ALIYEKUWA mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba (pichani kulia) pamoja na Meneja miradi wa Benki hiyo Deogratius Kweka (pichani shoto), wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka waliyonayo, wameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mahakama hiyo kufuta hati ya mashtaka iliyotumika kuwashtaki.
Maofisa hao wa BoT waliokuwa wakishtakiwa kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasala ya zaidi ya Sh Bilioni 200 kupitia ujenzi wa majengo pacha ya Benki hiyo, waliahiwa na mahakama hiyo kulingana na na kifungu namba 128 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Hata hivyo mahakama hiyo baada ya kuwaachia maofisa hao, walikamatwa tena na jeshi la Polisi kulingana na kifungu hicho cha sheria kuruhusu upande wa mashtaka kuwakata na kuwatengenezea hati mlpya ya mashtaka.
Kutokana na kukamatwa huko upya, washtakiwa hao walipelekwa katika kituo cha Polisi cha kati, mpaka hapo hati ya mashtaka itakapoandaliwa ambayo itatumiaka kuwashtaki washtakiwa hao upya.
Awali upande wa utetezi katika kesi hiyo, uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kutaka washtakiwa hao waachiwe huru kwasababu ya kukosewa kwa hati hiyo.
Ombi hilo lilipingwa na upande wa mashtaka katika kesi hiyo, uliodai kuwa washtakiwa hao wanatakiwa kuachiwa kwa kufuata kifungu namba 128 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, ili hati mpya iweze kuandaliwa.
Kufuatia mabishano hilo, mahakama imelikubali ombi la upande wa mashtaka la kuwaachia huru kwa kufuata kifungu hicho cha sheria, kinachoruhusu washtakiwa hao kukamatwa upya pindi mahakama inapo waachia.

jamaani hakuna kuleana hapo, na kuendeleza kufuga ujinga huu mpaka lini,hawa watu wachache ndio wanangusha sana mataifa ya africa,na taifa letu kiujumla ndio maana kila siku tunaitwa watu wa ulimwengu wa tatu, kwa sababu ya tabia kama hizo, na hii inakua inaendelea isipolekebishwa
ReplyDeleteSASA KWELI TANZANIA IMEISHA!!WANAACHIWA HURU KWA VIPI?HELA ZILIENDA WAPI WAKATI WAO NDIO WALIOKUA MADARAKANI!JAMANI KWEL HII NI RUSHWA IMETOLEWA
ReplyDeleteJamani inatia uchungu sana kuona kesi yenye hisia za watanzania wote wenye uchungu na nchi yao zinakuwa na danadana sisizo isha.Hivi inakuwaje kesi nyeti kama hii hati ya mashtaka inakosewa? au ndio ufisadi mungine ndani ya vyombo vyetu vya sheria?kesi ya hasara bilioni 200 kwa serikali hati inakosewa!hivi hatuoni kama ni hasara kuendesha kesi za aina hii? tunawalinda hawa, tunawalisha na tunawasafirisha kwa pesa ya walipa kodi.mimi naomba hata uwezo wa hawa waendesha mashitaka uchunguzwe nahisi ni vihiyo wa sheria,na polisi uwezo wa kuandaa mashtaka ni mdogo hivyo kazi hiyo wapewe wataalamu wa mambo ya sheria.mbona kesi ndogo tu rushwa laki saba zinakamilika haraka na hakuna hati inayokosewa.nchi hii watafungwa masikini na mafukara tu.tajiri hafungwi, tutaendelea kuonyeshana kiini macho ili kuwafurahisha wahisani tu.Hizi kesi zote kubwa ni usanii tu unafanyika, ushahidi upo wazi ya nini kuzunguka? wahasibu wakigushi wanafungwa,polisi manesi wakila rushwa wanafungwa, mahakimu wa mwanzo pia mbona inakuwa ngumu kwa MAFISADI?
ReplyDeleteThat is so strange!!!
ReplyDeleteNdivyoo itavyo malizwa
ReplyDeleteduh bongo ni noma, evresing is possibo...
ReplyDeleteWIZI MTUPU
ReplyDeletewhats the point?
ReplyDeletewako wapi kina Mramba, Mgonja na Yona?
whats is gonna happen to Rostam Aziz?
PURE 100% Rubbish
Tangu lini fisadi akafungwa?kesi zitakwendaaaaaaa,mwisho wake zitazimika tu. hiyo ndio hali ya Tanzania.
ReplyDeleteWengi tulijua hili ni changa la macho.Bado kina nanilii nao waachiwe huru.
ReplyDeleteBtw- kiswahili fasaha ni hasara si hasala.
broo michuzi habri za leo ?
ReplyDeletehii habari haishangazi sana na wengi wataachiwa huru . haya ndo matokeo ya kuundwa kwa tume zisizo na faida kwani wahusika watume elimu yao ndogo pengine haipo kabisa kwa maneno mengine ni mambo ya kiushkaji ndio haya.
sasa serikali waandae jinsi ya kukwepa kuwalipa fidia hii serikali ni aibu !
msitake niamini wadau waliokuwa wanatoa maoni jamaa walipokamatwa kwamba ni janja ya jk kuwanyamazisha watu, na wapo walioapa kwamba hamna lolote litalotokea kwa jamaa, nawengine walisema bloguni "hapo utasikia tu ushahidi hakuna".
ReplyDeletewengine uliona wapi kigogo akafungwa jela?
NDIYO BONGO HIYO??
ReplyDeleteSasa mashitaka mapya ni yapi? Hivi viswahili vya shera ......zungusha zungusha mara wanahukumiwa tena na vijikesi visivyo na kichwa wala mkono.... mara kesho utasikia ......utasikia mvua moja basi wametoka na wanakeep mahela yote waliyoyaiba....hicho kifungu 128 walichoachiwa kinasemaje? Na sasa hivi wamewekwa kwa mashitaka yapii? Tuelezwe wazi kwa vili wanataka maji yapoe tu halafu kesho wako mitaani na mambo yanaisha
ReplyDeleteUnajua ndugu zangu mimi nafikiri sasa tusimlaumu JK, nafikiri tuwalaumu office ya mwanasheria wa Serikali kwasababu zifuatazo:-
ReplyDeletea) JK kashawapeleka mbele ya Haki
b) Wanasheria wanafanya intentionally very unprofessional mistake wajinga wanaachiwa inauma sana
c) Tatizo ni "Experts kwenye ofisi, wataalaamu watatumaliza kuanzia kusaini miktatba, kuachia wahalifu ..etc
d) uozo mtupu mungu saidia
Utasikia serikali imeshitakiwa kwa kuwachafulia jina, na wanadai fidia ya sh bilion 200 + gharama za kesi.
ReplyDeleteWajinga ndio waliwao.
Sasa mwendesha mashtaka wa serikali ajiuzulu kwa nini alifungua kesi isiyokuwa na miguu wala kichwa na serikali itaishia kuwalipa hawa watu kwa kuchafuliwa majina. Kwa msaada tu kidhibiti cha ufisadi ni hizo bilion zao za dhamana.
ReplyDeleteHadi leo sielewi hiyo HASARA inayozungumziwa hapo ni ipi?
ReplyDeleteMbona majengo yamejengwa tena mazuri tu, hata IMF nasikia wamepanga humo humo? Na isitoshe BoT ili-host mkutano wa dunia kwenye ukumbi wao ambao hakuna mfano wake hapa Tanzania.
Cha mwisho, hii figure ya bilioni 200 wameitoa wapi wakati kazi ya Evaluation (audit) ya Majengo bado haijaisha? Kwa kufungua kesi ya namna hii tayari italeta influence katika ripoti ya wakaguzi.
Wanaoshitaki wakubali ukweli kwamba WAMEKURUPUKA.
Hapa watanzania tunafundishwa kitu kimoja ukitaka kuwa na maisha mazuri bongo kuwa Fisadi tu ndio system now. Ukipiga pesa pesa kubwa km billion 200 hufungwi. kwanza unakuwa maarufu; pili ukienda mahakamani kesi inaisha pole pole .we unaendelea kupeta. Ila ukiiba kuku au simu utafungwa maisha. Sasa ujinga gani huu mtu anaachiwa huru analeta hasara billion 200 estimation. Na bado mtamuongeza pesa Utajili kwa kumlipa Fidia. Tunakwenda wapi? Nyerere na Sokoine hupo mlipo tuombeni nchi imekwisha ,nyie wawili ndio Viongozi niliowakubali
ReplyDeleteKaka,Michu
ReplyDeleteNani mtoto asiyeelewa kama hii ni serikali iliyojaa ushkaji,usanii na ufisadi uliokithiri?
Kinachofanyika ni kupoteza maboya tu,na kuwadanganya watanzania,lakini hakuna jipya litakalotokea.
Kifupi,JK na serikali yako tumechoshwa na usanii wenu.
Na mmiss SOKOINE period
ReplyDeleteBONGO TAMBALALE...
ReplyDeleteMAHAKAMANI MAIGIZO...
DODOMA ZE COMEDY