


MSANII ASHIMBA AMEWASILI DENMARK KWA AJILI YA MAONYESHO KADHAA YENYE LENGO LA KUITANGAZA ALBAMU YAKE MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA “NURU NYIKANI”.
ALBAMU HII IMEREKODIWA CHINI YA USIMAMIZI WA PRODUZA JAKOB POLL NA NI MCHNGANYIKO WA JUMLA YA NYIMBO 14 ZILIZOIMBWA KWA LUGHA MBALIMBALI ZA TANZANIA ZIKIWEMO KINYAMWEZI, KIMASAI, KISUKUMA NA KISWAHILI.
LADHA ILIYOMO KATIKA ALBAMU HII NI MSETO WA VIONJO VYA KITANZANIA NA KIELEKTRONIKI. UNAWEZA KUPATA NYIMBO ZA ASHIMBA AMBAZO TAYARI ZINAUZWA KWENYE MTANDAO KWA KUTEMBELEA
MZStore.woa/wa/viewAlbum?
id=310857774&s=143458
KWA TAARIFA ZAIDI YA ASHIMBA PAMOJA NA MAISHA MUSIC AMBAYO NDIYO KAMPUNI INAYORATIBU KAZI ZA ASHIMBA.
Nimependa muziki wake ni unique unaweza kusema wa kiasilia hakuna mauzungu sana wala mauzaire kabisa na kawashirikisha madada makini Enika na Naakaya big up brother tukipata watu 5 kama huyu itakuwa bomba!
ReplyDeleteNimebahatika kununua CD hii kutoka kwa rafiki yangu anaitwa Kwame. Baada ya kusikiliza nyimbo tatu tu, niliipenda na kuinunua.
ReplyDeleteKama unapenda muziki wa asili uliochanganywa na vyombo vya kisasa basi hii ni CD nzuri sana. Mwanamuziki huyu anaimba vizuri na vyombo vimepangwa kwa umakini. Kwa kweli akiendelea kama alivyoanza basi atafika mbali sana basi siku moja tunaweza tukamuona kwenye majukwaa wanayopita wanamuziki wa waliobobea kama Youssou N'dor na Salif Keita.
Nimeipa cd nyota 4 kati ya 5