mshambuliaji nyota wa al ahly mohamed aboutrika akipewa onyo kwa kuchomekea vibaya
neshno lilifurika kiaina
kipa wa al ahly wala hakuwa na kazi sana leo
gado-kwa-gado: washambuliaji mrisho ngasa (tatu shoto) na george ambani (pili kulia) hawakupewa nafasi hata ya kupumua
kocha wa yanga profesa kondic akiongea na mwandishi maulid zuberi baada ya gemu

mlinzi nurdin bakari wa yanga akikabilina na winga wa al ahly katika wa nja la neshno jipya.
yanga wamepigwa 1-0 katika dakika ya nne ya kipindi cha kwanza na al ahly wanatawala mpira kwa muda mrefu sana, na inakuwa kama wanacheza mtu kati, huku mashabiki wa upande wa kaskazini wakihesabu kila pasi kwa sauti. yaani kila pasi wao 'moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kuuuumi.." kuna wakati al ahly walipiga gonga hadi 15 kabla ya yanga kugusa mpira
Naaaaaam NA MPIRA Ndo UMEKWISHA matokeo ni AL AHLY 1 na YANGA 0.
AL AHLY WANASONGA MBELE KWA USHINDI WA JUMLA YA MABAO 4-0

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Cheki jamaa anavyovuta mpira, unaona kabisa anajua anafanya nini.

    Mimi nilimwambia mshabiki mmoja wa Yanga ambaye huwa anatoa visenti vyake kusaidia Yanga, kwamba haiwezekani Yanga ikawafunga mabingwa wa Afrika, mbaya zaidi timu ya Misri. Ni kitu ambacho hakiingii akilini.

    Haya ni mambo ya Simba tu kuwafunga Wamisri ingawa vipigo vya Enyimba ya Nigeria hatutavisahau.

    ReplyDelete
  2. HAHAHAAHAHAHAHA nacheka mpaka nakohoa ngoja nichukuwe maji WEKUNDU wa Misri wamewala KIMOJA tu hahahaah.

    ReplyDelete
  3. Abdul TikaApril 04, 2009

    Mie binafsi nilijua tu bado Wabongo hatuna uwezo wa kumtoa AL-AHLY,ni club kubwa hapa Afrika kwa kila kitu(chenye manufaa kwa club)ukilinganisha na Yanga.Hebu tu cheki hiyo picha hapo juu,maumbile tu ya mchezaji yanakufanya ufungwe kabla ya mechi.Yanga msikate tamaa kwani mnayo nafasi nyingine mwakani.Kila la KHERI kwa AL-Ahly,kwani ingawa ni MTZ lakini navutiwa sana na soka wanayopiga hawa ndugu zetu wa Afrika ya Kaskazini(Waarabu wa Afrika).
    Abdul Tika(THE KOP)
    Msolwa Kisayani
    MKURANGA.
    PWANI

    ReplyDelete
  4. A lesson of some sort to Tanzanian football associations...that there are a lot to be learned and changed to be able to compete with and play against football teams of today. A lot. If they/you need me to explain in details, i will be ready.

    ReplyDelete
  5. Wanafungika tu, tutawafunga goli 4 bila matatizo by Maungila Madega

    Tukijitahidi sana wanaweza kutufunga goli 2 - 1 au 1 - 0, jamaa uwezo wao ni mkubwa sana kwetu by Kondic

    Leo hawatoki AL AHLY by mashabiki wa Yanga

    YANGA 0 AL AHLY 1 by matokeo

    ReplyDelete
  6. Wanafungika tu, tutawafunga goli 4 bila matatizo by Maungila Madega

    Tukijitahidi sana wanaweza kutufunga goli 2 - 1 au 1 - 0, jamaa uwezo wao ni mkubwa sana kwetu by Kondic

    Leo hawatoki AL AHLY by mashabiki wa Yanga

    YANGA 0 AL AHLY 1 by matokeo

    ReplyDelete
  7. Yanga hata iweje ni pasua kichwa tu.

    ReplyDelete
  8. Ubabe nyumbani...nje fisi tu!

    ReplyDelete
  9. Mwarabu katuchinja bila bismilahi!!!

    ReplyDelete
  10. Hongereni ndugu zangu wa jangwani. Jumla imekuwa alba mwaka huu, sio hamsa.
    Sijui nani alisema mtumie uwanja mpya. Ingekuwa mechi ichezwe kwenye uwanja wa zamani msingecheza leo, mambo yangekuwa safi. Na vile vitu mlivyofukia pale vingewasaidia.

    ReplyDelete
  11. Haya wafuga kambale wa jangawani,mukatafute mchezo mkacheze na Bwana wenu manji,we unafikiri kila timu inaweza kumtoa Mmisri? mambo hayo wanafanya wekundu wa msimbazi...Yebo Yebo...!!! Hamna cha ngasa wala ngisi,wala MussaJibwa...!!! Ngoma yenu bado ya kitoto...!!!

    ReplyDelete
  12. Hadi yanga mtakapocheza mechi za nyumbani na kupata ubingwa ki halali ndipo mtaweza kushindana na mwarabu, hata mwaka kesho mambo ndo haya haya maana yanga tena ni mwakilishi na utaratibu wa kupata ubingwa wa nchi ni ule ule.

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya nanihii, kuna camera imekunasa ukiwa na mikoba uwanjani, labda ndiyo maana hatujashinda leo. Hebu chungulia kwenye blogu ya Yanga (yangatz.blogspot.com)

    ReplyDelete
  14. mpira wa sasa sio uchawi, kwani yanga walitegemea zaidi kufukia uchawi ili washinde,ndo maana walitaka kugomea uwanja huo kwa sababu hawakuwa na pa kuchimba. sasa yakowapi,waache ujinga na kuua albino.

    ReplyDelete
  15. KWANI SIMBA IMESHAWAHI KUITOA AL AHLY???? NINACHOKUMBUKA NI WALIWAFUNGA MWANZA LAKINI HATIMAYE WALITOLEWA MISRI. SIMBA WALIITOA ZAMALEK KWA MATUTA.

    ReplyDelete
  16. George Ambani labda yuko Simba,sisi hatuna hilo jina

    ReplyDelete
  17. Japo wamefungwa lakini mijihela mwanawane wamevuna. Ndio maana TFF walikua wakililia wachezee Taifa stadium.
    Ila nashangaa sana jamaa hawa "gongowazi" hawatokeagi uwanjani Simba ikicheza big game kama hivi,yaani leo huwezi amini washabiki wa Simba na wa Yanga karibu idadi ilikua sawa. Sisi japo ni wapinzani wao wa jadi lakini tunawachangia wenzetu ki maslahi ila wao wana ka"solidality" ka kususia mechi za Simba ili kutowachangia mapato.Madega anailaumu Simba hadi kwenye tuzo za KILI kalalamika kuhusu Simba, jamaa noma sana kankshangaza kweli yaani kachukua muda wke badala ya kutoa tuzo anazungumzia wana Simba, ajabu sana huyu "Rais".
    Kasahau kwamba Simba iliwapa Monja Liseki,Shaban Ramadhani na mwengine nimemsahau ili waongeze nguvu kwenye ushiriki wao wa club bingwa Afrika, na kwa shukrani yao wakawang'ang'ania,"Rais" kasahau ule udugu.
    Haina sababu ya kuwapa pole Yanga kwa sababu wenyewe wanakiri wamefungwa na timu bora,ila sote Yanga na Simba tuna cha kujifunza kuhusu timu hii. Sawa tutasema tofauti ya uchumi kati yetu ni tatizo lakini je kwa timu kama Yanga mechi kama ya leo wangetengeneza fulana bendera,kofia,jezi, mitandio halafu wakaifanyia "promotion" wangepata kiasi gani leo?
    Lakini kina Madega hili wala hawaoni kama ni jukumu lao kabisa, na si Madega tu hata Dalali sijawahi kuona akitoka na wazo kama hili badala yake wamewaachia wezi tu wa mitaani wanufaike kwa uzembe wao wa kutegemea fitina na wafadhili.
    Tujifunze Simba na Yanga na sisi tuwe na uwezo wa kulala Kempiski kwa gharama toka timu zetu na si kutegemea wafadhili pekee
    Kalunde

    ReplyDelete
  18. "Kipa wa al ahly hakuwa na kazi" hata kwenye mechi ya kwanza misri alikuwa na mapumziko mno, mie mpaka nikadhania kuwa Yanga walienda kulinda goli lao na si kushambulia. Hamna timu Tanzania itayowaweza hawa jamaa. Mifumo ya uendeshaji wa timu itabidi ibadilike kwanza.

    ReplyDelete
  19. Ndio shida ya kupata ubingwa kwa mbeleko.
    Imenikumbusha miaka ya themanini yanga walipofungiwa kwa kutaka kumshikisha takrima refa kabla ya mechi.

    ReplyDelete
  20. HAWA KANDAMBILI YANGA NI SHOMBO TUPU, WANATUPOTEZEA WAKATI TU BURE.
    MI SIJAPATA KUONA WACHEZAJI WAZEMBE KAMA HAWA, INAONESHA WALA HAWAFAHMU NI NINI HASA MAANA YA KUSHIRIKI MASHINDANO NA KUWAKILISHA TAIFA.
    NIMEONA MECHI YAO, WAZITO MNO JAMAA HAWA, HAWAJITUMI, HAWANA MPANGILIO WA UCHEZAJI, MRADI NI TABU TU UKIWAONA UWANJANI.
    NAKUMBUKA NILIUONA KUTOKEA HAPA UKEREWE MTANANGE WA SSC VS. ZAMALEK ULIOPIGWA MISRI, SI MCHEZO BABU YANGU, SSC WALIWANG'ANG'ANIA WAARABU HASA, UNAJUA KUWA VIJANA WANAELEWA NINI MAANA YA USHINDANI.
    HAWA YANGA UTUMBO MTUPU, NA KAMA TUTAENDELEA HIVI KUWASAIDI SAIDIA WAPATE UBINGWA KILA MWAKA SABABU YA VIPESA VYA HAO WAFADHILI WAO, SOKA LA BONGO LA VILABU LITAKUWA NEGATIVE KILA MWAKA, NA RANK YETU ITAENDELEA KUPOROMOKA.
    TENA BASI HATA HAO VIONGOZI WAO HAWANA UPEO, MANENO NA FIKRA ZAO NI VICHEKESHO VITUPU WE MSIKILIZE HATA HUYO KOCHA WAO, ETI "KILA MSHAMBULAJI AFUNGE BAO MOJA TU UWATOE AHLY" MI SIJAPATA KUMSIKIA KOCHA NA KAULI KAMA HIYO, UTOTO MTUPU.
    YANGA BOMU!
    Mndengreko, Ukerewe

    ReplyDelete
  21. We Anon wa 7:22 na Ndugu yangu Mndenge mwatakiwa kulaumu "Ulipojikwa na sio ulipoangukia".Chamsingi hapa hawa YANGA hawauwezi MZIKI wa EL-AHLY na sio YANGA tu,hakuna timu ya BONGO inayoweza kupambana nao.Hebu tuchukulie mfano mdogo tu hao tunaowaweza(Washelisheli) YANGA kawapiga ngapi? Naomba mnikumbushe.Huwezi kusema WANABEBWA KUPATA UBINGWA huo ni ushabiki wa UCHOCHEZI.Ukweli uliowazi nikwamba hawa Yanga kwa TZ ndio inayotamba kwa miaka mingi,lakini kutamba huko huwezi kulinganisha na El-ahly.Usiumie roho YANGA kuwakilisha kila mwaka,laumu vilabu vyenu vinavyoipatia Yanga ushindi.Mfano mwaka huu ni timu moja tu(KAGERA SUGAR) iliyoifunga Yanga,we wategemea nani awakilishe nchi hapo.Acheni UNAZI usio na Msingi,soka sio lelemama.
    THE KOP
    CANADA

    ReplyDelete
  22. Moja,mbili,tatu,nne,tano ..6,7,8,9,10,11,12,13,14..15 ahaah.mpaka raha.Kweli wekundu ni wekundu tu.
    Balozi nilikuona mpirani jmosi na the fulanas,mambo naona sio mabaya sana-vijesenti inaonekana unavyo.
    Hongera sana wekundu wa Misri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...