yatakuja bila rushwa amen.
inashangaza na kutia uchungu sana kuona watanzania jinsi tunavyohalalisha kuibiwa,hapo mengi katoa maneno ambayo natumai ushahidi anao na anajua anachosema.sasa sie tunaobisha hapo juu hatuelewi kweli hao wote waliotajwa kama ni mashina ya ufisadi?na jeuri wanaypo kwani wao hiyo ccm kwao iko kiganjani watafanya lolote wanalotaka na hata machafuko yakitokea usidhani kama tutawaona hapo tz mi yangu macho,najua mengi hiyo fidia hatatoa na kinachokuja ni kwamba atazidi kusema zaidi madhambi ya hao jamaa,na hao viajana sijui kutoka igunga eti wanamtetea rostam mweeh rushwa hizi,haya tuendeleze libeneke
ReplyDelete