Tarehe 25 Mei 2009 Balozi za kiafrika zilizopo Abu Dhabi Umoja wa Falme za Kiarabu ziliadhimisha siku ya Umoja wa Afrika kwa semina juu ya fursa za uwekezaji barani Afrika maonyesho ya utamaduni na utalii wan chi za bara letu. Ubalozi wetu nchini humo ulishiriki vilivyo na wenzao.
Pichani juu na chini Balozi wa Tanzania Mhe. Mohamed Maharage Juma akimkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje katika banda la Tanzania na kumpatia vijarida juu ya fursa za uwekezaji Tanzania na zawadi za bidhaa za kitanzania ikiwemo asali, chai na kahawa. Kivutio kikubwa kilikuwa picha kubwa ya mlima Kilimanjaro ambapo wengi walipata somo kwamba upo Tanzania na si kwingine popote




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2009

    naona picha ya Kikwete ni kubwa na imedominate hata bidhaa wanazotangaza.

    nabaki kujiuliza kama wanamtangaza Kikwete au wanatangaza bidhaa toka Tanzania?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2009

    Yakhe! Hii asali ni asilia nakuapia.Imetoka kwa nyuki wa kienyeji walitunzwa kwa maadili safi ya kiisilamu.Hakuna kitu haramu wallah ladhimu.Omba dua kuhakikisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...