Ndio Mukulu wa Libeneke wa Wilaya ya nanihii, tunashukuru kwa tips za safari yako ya USA, tunasubiri za Ujeruman, Japan nk. Hapa ninaombi langu ninaomba ulitundike kwenye mtandao wetu ya jamii.
Kuna waheshimiwa ninawatafuta kwani sina habari zao kwa muda mrefu sana tangu tumalize shule.Kwanza kabisa ningependa kuwasiliana na ndugu Solomoni Mwakyuse(samahani kama nimekosea jina la ukoo siunajua tena majina mengine mpaka ulimi uwe umechachushwa kwa ndimu), huyu ni mtu wa mbeya, alisoma elimu ya Sekondari hapo DSM Tambaza kama sikosei baadae akasoma chuo cha uganga Mafinga na kumaliza mwaka 2000, baada ya hapo akaenda Marekani.
Mwingine ni Fridolin Nanyanje chinga Boy wa Newala, huyu nilimaliza naye Sekondari ya juu ya Ndanda1995,alikuwa Jeshi la Polisi huko Nzega na baadae nasikia akaacha na nasikia anafanya kazi Dodoma( Pia mate wote wa Ndanda High school (LY 2005)enzi za mnoko Mwl Mlaponi, tuliyekuwa tunamkomoa kwa kumuibia maindi shambani kwake lol ).
Aidha ninawatafuta mate wote tuliomaliza nao Kibiti Sekondari (Kinyanya Juu 1992, Unakumbuka kwenye graduation tulipopigiwa Disco na Radio Tanzania na Late Michael Katembo kama DJ?) hasa Salum Kapilima huyu tulikuwa tunaiba nae sana machungwa ya shule na madafu, alikuwa na utaalamu wa kukimbia kukwepa kukamatwa.
Nakuaminia mzee wa Libeneke hutaniweka kapuni.
Naomba uanike anuani pepe ili wadau tutafutane.
Benedict Kimbache

Skype Name: Kimbache1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    Ha ha haa.... inaonekana ndugu yangu una karoho ka wizi wizi eee? maana o'level ulikuwa ukiiba machungwa, A level ukawa unaiba mahindi, sasa hivi dili lako ni lipi? angalia lakini za mwizi ni 40, jihadhali kuna moto wa matairi mwanangu, huo huwa ukiwaka hauzimi. Mdauz ndani ya Toulouse.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    Anaitwa Solomon Mwankusye, yuko huko huko marekani, nitakutumia namba ya simu ya baba yake ili aweze kukupa mawasiliano yake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Kwanza wewe Benedict una kesi ya kujibu afadhali umetoa ushahidi mwenyewe kwamba mlikuwa wezi wa mahindi na machungwa!
    Subiri summons ipo njiani mtahitajiwa mahakamani muda sio mrefu! Mlikuwa watoto wabaya sana mlipokuwa sekondari!! Hahahaaaaa mmekwisha!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2009

    Mweshimiwa mtoa maoni wa pili ningefurahi sana kama utanipatia contact ya dingi wa Solomoni, nasubiri. Ahsante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...