YU WAPI MWALIMU INNOCENTUS ALHAMIS?

Hellow Brother Michu
NAOMBA NAFASI KWENYE BLOG YAKO KUULIZIA ALIPO MHESHIMIWA MMOJA. BWANA NINASHIDA KUJUA ALIKO NDUGU INNOCENTUS ALHAMIS.

 HUYU JAMAA ALIKUWA MWALIMU WA CHUO KIKUU HURIA CHA HAPA BONGO NA ALIKUWA MWALIMU WANGU NILIPOKUWA NIKISOMA PALE. KWAKWELI HUYU JAMAA ALIKUWA NI KICHWA KWELIKWELI NA MSAADA MKUBWA SANA KWA WANAFUNZI (NITAUNGWA MKONO NA KILA ALIYESOMA PALE NA ALIBAHATIKA KUKUTANA NA HUYU JAMAA). 

NILIPATA HABARI KWAMBA ALIKWENDA KUSOMA JAPAN KIPINDI FULANI HIVI NA ALIPORUDI SIKUWEZA KUMWONA. NILIJITAHIDI NIONANE NA YEYE LAKINI NIKAAMBIWA ALIONDOKA KWENDA KUCHUKUA NONDO YA PHD MAREKANI TANGIA MIAKA YA 2001 AMA 2002 HIVI. 

HADI WA LEO SIJAWAHI KUSIKIA HABARI ZAKE NA NINA HAMU SANA KUMWONA NIMPE SHUKURANI ZANGU ZA DHATI KWA MSADA ALIONIPA NIKIWA MWANAFUNZI. NILIKUWA MBUMBUMBU KWELI WA HISABATI LAKINI JAMAA ALINIPELEKESHA KWA DESIGN YA AJABU NA NIKAWA KIPANGA WA HISABATI. NI WENGI WANAMSIFIA SANA KWA HILI ENEO NA TABIA YAKE ISIYOFANANIA TABIA ZA MA LECTURER WA
 KIBONGO. 

NILIBAHATIKA KUKIPATA KITABU CHAKE KIMOJA ALICHOANDIKA CHA RESERCH METHODOLOGY NA NILIFURAHI SANA KUKITUMIA KWENYE MASTERS YANGU. KITABU CHKE HIKI NI KIZURI ASIKWAMBIE MTU NA KWAKWELI KILINISAIDIA SANA KWENYE MASTERS YANGU. WASIWASI WANGU NI KUWA ISIJE AMEAMUA KUKIMBIA NCHI AMA AMEIBIWA NA WENYE KUJUA MANUFAA YA VICHWA KAMA YEYE KWANI TUTAKUWA TUMEIBIWA PROFESSOR MAKINI SANA.

NITANGULIZE SHUKURANI ZA DHATI KWA YEYOTE ATAKAYE NISAIDIA KUMPATA HUYU LECTURER.
WASALAM
MR. MTEI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Open University of Tanzania imemnyanyasa sana huyo jamaa. Majungu, fitina ndio vilivyomkimbiza Alhamis Open University. Alhamis yupo Marekani.

    ReplyDelete
  2. Flora KitaliApril 07, 2009

    Mdau, wasiliana na Dr Hildebrand shayo wa UK, ninafahamu fika kuwa hawa ndugu wanawasiliana na ataweza kukupatia number yake ya simu na e mail

    e mail ya Dr shayo ni shayoh@lsbu.ac.uk

    Hivi ni vichwa ambavyo taifa linapoteza!

    ReplyDelete
  3. waweza kumgoogle ama nenda kwenye sites zifuatazo:http://www.ratemyprofessors.com/ShowRatings.jsp?tid=1002993

    http://www.ace.coop/portals/0/institute/05/ca.pdf
    na nyinginezo
    Inaonekana kweli lijamaa ni poa kichizi. Sijui kama limezamia ama vipi lakini majuu wanamtumia kama ulivyosema ni hazina tosha
    Sunday Maneno

    ReplyDelete
  4. Unanifanya na mimi nimkumbuke mwalimu wangu wa 1986, 1987 - 1990 na 1991-1992 aliyenifanya nipende na nimudu hisabati, huyu si mwingine ni MR. NDOMONDO wa Shaaban Robert, nahiki ni kichwa kilichojificha pale shuleni.
    Mwalimu Upoooooooo?!

    ReplyDelete
  5. ebwana msaidieni jamaa watu ambao mna connection na INNO!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...