USIWE NA HOFU YA KUIBIWA GARI LAKO TENA! 
 TUMIA NJIA HII. KWA MSAADA ZAIDI TUWASILIANE 
MDAU Rhxoqsa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Gari hilo linaibiwa na nyoka pia anaibiwa, wewe unacheza na wezi!

    ReplyDelete
  2. Ulinzi wa Gari tosha huo. sema wa Swahili wataalamu kila njia watatumia atachoka nyoka mwenyewe tu na mwenye Gari.

    ReplyDelete
  3. Hiyo sio dawa ya wezi,nyoka anauwawa na gari linekwenda pia.uncheza na wezi nini wewe!!nadhani huyo nyoka sio wa kweli ni toy tuu!WEZI MSIJALI NI LIPLASTIKI TUU HILOO

    ReplyDelete
  4. Hata kama ni joka la ukweli hapo unahitaji mafuta ya taa au bakora tu. Ukitaka ulinzi wa kweli wa asili ingia Sumbawanga...au Mlingotini, Bagamoyo.

    ReplyDelete
  5. utakosa demu ukitembea na Nyoka kwenye gari wewe.

    ReplyDelete
  6. Hivi huko hakuna WATANI zangu WASUKUMA? Maana wao wanajua kucheza na nyoka.Kama walivyosema hao waliotangulia,kwa Wezi waliokubuhu hapo gari linaibwa na Nyoka anaibwa.We Mdau wa kwanza nyoosha Kiswahili chako.Ukisema Gari 'linaibiwa' umeemaanisha kitu kingine kabisa,yaani kifaa cha gari(mfano Kioo) kinaibwa.Pia Nyoka 'aibiwe' ana nini cha kuibiwa? Ingekupasa useme Nyoka anaibwa.Sitakuwa Adui kwa kutoa Mchango wangu ktk kusaidia kuiendeleza Lugha yetu adhimu ya KISWAHILI,maana Waswahili wanasema 'NYEGE NI KUNYEGEZANA! Wasalam.
    THE KOP
    ST-JEAN
    CANADA

    ReplyDelete
  7. Mdau KOP ST jean! ashakumsi matusi yakhe, msamiati ulioutumia hapa nahisi kama ni mkali sana, unaonaje ungemwabia kuwa waswahili walisema "KUPOTEA NJIA NDIO KUJUA NJIA?" sihitaji vita nawe ni katika kuboresha lugha tauria/lugha laini/lugha murua

    Bibi wa Bule kwa Kidensi.

    ReplyDelete
  8. Kwa hapa jijini inaweza ikawa msaada lakini usukumani ndio kwanza umewapa wezi wa huko sababu zaidi ya kulivunja gari lako. Maana usukumani chatu nae ni dili!

    ReplyDelete
  9. Hivi kweli jamani kwa joto lote la Bongo unategemea huyo nyoka atakaa hapo kwenye kioo hata kwa nusu saa?. Fumbo mfumbie mjinga mwizi ataling'amua

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  10. Tena nimekumbuka. Hilo gari ukienda nalo maeneo yenye wataalam (Sumbawanga, usukumani, Bagamoyo, etc.)watakugeuzia kibao. Watasema "huyu mtoto anajifanya anajua sio, ngoja tumjaribu". Hilo plastiki lako linageuzwa nyoka wa kweli halafu huo muziki wake atakaokuanzishia humo ndani, kama hukulitupa hilo gari mtaloni basi utachomoka mwenyewe huku gari likiwa speed 80kph.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  11. Bibi wa Bule,mi ni mtoto ambaye nimetoka ktk familia ya waungwana wa Pwani wanaojua Kiswahili vizuri,hivyo huwa naogopa KUTUKANA lakini siogopi KUTUKANWA! Hakuna Tusi hapo ndo maana NANIHII hakusita kunirusha Hewani,waulize wanaojua wakufahamishe.Kidumu KISWAHILI!
    THE KOP
    ST-JEAN
    CANADA

    ReplyDelete
  12. Rhoxoqsa ndugu yangu asante kwa mtazamo wako,ila huyo chatu sio dawa ya kuzuia gari lako lisiibiwe,mfano nakuja nafungua kioo kisha namwaga mafuta ya taa nakwambia atanipisha mwenyewe na kuondoka nalo kilaini,kwanza na yeye chatu dili vile vile namuiba pamoja na gari yako kisha nakwenda kumuuza kwa wadua wahusika naye
    mdau Baraka

    ReplyDelete
  13. wizi wa kweli wanamuiba uyo nyoka alaf wanakuachia gari yako, so siku ya pili utatafuta chengine cha kuweka, kila ikiwa tabu kuiba wao ndo wanafrahia

    ReplyDelete
  14. Ukinyunyiza mafuta ya taa humo kwenye gari huyo nyoka atatafuta mwenyewe upenyo wa kutokea...!!

    ReplyDelete
  15. Weweeee, kwa taarifa yako, huyo nyoka wako watu wanampika supu wanakunywa hapohapo, na Gari wanachukua. So Don't try that at home (TZ).

    ReplyDelete
  16. Bora weka simba au mbwa wataogopa huyo nyoka watu wanafungua mlango na atatoka mwenyewe gari hilooo kwa upoleeeeeee

    ReplyDelete
  17. Mdau kila la kheri katika jitihada zako za kulinda chako. Lakini huyo fashisti, nduli, dikteta usimfungie vioo la sivyo utamwua kwa joto. Na hapo bongo si nasikia Wachina kibao?, basi angalia usijemkuta mshikaji yuko kwenye sahani dining!!

    Mdau, Boston, US.

    ReplyDelete
  18. VOODOO!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...