MDAU WA SWEDEN

KAKA MICHU NAOMBA UNIPE NAFASI YAKUWATAKIA PASAKA NJEMA WALOKOLE WENZANGU DUNIANI KOTE HASA WAPENDWA WA KANISA LA UBUNGO KWA PASTOR GWAJIMA NA WEWE PIA.

  PIA NAOMBA NISEME MACHACHE JUU YA ILE MADA YA DNA KAKA.MIMI KAMA MLOKOLE NASIKITIKA KWANI HAIMPENDEZI MUNGU KUSALITI NDOA ZETU HADI KUFIKIA KUBAMBIKIZIANA WATOTO.ILA KILICHONISIKITISHA ZAIDI NI BAADHI YA COMMENTS ZA KINA BABA ZILIZOJAA DHARAU NA MTAZAMO POTOFU JUU YETU KINA MAMA.SHUTUMA NYINGI ZILIZOTOLEWA DHIDI YA KINA MAMA SI ZA KWELI KWANI HAZIJACHIMBUA KIINI CHA KWANINI WANAWAKE WANAOCHEAT WANACHEAT.

     NI WAKATI SASA KWA WANAUME KUKUBALI KUA HAMNA TOFAUTI YEYOTE KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME LABDA NI MISULI TU NDIO MWANAMKE KANYIMWA NA HAINA UMUHIMU WOWOTE KTK KULETA MAENDELEO KWANI KWAKUTUMIA AKILI TU HATA MWANAMKE ANAWEZA KUPASUA MWAMBA BILA KUA NA HIYO MISULI.

  UBONGO WA MWANAMKE NA MWANAUME HAUNA TOFAUTI YEYOTE KIBAIOLOGIA NA KWA MAANA HIYO KAMA MWANAUME AMEOA MWANAMKE MJINGA BASI ASISEME  MKEWE MJINGA SBB NI MWANAMKE BALI ASEME NI MJINGA KWAKUA AMEZALIWA MJINGA KWANI PIA WAPO KINA BABA WAJINGA.

    KUNA WANAWAKE WENGI SANA WENYE AKILI NA WAMEFANYA MAKUBWA YA MANUFAA HAPA DUNIANI.CHUKULIA MF. KINA MAMA WANAOLEA WATOTO BILA MSAADA WA BABA HADI WANAKUA HALAFU MTU ANASEMA WANAWAKE NI WAVIVU JAMANI.MAHOUSEWIVES WANAZARAULIWA LKN KAZI WAFANYAZO HAMNA MWANAUME AMBAYE ATAWEZA HATA BONY MWAITEGE ALIKIRI HILO.

  YULE ALOSEMA WANAWAKE WAKI WEST WAKICHEAT WANACONFESS NDIO LKN NA WAUME ZAO WANAWASAMEHE SASA WEWE MBONGO MKEO AKIKIRI KUA KATEMBEA NJE YA NDOA UTAMSAMEHE?

       NDO MANA NIKASEMA WANAUME HAWATUJUI , UNAPOISHI NA MWANAMKE ANA AKILI LKN WEWE UNAMUONA AAAH HANA AKILI SI DEMU TU NA MADEMU HAWANA AKILI UNAFIKIRI UTAMJUA?

    NDO MAANA WANAUME WANAPOTEZA CONFIDENCY MBELE YA MWANAMKE MWENYE MALI NYINGI KUWASHINDA NA NDIO UTAKUTA WANABAKIA KUSEMA OOH MWANAMKE MWENYE MALI ANA KIBURI BLA BLA ZARAU SI KWELI NI KWA VILE MNAFIKIRI  MWANAMKE HAWEZI KUFANYA MAMBO YAKIMAENDELEO KUWAPITA.

    ANYWAY MADA NI NDEFU LKN MNAICOMPLICATE KINA BABA KWAKUMKANDAMIZIA MWANAMKE KILA UCHAFU UTOKEAO KTK JAMII LKN MKIKUBALI KUA TUKO SAWA PATAKUA NA MAENDELEO SANA KTK JAMII HASA HUKO KWETU BONGO.

            MUNGU AWABARIKI WOTE NA TUITUMIE PASAKA HII KUPUNGUZA MATENDO YETU MAOVU.
          -MDAU WA  SWEDEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. Ndiyo wanawake wengi ni waongo wanazaa nje halafu wanazaa nje halafu wanakuja kubambikiza wanaume watoto.Hasa hasa wanawake wasio na mwelekeo maishani wakiona dume mwenye uwezo au anatoka ktk familia nzuri na wametembea naye ndo kinakuwa chanzo.
    By the way ww dada bora hata usingekuja kuongea mambo ya Mungu halafu ukamuorodhesha huyo mchungaji Gwajima humu.Biblia inasema siku za mwisho patakuwa na manabii wa uongo,wachungaji FEKI wanaopenda pesa,nafsi zao, mali kuliko kumpenda Mungu.Siku hizi nimechoka hii mirurundiko ya makanisa yanayodai ni ya kiroho wakati ni uongo mtupu. Huyo GWajima ni mmoja ya wale wanaojifanya wanafanya miujiza ya kufufua watu wakati ni uongo mtupu.Mchungaji gani ni mdhulumaji nasema hivi sababu ni kweli kashatudhulumu pesa za gari letu.Mungu anamsubiri kumchoma yule mchungaji.

    ReplyDelete
  2. Heri ya Pasaka na wewe pia!

    Dada mpendwa hapo juu, sidhani kuwa wanaume na wanawake wako sawa...hiyo tu ya mmoja kuitwa mwanamke na mwingine kuitwa mwanaume ni tofauti.

    Pili sijawahi kusikia mwanaume aliyembambikia mke wake mtoto ambaye si wake.....ila mwanamke ndiye mara nyingi anamdanganya mmewe kuwa huyu ni mtoto wake wakati siyo...hii ni tofauti nyingine.

    Hizo akili unazolinganisha, sidhani kuwa katika hili la DNA lina mantiki yoyote...na kwa kifupi nadhani unazidi kumkandamiza mwanamke mwenzako, mimi sidhani pamoja na cheating zote kuwa mwanamke ambaye hajui hata aliyempamimba kuwa anauwezo mzuri wa kufikiria...najua akili anazo, lakini lazima ukili kuwa linapofikia suala la uangalifu anajisahau...hiyo nitakubali.

    Ila kuhusu suala zima la cheating, mimi kwa upande wa maoni yangu nadhani kiasi cha wanawake na wanaume kucheatiana kimahesabu na katika logic ya utambuzi nadhani wote ni sawa kwa sababu multiplier effect ya cheating iko pale pale kwani wanaume wanaocheat huenda kulala na wanawake wanaocheat, kwa hiyo uwiano wa cheating lazima kwa mahesabu ya kawaida utalingana mfano wanaume sita watakaocheat wake zao watenda kulala na wanawake sita waliocheat waume zao, hivyo uwiano wa cheating nadhani tukitumia commonsense utabalance.....hii inaweza kuwa tofauti kama any cheater atalala na kiumbe mwingine zaidi ya binadamu..au mwenye jinsia sawa...ambazo hizi ni zile tunazoziweka kwenye other factors remain constant.

    Kuhusu maada yako nilitegemea advocacy yako ingefocus kwenye suala la kumuogopa mungu kama makanisa ulidai kuhudhuria yanavyofundisha...lakini hata kama utatumia hiyo global thinking yako (ambayo kwa upande wangu nadhani ndiyo itakayokuangamiza), hii naona kwamba msg yako haijakazania hata kidogo maandiko ya vitabu vitakatifu, mimi nadhani utabakia na global thinking yako ambayo nasikitika kusema kwamba...inaweza kujeopardise hata maandiko unayoyajua.

    Kibiolojia naamini mwanamke pengine yuko multitasked kuliko mwanaume....lakini hii haiondoi tofauti zao kwani ni tofauti nyingine tuliyonayo.

    If we don't learn to celebrate our differences i'm sure hata shule zetu hizi zitakuwa hazina option zaidi ya kutufrustrate.

    ReplyDelete
  3. Mama born again unachosema ni kweli, wote ni binadamu, lakini mmoja ni mwanamke na mwingine ni mwanamume kama ulivyowatambua katika hoja yako na hiyo ndio tofauti ya msingi - tuweke kado siasa na mantiki za kidini - ukweli ni kwamba hata siku moja mwanamume hatakuwa mwanamke na mwanamke hatakuwa mwanamume labda hadi siku Yesu atakaporejea tena - PASAKA NJEMA

    ReplyDelete
  4. Dada anaonekana mkali!! Nadhani dhumuni la hiyo picha lilikuwa kupozi kama modo. Enewei,

    Ana point za kweli lakini.

    Mi mwanasaikolojia naona wazi huyu dada emeshapata "rabsha" za mapenzi na ana kahasira fulani hivi -- labda ndo maana "kaokoka" -- watu hawaokoki hivi hivi tu!.

    Tupo wanaume wengi tu tunaotambua na kukubaliana na aliyosema sister. Tatizo wanaume walio tofauti na maoni yako ndo wanakuwa na sauti juu kwenye board kama hizi na hivyo wengi wenu wadada kuchukulia kwamba waume wote kimsingi tunapinga maoni kama ya huyu dada. Hata hivyo wanawake wengi mna yenu makuu na wanaume kama mimi tunaokubaliana nanyi ndo kwanza mnatunyeaga vichwani -- si tunaonyesha veli wikinesi zetu sasa? Ni kitendawili my dear!!!

    ReplyDelete
  5. NILIPOONA TU PICHA YA HUYU DADA NILIHISI KWAMBA NI ARROGANT, NILIPOSOMA NIKAPATA USHAHIDI.

    DADA NGOJA NIKUSAIDIE KIDOGO, MUNGU ALIPOUMBA MWANAUME NA MWANAMKE, ALITOFAUTISHA VEMA KABISA. KINACHOTAKIWA NI WATU KUTOKUTUMIA HIYO TOFAUTI KWA MABAYA, BALI WATUMIE KWA MAZURI.

    SI KWELI KWAMBA TOFAUTI NI MISULI TU. SI KWELI KWAMBA KIBAIOLOJIA HAKUNA TOFAUTI. PENGINE UNA TATIZO LA KUWA NA ELIMU NDOGO YA KIBONGO.

    UMEWAHI KUSIKIA KITU KINAITWA HORMONES KWA KIZUNGU? WATU WA JINSIA MBILI HAWALINGANI KWA KITU HIKI. TAFUTA VITABU USOME.

    PIA, WANAWAKE HUUNDWA NA CHROMOSOMES ZA X-X WAKATI WANAUME NI X-Y. UNAFIKIRI HIVI VITU NI SAWA?

    NISIMALIZE NAFASI YA WENGINE, LA MSINGI HATUTAKI UBABAISHAJI HAPA. WANALIOTOA MAONI WANAWEZA KUWA WALIPITILIZA, LAKINI UKWELI UNABAKI PALE PALE, KWA SAMPULI ILE NI WAZI KWAMBA WANAWAKE WANA TATIZO. SANA SANA LABDA TUSEME KWAMBA NA WANAUME NAO WANA MATATIZO, KWAMBA KWA NINI WALITEMBEA NA WANAWAKE WALIOOLEWA? LAKINI TUKUMBUKE KUWA MWANAMKE ANA UAMUZI WA MWISHO NA KAMA HAKATAI ASIKWEPE LAWAMA.

    MADUME TUMEUMBWA KUTAWANYA MBEGU, NDIYO ASILI YETU, NINYI MADEMU TUKWEPENI YAISHE.

    ReplyDelete
  6. DADA UMEOKOKA LINI?
    UMEZUNGUMZA MAMBO MENGI KIDOGO NIDHANI YOOTE ULIYOYASEMA UNAMAANISHA ILA NINASITA KUAMINI HIYVO KWANI ATA WEWE UMEMKOSOA MUNGU KWA KUFANYA TREATMENT YA NYWELE ZAKO, JIREKEBISHE WEWE KWANZA NDO UFIKILIE KUASA AU KUKOSOA WENGINE

    ReplyDelete
  7. Dada Mdau wa Sweden,

    Samahani, maada sio ndefu, wala haiko complicated.

    Naona wewe ndio unataka kuicomplicate.

    Naomba nikurudishe kwenye mada. Kati ya couples 250 waliopimwa DNA 150 wamegundulika kwamba wanalea watoto ambao sio wao.

    Hivyo basi katika kudraw conclusions ndio debate imeanza. Kwamba sample ni ndogo hivyo tusigeneralize.

    Lakini watafiti wanasema "biased sample is better than no sample at all"

    Na hoja nyingine ni kwamba hao waliokwenda kupima tayari walikuwa na mashaka na hao watoto.

    Hilo hatujui. Kwenye article hawajasema hivyo. Lakini anyway let's give them the benefit of the doubt.

    Hivyo basi concluasion sahihi na iwe:

    "Nchini Tanzania mwanaume ukihisi kwamba mtoto si wako kuna uwezekano wa 60% kwamba uko sahihi"

    Suala la kwa nini wanawake wanacheat, etc liko nje ya hoja.

    NAMBA MBILI: Wanawake kubambikia wanaume kesi za ubakaji.

    Kwa hili sample ilikuwa ndogo zaidi (watu 31 tu) lakini matokeo yalikuwa ni balaa.

    Watu 30 kati ya 31 walibambikiwa kesi za ubakaji.

    Sasa dada yangu mdau wa Swedeni, kesi ya kubaka hapa Bongo adhabu yake ni mvua 30.

    Hao wanawake 30 wanaotaka wenzao wakasote jela kwa miaka 30 sijui tuwaiteje?

    Hivyo katika kesi za ubakaji kuna umuhimu wa sheria kurekebishwa kwamba mtuhumiwa asihukumiwe mpaka ushahidi wa DNA utakapokamilika.

    ReplyDelete
  8. Wanawasema tu wanawake lakini wabaya ni haoa hao wanaume waliooa na ndoa zaoa hawazijali bali kufuata watoto wa watu. Kaka yangu alibambikiziwa mtoto hivi hivi. Kaka yangu alivyokua form VI girlfriend wake yeye alikua form III wanakutana tu Xmas. Kumbe yule msichana alikua anatembea na mume wa mtu tena. Kuja kupata mimba kasema ya bro. Bro ikabidi alazimishwe kuoa na baba wa yule msichana. Akaacha malengo yake yote ya kusoma college ikabidi atunze mke na mtoto. Wamekuja kuzaa watoto wawili tena na kaka yangu. I hope ni wakwake hao. Lakini toka alivyozaliwa huyu wa kwanza mama yangu kumwona akasema huyu si wetu. Nobody believed her. Baada ya miaka 9 anakuja kumwambia ukweli kuwa mtoto si wake. Ati anasema niliogopa kumwambia yule baba kwa vile alikua na mke wake na familia yake.

    sasa hao waliopima DNA na kuona kuwa watoto sio wao watafute baba za haoa watoto waone ni nani....watakuta ni wanaume za watu wenye ndoa zao mafisadi wakubwa wa ndoa zao.halafu mnakuja kulaumu wanawake hapa. Most of the time mtoto asiye wa ndani kwa mwanamke ni mtoto wa kwanza....lakini kwa wanaume utakuta watoto wa nje wadogo kuliko wa kwake wa ndoa ....how comes ....get real people

    ReplyDelete
  9. KAMTUI KATIMAUZZApril 12, 2009

    VILKEN DUM DU?KWANZA AHSANTE KWA SALAM ZA PASAKA ALAFU UNAJUA AU ULIKISOMA ULICHOANDIKA?UNGEKUWA MWELEVU USINGE WASHAMBULIA WANAUME KWA MTAZAMO WAKO BAALI UNGEJARIBU KUWAWEKA SAWA NA NINI WAFANYE LINI NA WAPI IKIWA NYUMBANI NA HATA KWENYE MKUSANYIKO WAKO,WENGI NYINYI MLIOTEMBEA KATIKA NCHI YA SWEDEN MNATAZAMO MWANAMKE NA MWANAUME SAWA KWA KILA KITU JAPO WEWE UMESEMA MWANAMKE HANA MISULI SASA UJUI HADI HAPO KUNA TOFAUTI,MWANAMKE USHIKA UJAUZITI MIEZI TISA NA MUNGU KUMAJALIA KUJIFUNGUA MTOT SASA UTANAMBIA KUNA USAWA NA MWANAUME WE SI KENGE KWELI,TUAMBIE KUH ULOKOLE NDIO UKO SAWA KATI YA MKE NA MME,MIMI NAMUESHIMU NA KUMKUBALI MWANAMKE MAMMA AU DADA OR SHANGAZI ANASTAILI HESHIMA YAKE YA PEKEE SI KWA LENGINE
    NAJUA BAADHI WATAKAO SOMA MAONI YANGU WATACHUKIA WENGINE KWAO ITAKUWA POA LAKINI MSG SAND
    WENU MDAU WA OSLO KAMTUI KATIMAUZII

    ReplyDelete
  10. Nakubaliana na dada katika kipengele alichosema kuwa kwanini watu wanacheat? moja kati ya hayo ni kutokuwa na uwazi ndani ya ndowa kwani jamii ya kibongo leo imekuwa na mchanganyiko wa madili ya kiwest na ya afrika sasa inapokuja mambo ya kiwest unakuta kunaupungufu wa mambo fulanii yanakwepa wakati wa kitendo cha (Honeymoon)kwa mfano mara nyingi msichana wa kiwest ni jambo la kawaida kwao kumueleza mvulana wake nini anapenda afanyiwe wakati wakiwa ndani ya Bustania ya (honemoon) na hilo haliwi tatizo kwa mvulana kumkamilishia mpenzi wake, lakini inapofika hali kama hiyo kwa sisi wabongo tunaojaribu kufuata mambo ya kiwest inakuwa mbine pale msichana aposema anataka afanyiwe jambo fulani mara nyingi wavulana wa kibongo huja juu na kumwita msichana majina machafu ya kila aina sasa msichana kama huyo mara nyingi huwa yumo katika hali ngumu kwa kukosa kile anacho kihisi kinamridhisha ndani ya moyo wake inapofika mambo ya kupokea raha za (kitam tam chamwili)pia inapokuja kwa wavulana wenye kupenda mambo ya kiwest hupendezewa wasichana wao wafanye mambo karibu na yale yanayofanywa na wasichana wa kiwest na akikosa hapo ndio hutafuta upande mwingine kukidhi fantasi zake watu wa west wana spices nyingi inapofika shughuli za (Honeymoon)kuanzia kivazi na vingine havitajiki hapa kutokana na madili ya MTZ lamwisho na himiza dada zetu usafi ni muhimu na hapa nikisema usafi sio kuoga tu lakini pia manukato kama mtu wa hina kidogo au hizi rangi za kucha vipodozi na kama huna uwezo wa manukato japo poda inasaidia manukato halisi hayo wanja unatakiwa uwe (wild cat) ukiwa ndani ya bustani ya Adam na Hawa.

    ReplyDelete
  11. Mimi nataka niseme kidogo na wewe kaka yako aliyebambikizwa mtoto hapo lawama ni ya nani?msichana alijua ana mpenzi wake tena wakiwa wote bado wanasoma lakini akaona kuwa hawezi kuvumilia wamalize masomo waanze maisha yao,
    tamaa ikamwingia ya chips kuku sim nzuri akaamua kutafuta mume wa mtu na ndio matokeo yake hayo baada ya kupata mimba kamtafuta mnyonge wake akampa.
    Wmimi bado naona kuna umuhimu wa wanawake kujishughulisha hiyo ni muhimu sana sisi tuliotoka nje ya nchi tunapata tabu kukopi na maisha ya huku sababu huku bwana ukishaoa mambo ni kuchangia kila mtu anaweka kipato chake cha mwezi mezani mnafanya hesabu kidogo inaleta maendeleo na mtu hana muda wa kucheat sababu anajua ana familia na inamtegemea na ikitokea bahati mbaya basi hapo lazima ukweli uchukue nafasi yake.
    jamani watanzania tupeane mapenzi ya kweli na kuambiana nini unataka kwa mwenzio na mambo yatakuwa shwari.
    mdau jp

    ReplyDelete
  12. lakini je ningependa kuzungumza juu ya utafiti au data zilizowakilishwa na ofisi husika, asilimia hiyo sidhani kama inawakilisha ndoa ambazo zipo katika maelewano inawezekana ni watu wenye matatizo ya kifamilia, ndoa zenye migogoro hivyo wanavyokuwa na kesi na migongano inapelekea kufikia uamuzi wa kupima DNA kuhakiki watoto, kama ni hivyo basi hiyo asilimia ilitegemewa maana ni ndoa ambazo zipo katika migogoro, ila nataraji kama utafiti utafanywa kwa ndoa amabzo si zenye migogoro asilimia haitokuwa hiyo, kwa hiyo hii si sababu ya kufanya watu wawe na wasiwasi wa familia zao, ingetakiwa iandikwe kuwa kama ni utafiti je ulikuwa ni random au ni kuwalenga watu wenye kundi fulani,

    mdau sverige!

    ReplyDelete
  13. Da Chemi naye ana yake. Mtazamo tu!: http://swahilitime.blogspot.com/2009/04/dna-test-bongo-matokeo-yanatisha.html
    “DNA Test Bongo - Matokeo Yanatisha!
    Jamani, mimi ni mmoja wa wale waliopigania testi ya DNA iwepo Bongo. Nilitaka iwepo kwa sababu akina baba wengi walikuwa wanatupa watoto wakidai si wao. Nilisema kuwa kama testi kama hiyo ingekuwepo ingeondoa hofu. Watu walikuwa wanasema tungoje kuona kama mtoto anafanana na baba yake. Hiyo haitoshi maana mtoto anaweza kufanana na mama yake.

    Sasa maabara ya mkemia mkuu Tanzania anasema kuwa karibu asilimia sitini ya sampuli testi zilithibitisha kuwa watoto si wa baba zao! Mmmhh! Kwa kweli hiyo takwimu inatisha na zinasikitisha.

    Akina dada wengi hawaelewi biology ya uzazi. Kitu kikuu ni kuwa mbegu inaweza kukaa ukeni siku tatu. Hivyo mtu anadhani akitembea na mtu mwingine siku fulani na mume wake siku nyingine mimba itaiingia ya mume. Ni ushamba.

    Pia kuna kesi za mapacha ambazo wamegundua kila pacha ana baba yake! Mnafanya mchezo na shahawa! Hata jamaa akimwaga nje mimba unaweza kupata! Mbegu zinakimbia! “

    ReplyDelete
  14. HEEEE....KUMBE HATA WABEBA BOX WAKIKE WAPO....!!!!!???
    Mdau vumbini

    ReplyDelete
  15. hiyo radi ya dubai hapo juu naona imemfikia huyo mdada .Pole !!!

    ReplyDelete
  16. Yaani Mnajadiliana Kuhusu ZINAA! Ama Kweli Dunia Inaisha.... Hakuna Majibu ya sawa sawa kama kila mtu anaona anahitaji haki flani katika Nyumba yake na Haipati... Jiulize kwa nini Umeoa??.. Kama Jibu si Kujiepusha na ZINAA na Kumuogopa MUNGU basi ndoa Yako Kila siku itakuwa na MATATA. Huo ndio msingi Thabiti na Dawa ya kutocheat, Mkiwa mnamuogopa Mungu, mtavumiliana, mtatimiziana, Mtaheshimiana na kila sifa njema Itakuwepo Ndoani, Lakini mkiwa ndani ya Nyumba Moja kisa fulani ana ngozi ya aina fulani na mwili wa namna Hii, nampenda huku hamuheshimiani na hakuna marejeo ya kuwafanya Muwe na Muongozo sahihi basi mmekwenda na Maji, (Marejeo yaani Sababu Kubwa iwe ni Ridhaa ya Mungu)
    NB: Mzinifu Hutembea na Wazinifu wenzie, Na waadilifu hubaki na waadilifu wenzao.

    ReplyDelete
  17. pole dada kwa hiyo radi hapo juu!!!!!

    ReplyDelete
  18. Mdau JP big up, naiunga mkono sentensi yahi hii, naku-quote "jamani watanzania tupeane mapenzi ya kweli na kuambiana nini unataka kwa mwenzio na mambo yatakuwa shwari."

    Tukizingatia hili, kila kitu kitaenda sawa, I am trying to do so with my wife, namuomba Mungu aendelee kunipa moyo huu huu na ampe mwenzangu na nyie wote pia.
    Pasaka njema

    ReplyDelete
  19. MIEZI MIWILI ILYOPITA HAPA UK WALI PUBLISH KUWA KUNA DADA ALIJIFUNGUA MTOTO WAKATI YEYE NA BOY FRIEND WAKE WANA CHINI YA MIAKA 15,IKAWA KAMA NI RECORD HAPA UK,MAGAZETINI NA TV ZILIKUWA KAMA NDIO BREAKING NEWS!BAADA YA WIKI KUPITA KUNA VIJANA WAKAJITOKEZA HADHARANI NA KUSEMA KUWA MTOTO NI WAO,FAMILIA ZIKAAMUA KUPIMA DNA,KUMBE IKAGUNDULIKA KUWA MTOTO SIO WA YULE ALIYESINGIZIWA!YANI MIMI ILINIUMA SANAAAA!NILI IMAGINE KAMA NIMEFANYIWA MIMI AISEEE!SIJUI YULE KIJANA MDOGO ALIJISIKIAJE?MANAKE KILA GAZETI ALISHATOLEWA AMEMBEBA MWANAE AMBAYE AMEBAMBIKIZWA NA HUYO DADA!!

    ReplyDelete
  20. Mwanamke na mwanamme wako sawa kiroho. Kibailojia, kisociolojia, ki...jia wako tofauti.

    Kimsingi hamana justification ya kucheat.

    Kama kweli wewe ni mlokole basi hujui hukumu za Mungu, mtu hatasamehewa kosa ya uzinzi eti kwa sababu mme wake hafanyi mara tano kwa usiku, na yeye alikuwa na hamu kubwa. Alitakiwa ajizuie na atumie akili kutatua tatizo kwa njia inayompendeza Mungu.

    ReplyDelete
  21. Kimsingi mtoa mada anaonyesha kuwa "strong feminist."

    Justification za kucheat zote ni excuse na mbinu na hadaa za shetani.

    Kwa Mungu, hakuna justification ya kucheat whatsoever.

    Mleta mada ana inferiority complex, kwa sababu great women wako respected na recognized na hamna mtu anawadharau.

    Wanawake hudharauliwa wale wanaoshea uswahili na upuuzi nk. kama figa moja halibebi safuria.

    Wewe unaotetea madhambi pia kuna uwezekano ukawa mdhambi rohoni hata kama hutendi. Kwa nini husaidii kukemea madhambi na kusaidia kuondoa cheating bali unataka kuleta feminist fealings kuwa kama wakimtamani jamaa basi waonje.

    Kuwa "feminist sio solusheni"

    ReplyDelete
  22. all in all wanaume wametuonea sana,wangekua na wao wanapata mimba basi hosp zingejaa na kukosa nafasi kwa jinsi ambayo wangepata mimba,hapo ndio wanaume wamepatikana dada amezungungumzi ni kwa nini wanawake wana cheat,ni matatizo ndani ya noda wanaume walianza na wanawake wamejionea sasa imetosha utachea na mimi nita cheat ndo maana unaona hizo DNA watoto wengi wa nje imefika wakati wanawake uvumilivyo walionao umewashinda,wanaume wakibadilika basi wanawake hawata cheat,wanaume wanadharau sana wanawake wakishawaweka nje wanadhani ndio kila kila.imefika wakati wanawake wamedhindwa uvumilivu!hiyo ndio adabu yetu wanaume na sisi vile tumezidi

    ReplyDelete
  23. Cheating is even too much for divorce.

    Utasikia "I accept your appology babe but we still are divorcing."

    Msamaha ni ili usiadhibiwe, talaka si adhabu bali njia ya amani ya kutengana ikiwa watu wanafanya umalaya ndoani. wawe huru ili kila mtu awe na furaha siyo

    " getting people trapped and stuck in this whole marriage thing on religious pretexts."

    ReplyDelete
  24. Kosa ni la waume kuto-match wakati wanaowa.

    Msichana amesha kuwa "dirt and filthy" (kwa saifa kimagharibi) sasa we jamaa utaweza wapi "oral" na "kugeuza samaki"?

    Mwache akapate nje kama alivyosema anon wa April 12, 2009 9:53 AM.

    We pweza kantia uchefu ije "oral ?" Sisi waume wa afrika wasafi bwana.

    ReplyDelete
  25. Dada hapa anatetea watu wacheat ili baadaye wapate kuokoka.

    Hakuna anayeokoka bila madhambi mazito.

    Wasiotenda dhambi hawahitaji kuokoka.

    Mungu ni wa haki hatomwadhibu mtu kwa dhambi ya mzaziwe au dnuguye.

    ReplyDelete
  26. Dada samahani, mbona sura yako inasomeka kuwa una hasira na unaweza ukawa unasumbuliwa na mawazo kwa nini maumbile ya mwanamke na mwanaume ni tofauti.

    Jibu: mapenzi ya Mungu.

    Usawa uko kiroho na kiuchumi basi.

    ReplyDelete
  27. Waongo wakubwa, wanabambika watoto na kesi za ubakaji.

    ReplyDelete
  28. Kama ma-sister wanajizuia ngono kwa nini nyie mnasema hamwezi?

    Mkubali nyie ni wadhambi na msisingizie maumbile maana wake na waume wako sawa kiroho.

    ReplyDelete
  29. Hii conclusion ina make sense: "Nchini Tanzania mwanaume ukihisi kwamba mtoto si wako kuna uwezekano wa 60% kwamba uko sahihi".
    Nimefurahishwa sana na hii mada. Baada ya conclusion ya hapo juu, bado ni kosa la mwanaume anayesingiziwa kwamba mambo yote hayo yametokea. Halafu mnashangaa kwa nini tunasita kuwaendea uchumvini...

    ReplyDelete
  30. Hongera mama kwa kujitoa kimasomaso kwenye hii mada nzito, sema mama sema usiogope.Wanaume wa Bongo wengi ni tatizo(siyo wote lakini-baadhi yao),hawaheshimu ndoa zao,ni visingizio tu, nyumba haziangaliwi, mama ni wa kulaumiwa,kusemwa kwenye vikao vwa bia,Mara nyingi wanaume huwa hawaoni mchango wa akina mama katika maisha; kosa dogo tu we! mazuri yote aliyotendewa baba yanafunikwa na kale kaubaya kamoja tu;utadhani yeye mwenyewe huwa hakosei,kumbe ukilinganisha makosa,utakuta ya baba yamezidi.Ni kutafuta visingizio tu vwa kutoka nje ya ndoa zao.Na utakuta mara nyingi mwanamume akitaka kumuacha mke wake tu basi, atapakwa mama wa watu huyo!ili mradi amchafulie kweli kweli,ili a-"justify" yeye kutembea nje au kuoa tena.Tabia mbaya hiyo!! Baba akiwa na hela nyumbani hakai, ni kutunga safari kila siku na kurudi nyumbani usiku wa manane,lakini ngoja aishiwe,ni wa nyumbani.Huu ni ushamba!karne ya 21 lazima iende na mambo mapya.We maisha kila siku hivyo hivyo hambadiliki.Upendo lazima umpe mkeo,Mama lazima umjali; leo hii wakianza wa nje kukusaidia unaanza ooh,mke wangu siku hizi muhuni, sijui nini.Nyie wakina baba wenye tabia hii ni lazima mbadilike.Hivi hamuelewi kwamba dunia ya sasa imebadilika sana na inatisha,utakutana na mwanamke mzuri,unaamua kuisaliti ndoa yako;mdada anakupa mapenzi motomoto, we unajiona umepata kumbe ndugu yangu umepatikana,anaweza kuwa Jini huyo wewe hujui;baadae unaanza kuandamwa na mikosi,hujui kwa nini.Badilikeni

    ReplyDelete
  31. mimi nilipata wasiwasi wa ulokole wa huyu dada. ama ni kutoelewa maana yake. mbali na mywele pia alitoa laana ktk maoni huko mwanzo. inaonekana ana hasira, au frustration au kumbukumbu ya hili.

    kuwa mpole dada. jadili bila jazba. utaumia bure.

    ReplyDelete
  32. Kina baba mdau wa Sweden kawatoa jasho, ona mnavyojikanyagakanyaga na maoni. Dada wa Sweden umejaaliwa busara, mungu akubariki.

    ReplyDelete
  33. Mmezidi kuwasema wanawake. Lamsingi Wanawake tujikomboe na tujitambue kwa kusoma sana na kufanyakazi yaani kuwa nakipato ili tuweze kusimama kwa miguu yetu hapo mwanaume hawezi kutuchezea.

    Wanawake wengi wanapata shida kusikiliza ukiritimba wa wanaume ambao kwa sasa hauna maana, wao wanajidai ndo watafutaji na ndo ``last say`` .

    Hayo yote yanatokea sababu wanawake nao wamechoka kwa mateso wanayo yapata hasa mwanaume kuisusa nyumba, unadhani mwanamke nae hatamani? Ndo maana nae anapata nafasi yakutafuta pakupumzikia.

    Jamani kuna mambo mengi yanayotisha katika ndoa/familia, milango tu ndo inayojua siri zote.

    ReplyDelete
  34. Wanawake wengi wa Tanzania hawafai na mtu ambaye ataamua kuoa mwanamke wa kitanzania ajue kwamba huyo mwanamke ana mabwana zaidi ya 20 pembeni na ujiandae kwa hilo. Mtoa mada umejitahidi kadri ya uwezo wako kutetea ufedhuli huu unaofanywa na mademu wa kitanzania, inawezekana kabisa wewe nawe ni mmoja wao katika kundi la hao wanao-cheat left and right.

    Tatizo kubwa la wanawake wa kitanzania ni uwongo, yaani wanaongopa kupita kiasi ili uwaone ni watu wa maana kumbe ni cheaters tu, wako tayari wakuambukize STDs na AIDS ili tu afiche uchafu wake wa ku-cheat na usimpige chini. Sifa moja ambayo wanawake wa kitanzania wamepewa ni urahisi wao, kuna rafiki yangu mmoja wa Afrika Magharibi aliwahi kuniambia hajawahi kuona wanawake rahisi kuwapata kama wa kitanzania, akasema kabisa hawana "NO" yaani ukimfuata anakubali muda huo huo na ukimfuata rafiki yake nae atakukubalia bila ya matatizo. Kwa hiyo unaweza kukuta mtu mmoja ametoka na wanawake marafiki wa kitanzania kama 6 au 7. Hii ni habari ya kweli.

    Ushauri wangu ni kuwa wanawake wa Tanzania ni waongo, hawafai, chaters, wanaweza kukupa STDs na AIDS na watakubambikia mtoto kwa hiyo achana nao.

    ReplyDelete
  35. Unaweza ukasoma, ukawa na mali, na vyeo, lakini kama hujarekebisha tabia utabaki yuleyule mjinga au bitch.

    Dawa ni kuwa na tabia nzuri siyo hela wala cheo.

    Ukombozi mzuri ni mabadiliko ya kitabia.

    ReplyDelete
  36. kina babaz bwanahhh mnatumia MISULI hadi ktk kuongea.dada wa watu kasema hakuna BIOLOGICAL DIFFERENCE KATI YA BABAZ AND MAMAZ BRAIN!Nyie mwaanza kutaja sijui hormones sijui xy+xx.acheni kutuma comments zakuatack kisa tu aliyesema hayo ni mwanamke.wengi mmecoment nje ya point japo rohon mwenu mwajua kasema kweli lkn kukiri mwaona vigumu kisa ni MWANAMKE.

    ReplyDelete
  37. Kwani we dada umeshatembea na wakaka wangapi bila ndoa?

    ReplyDelete
  38. Kimsingi 60% ni "bambikia rate", cheating rate is even higher.

    Watu waliocheat na wasipate mimba kwa ujanja au kondomu ni wengi mno.

    Mshichana TYPICAL wa bongo anaolewa akiwa amekwenada na wakaka kama 20 hivi halafu ana-maintain mafiga kadhaa baada ya ndoa.

    Kwa waliokoka ndo zaidi maana idadi inatisha mpaka inabidi aokoke kushawishi jamii kama kawa msafi.

    Maana kama mtu si mdhambi utamshawishi vipi atue mizigo asiyonayo, atakwambia sina mizigo au mizigo yangu myepesi naweza kuibeba mwenyewe sihitaji msaidizi.

    ReplyDelete
  39. Katika wote waliotoa maoni huyu aliyesema haya ndo KANENA:

    "Cheating is even too much for divorce.

    Utasikia "I accept your appology babe but we still are divorcing."

    Msamaha ni ili usiadhibiwe, talaka si adhabu bali njia ya amani ya kutengana ikiwa watu wanafanya umalaya ndoani. wawe huru ili kila mtu awe na furaha siyo

    " getting people trapped and stuck in this whole marriage thing on religious pretexts."

    WE NDO MTU. Na mi karibu tu nampiga chini wakwangu -- na sirudi. Ameashalia na kubembeleza sana lakini its too late. Na hao bwana zake washamtosa tayari anyway.

    ReplyDelete
  40. Dada, kwa nini kuitwa wanawake mafisadi kunakuumiza kuliko ufisadi wao hao wanawake?

    ReplyDelete
  41. Bora ndoa ivunjike kuliko kufanya utundu ulozidi mipaka.

    Chumvi na kisanvu siyo mboga kabisa.

    Mmesahau watu wa Lutw/Lutwi/Lot?

    ReplyDelete
  42. Kama kutunza ndoa kunahitaji watu watalii mitaa ya SODOMA na GOMORA basi ndoa yangu wacha iishe.

    ReplyDelete
  43. Dada mlokole inabdi ujibu mapigo kwa post ya hitimisho.

    Just summarize the comments and analyze them.

    ReplyDelete
  44. Kama wake zenu hawakubali kula bila chumvi waambieni hamna uwezo wa kununua chumvi waondoke waende kwa wenye maduka ya chumvi wakaolewe.

    kama pia hawawezi kula mboga nyengine ila kisamvu pia waambieni watu tumezoea nyama bibie!

    ReplyDelete
  45. kunzisha DNA siyo kuwakomesha, kama wanataka kuwa na mabwana wengi, they will always manage them unknowingly.

    ReplyDelete
  46. Kilaaniwe kipimo cha DNA. Kimekuja ndoa zilizofungwa mbinguni.

    Kimsingi hakuna sababu ya kutalikiana hata kama mtu anacheat au anakula watu. Vumilieni, mmesahau masomo ya shule za jumapili?

    ReplyDelete
  47. Kimsingi nina wasiwasi na ulokole wa huyo mdau wa sweden.Biblia iko wazi kuhusu usawa wa mwanaume na mwanamke.Huyu dada anamix mambo ya kidini na ya kidunia na hiyo sio sera ya mlokole halisi.Unataka kuikosoa biblia kwa kwenda na wakati?"Eti sasa tukubali kuwa tuko sawa kwa ushawishi wa mikutano ya beijing na mwanamke kupata mafanikio"!Huku ni kujidanganya na kama ni mtu wa mungu utakemea hilo.Wanawake walipigana vita gani kupata huo usawa kama sio wanaume ndo walianza kuwasemea awali,peluzi kwanza historia

    ReplyDelete
  48. 1. A successful man is one who makes more money than his wife can spend.

    A successful woman is one who can find such a man.


    2. Men wake up as good-looking as when they went to bed.

    Women somehow deteriorate during the night.


    3. A man will pay $2 for a $1 item he wants.

    A woman will pay $1 for a $2 item that she doesn't want.


    4. A woman marries a man expecting he will change, but he doesn't.

    A man marries a woman expecting that she won't change, and she does.


    5. There are two times when a man doesn't understand a woman.

    Before and after marriage.


    6. A woman worries about the future until she gets a husband.

    A man never worries about the future until he gets a wife.


    7. To be happy with a man, you must understand him a lot and love him a little.

    To be happy with a woman, you must love her a lot and not try to understand her at all.


    8. Any married man should forget his mistakes.

    There's no use in two people remembering the same thing!


    9. A woman has the last word in any argument.

    Anything a man says after that is the beginning of a new argument.


    10. Women look at a wedding as the beginning of romance,

    while men look at a wedding as the ending of romance.

    ReplyDelete
  49. DNA bado haitoshi kwa sababu haiwanasi wasiopata mimba.

    Tunataka LIE DETECTOR.

    ReplyDelete
  50. duh sijawai ona,hahahahahaaaaaaaaa

    watu mna hasira mkiguswa na ukweli?

    ila ilivo ktk "tamadunu"za afrika mwanamke ni bidhaa tuu yan kero tupu

    nakuunga mkono annon apo,"MWANAUME ANAKOSA CONFIDENCY KABISA AKIKUTANA NA MWANAMKE MSOMI"lazima mitusi imfuate mdada tu tena kwa wale wasioolewa bado.JAMAN HUU ULIMBUKENI?

    anyway,tutaishi tu kwa kuvumiliana Mungu atutie nguvu ingawa ni ngumu sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...