Jaffer Iddi Amin Daddah (kati) akiomba dua kabla ya mlo huku Madaraka Nyerere (shoto) na Vincent Nyerere wakiikia wakati wa dina la mchana kijijini Mwitongo, Butiama, Jana
vikundi vya ngoma asilia za Kizanaki vikitumbuiza wakati wa ujio wa Remo Jaffar Iddi Amin Daddahy huko Mwitongo Butiama jana mchana

Mtoto wa tatu wa Idd Amini, Jaffer Iddi Amin Daddah 'Tshombe' akipokewa na Madaraka Nyerere huko Mwitongo, Butiama, jana. .pichani amini akiingia nyumbani kwa mwalimu,pia madaraka Nyerere na Mdogo wake vincent Kiboko Nyerere pamoja na Remo Jaffar Mwitongo Butiama


Gofrey Madaraka Nyerere na Remo Jaffar Amin Daddah wakati wa mlo huko Mwitongo Butiama

msosi wa nguvu wa kizanaki uliandaliwa kwa mgeni huyu mashuhuri.


Globu ya Jamii inapenda kutoa heko na pongezi kwa BBC kwa kuandaa mkutano huu wa watoto wa watani wa jadi, marehemu baba wa Taifa Mwalimu Jiuluis Kambarage Nyerere na Rais Iddi Amin Daddah wa Uganda ambao miaka 30 ilopita wakiwa majemedari wakuu nchi hizi zilipigana vita kwa miaka miwili na bongo tukaibuka kidedea.
Ni kweli kwamba kuna wanaoona kwamba hakukuwa na faida kwa vijana hawa kukutanishwa, lakini pia si uwongo kwamba BBC Idhaa ya Kiswahili imepiga bao la kisigino kwa ubunifu huu ambao redio za bongo zingeanza kuiga kwani idadi ya wasikilizaji waliofuatilia zoezi hili haisemeki.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. WABONGO WAO KILA KITU KWAO SIO MUHIMU ,TATIZO UBONGO UME FREEZE.NCHI YENYE MALI NYINGI NA WAJINGA WENGI.

    ReplyDelete
  2. Idadi ya wasikilizaji haisemeki. Too vague. Wangapi? tupe idadi kamili. na hiyo audience research umeifanya lini au unaigeuza blog ya jamii kufanya PR?

    ReplyDelete
  3. Kwa kawaida audience ya BBC Swahili ni milioni 21 [21 milion listeners across East and Central Africa], hizo ni weekly figures.

    Sasa kama hii story ilikuwa record-breaking, ongeza kama laki tano au milioni moja. Hakuna ubaya Michuzi kufanya PR, mbona 90 per cent ya story humu kwenye globu ni PR? Au huoni hizo za TBL, Voda etc?

    Source: BBC Audiences

    ReplyDelete
  4. lakini hii si kwamba BBC inacreate news? kazi ya chombo cha habari ni kuripoti matukio sio kuandaa tukio halafu unaripoti. what's next mapirate wateke meli na mwandishi wa BBC ndani yake ili aripoti jinsi utekaji unavyofanyika? just thinking.

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu [o5:20], wewe unafuatilia media trends za wapi kama unashangazwa na BBC kuandaa mkutano wa aina hiyo. Very straight forward event.

    Nitajie leo hii, chombo gani cha habari kisichotaka kuwa news chenyewe kipate coverage.

    Nadhani mambo ya media waachieni media experts wafanye kazi yao. I'm sure Michuzi angekwambia anaanzisha blog miaka michache iliyopita ungemwambia haitafanikiwa, ni swala vision na attitude.

    ReplyDelete
  6. Anony 5:31pm Wakati mwingine tuwe tunakubali tuonapo point zetu azina uzito,Ubishituu .

    ReplyDelete
  7. Watani wa jadi???? Sikuwa najua kuwa ile vita ilikuwa ni kwa ajili ya UTANI :-(

    ReplyDelete
  8. Sasa naomba mniambie. Kwanini wamemgolify hivi huyu? Yaani baba yake aliyoyafanya yote yameshasahaulika? Leo mtoto apokelewe na ngoma na mambo yote hayo? What am I missing here?

    ReplyDelete
  9. Yeah namuunga mkono anony @ 5:31pm. Kwanini waandaye hii tukio halafu wareport? Tunagain nini from this report?

    Baba yake alikua dictator.Kwanini apokelewe kwa vishindo hivi? Baba yake hajafa muda mrefu ina maana huyu alikua mkubwa wakuweza kumshauri baba yake aombe msamaha. Je alifanya hivyo?Je baba yake angekua hai huyu angekubali kuja kwenye huu mkutano?

    ReplyDelete
  10. Ok,

    BBC wakimaliza na kina Madaraka Nyerere na Remo Amin waende Amman, Jordan na Texas, USA wakaandae mkutano wa binti za Saadam na Bush. Wendelee na hii series wakawakutanishe wake za Arafat na Sharon wapate chakula cha pamoja na mapicha kama hayo ya kina Madaraka na Remo.

    Wakimaliza hapo waandae mkutano wa wanawe Mandela na Verwood. Wasiishie hapo wakawakutanishe yule mwanae Thatcher na mwanae Nguema.

    Seriously, I don't understand this BBC thing, xchiiiiii.

    ReplyDelete
  11. Vita hakupiganwa miaka miwili.

    ReplyDelete
  12. Anonymous 5.20 pm Sasa hapo habari ilikuwa ni ipi kwa vipimo halisi vya habari? Nini chanzo cha habari hiyo kama kweli habari hiyo ipo? Tofautisha TBL, VODA na BBC. Kama BBC inaanza kufanya kazi kama VODA au TBL basi tuambie. Waambie watuandalie ya watoto wa Mobutu na Kabila au watoto wa Kagame na Habyarimana au watoto wa Museveni na Kabila au watoto wa Saddam na Bush.

    ReplyDelete
  13. HUYU WA APRILI KUMI 5:31 ANATULETEA MIZENGWE YAKE NAYE.
    SABABU SIJUI ANACHOCRITISIZE NI KITU GANI.
    CNN, REUTERS NA BBC TV VYOTE NI VYOMBO VYA HABARI, HURIPOTI NA PIA KUCREATE NYUZ.
    TENA KUNA TOFAUTI BAINA YA RIGHT NA WRONG, INAONESHA HUYU MDAU BONGO LAKE HALIWEZI KUCHANGANUA BAINA YA UZURI WA KUKUTANISHA MAHASIMU NA UBAYA WA MAHARAMIA KUTEKA NYARA MELI.
    WATU WENGINE BWANA, SO COMPLICATING.
    JAMAA TUENDELEE KUTAFUTA ELIMU VICHWA VIFUNGUKE!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  14. Sasa huyo mcheza ngoma ya kienyeji mbona kavaa viatu Nike?? :-)

    Mdau New York

    ReplyDelete
  15. Huyo bwana mdogo vincent mwenye suti nyeus naskia nakuja juu sana kisiasa huko Musoma mjini ila tatizo lake moja kajiunga na Chadema hapo kani kera ye arudi tu C C M ndo chama chao,

    ReplyDelete
  16. We Anon wa 707am untaka mcheza ngoma achomwe na miba? si atastaafu mapema???

    ReplyDelete
  17. Wacha wasameheane. Nyie wenye ugwadu ntaenda kaburini na maugwadu yenu. Mambo kusameheana. Vinyongo vyenu ndio vinawapeleka kwa waganga mkarogane au kukatana mapanga. Wacha watu wasameheane misosi iliwe na wapika misosi wapewe hel ayao ya nguvu wacheza ngoma wapewe hela yao ya nguvu basi ndio biashara zenyewe. Kwani kimeharibika kitu?

    ReplyDelete
  18. Ni anon wa 7:07.

    Nia yangu siyo kwamba aumie, bali ingekuwa vizuri kama angeweka viatu vilvyoenda sambamba na hiyo ngoma -- pengine vilivyochongwa kienyeji au vilivyoipa maana zaidi muktadha huu wa kitamaduni.

    ReplyDelete
  19. Angevaa hata matairi,tungemwelewa hapo kwa kugonga nike ametuchanganya sana!!hivyo viraba vya kitozz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...