Nani alikwambia Kuwa Ukerewe (Kisiwa kinachoongoza kwa kuwa na Maprofesa wengi nchini) hakina Ghorofa? angalia mwenyewe jengo hili ambalo mkandarasi wake ni Mzawa na mzalendo, lipo wilayani Ukerewe katika Kisiwa kidogo cha Ukara. Na Mdau Frederick M. Katulanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nadhani hii ni aidia/ wazo zuri sana endapo hii ghorofa ingetengenezwa kwa unadhifu ingevutia sana, ingawa ni tope tupu, nadhani angepata mkandarasi mzuri angeiboresha kidogo kwa kutumia vitendea kazi na malighafi hiyohiyo aliyotumia,kwa kweli hapo ni hesabu hazikupigwa sawa kidogo tu ingevutia sana, huu ni ubunifu wa bei rahisi sana kuwa na kagorofa hata sisi wa vijijini.

    ReplyDelete
  2. Aminia,si mchezo babaake.

    ReplyDelete
  3. Kuna UK mbili tu duniani...UNITED KINGDOM na UKEREWE. hizi hazitofautiani ki maendeleo.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  4. maprofesa wengi so what? nini wamefanya? Zaidi ni ufisadi tu.

    ReplyDelete
  5. HIYO ROSHENI HATA KWA DAWA SIKAI....LINAWEZA GEUKA KABURI GHAFLA!

    ReplyDelete
  6. Ya,kutembea lazima unyate!!

    ReplyDelete
  7. UKILA SAMAKI KWA WINGI LAZIMA UTAKUWA NA AKILI NYINGI, BABA MAMA WANATAKIWA KULA SAMAKI KWA WINGI WANAPOTAFUTA MTOTO, NA MAMA AENDELEE KULA SAMAKI KWA WINGI AKIWA NA MIMBA, MTOTO AKISALIWA PIA ALE SAMAKI KWA WINGI NA ANYONYE MAZIWA YA MAMA MTOTO LAZIMA ATAKUWA BUNDI/KIPANGA/KICHWA HII IMETAFITIWA NA WANASAYANSI NA NI KWELI KULA SAMAKI KUNAJENGA UBONGO

    ReplyDelete
  8. jamani hawa wakerewe kwao kuna maendeo gani? mbona umasikini ndio kwao. kama hao maprofesa wao wangelikua na akili nyingi si wangegundua njia za kupunguza umasikini kwao? pengine uprofesa wao ni wa kubeba mabriefcase peke yake. mimi naona iyo gorofa ni kichekesho tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...