Chaaz Baba wa Twanga Pepeta akiimba wimbo
maarufu uliotungwa na
kuimbwa na hayati Nico Zengekela uitwao
'Solemba' na bendi ya msondo ngoma music band
katika shoo ya kila jumapili inayodhaminiwa
na kilaji cha Kilimanjaro
lager viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
wataalamu wa muziki wanausifu wimbo huu sio tu kwa mashairi yake bali pia wanasema umekidhi haja zote za muziki katika mpangilio wa ala, sauti na midundo. maudhui yake yamekuwa msamiati ambapo mtu ukiwa umemkosa mpenzi wako katika ahadi mliyowekeana inasemwa umeachwa 'Solemba'


Daah nimekumbuka mbali kweli Bro michuzi...ahsante sana ila nimekuwa nikiutafuta original yake long time sijapata kama kuna mtu anajua wapi naweza sikiliza original ya wimbo wa solemba through internet please tell me.
ReplyDeletedah,hata mimi nimekumbuka enzi za mchana mwema na RTD..aisee bro michu kama ikiwezekana tuwekee na nyimbo nyingine kama ogopa tapeli ya vijana jazz na mesenja kaleta balaa ya tx moshi nadhani,samahani kama nitakuwa nimekosea. tnx
ReplyDeleteMashairi ni bomba, na huwezi kuulingamisha na Original version yake.....hivi kuna mwanasiasa bongo anayevaa heleni? maana kila star na maheleni inanikera mimi basi tu...
ReplyDeleteMichu...huu ndio muziki sio ujinga wa uigizaji wa fleva. Kazeni moyo Msondo....
ReplyDeleteOld is Gold always,japokuwa huu wimbo una muda mrefu tofauti na mimi lakini acheni tu.Asante Michuzi umenifanya nienjoy pasaka yangu kinyumbani nyumbani tu.Enjoy
ReplyDeletenimekuwa nikiita nyumbani kwako aibu nilopata ni kubwa sana te le le,ah ahsante kaka kwa kukumbushana mambo matamu ya zamani kaka si mchezo!!.
ReplyDeleteDah!! Kweli Kaka hapa umecheza. Lakini licha ya kukubaliana nawe kuhusu maudhui na mpangilio wa wimbo, pia lazima tukubali kuwa Mzee Mabera ni mpiga solo mzuri na pengine bora kuliko wote tulionao. Unaweza kusikiliza nyimbo alizopiga Original kisha ukasiliza remix na huto-feel tofauti.
ReplyDeleteKwa Anon unayetaka kusikiliza online wasiliana nami kupitia changamoto@gmail.com kisha nitakueleza.
nenda ktk bongo5 ktk muziki utaupata
ReplyDeleteold it is always gold
Duh Ray C ana mengi ya kujifunza. Nimekubali.
ReplyDeleteMbona mashibiki wamenywea vitini kama wanaombeleza vile!?
ReplyDeletewangetoa remix yake au part 2...hahaaaaaaa tehetehhhhh. hakuna mashambulizi jukwaani
ReplyDelete