flaviana matata katika pozi
flaviana akiwakilisha katika shoo sauzi
flaviana akiwa budapest kwenye shoo ya huko
miss universe TZ flaviana matata kesho anapaa kuelekea bahamas ambako amealikwa na waandaaji wa miss bahamas 2009 kuwa mmoja wa majaji kwenye shindano litalofanyika wikiendi hii.
akiongea na globu ya jamii kwa simu kutoka johannesburg sasa hivi, flaviana amesema anaona fahari kubwa kupata mwaliko huo ambao utazidi kuipeperusha bendera ya taifa nje ya nchi. hapo sauzi anasema anaendelea vyema na libeneke la mitindo na ni mmoja kati ya walimbwende kumi bora katika kuonesha mavazi kwenye shoo za huko.
kwa bahati mbaya flaviana hatokuwepo dar wikiendi hii ambapo mrithi wake atapatikana katika kinyang'anyiro cha miss universe TZ kitachofanyika dar wakati huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Walter MoyoMay 27, 2009

    Flaviana Karibu sana Bahamas. Watanzania tupo hapa Bahamas na tungependa kuonana ukiwa hapa. eamil yangu ni waltermoyo@gmail.com. Karibu sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2009

    Nampenda sana huyu binti...si kwa mapenzi ya ngono, nampenda kwa ubinadamu. mrembo kweli alafu anajituma sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2009

    Wee Walter Bahamas uko vacation au unapiga box? Duuh wabongo kweli tupo kila kona :)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2009

    Natafuta mchumba jamanieee.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2009

    Check mate yanavyowatoka! "Tupo bahama" "si kwamapenzi ya ngono" Jamani mtaishia kula kwa macho tu!Si huku joberg tunatafuna. Tehteteh

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2009

    Hivi nyinyi wabongo mlioko bongo mnadhani kila mtu anabeba box? Tupo wabongo wasomi kila mahala na tuna kazi za maana! Acheni wivu kama umenyimwa visa kwa sababu huna elimu, biashara, makazi ya kudumu then you need to put your acts together and do the right thing for your life. Mimi nipo huku since 90'S NA BOKSI SIJAWAHI BEBA! Hii lugha ya mabox muikome. Na hata hao wanobeba mabox wako better kuliko wewe, angalau wanaweza kuishi kwenye nyumba na kujipuliza AC, wewe unanuka kwapa hata umeme wa tanesco huuwezi kukikucha ni kuchochea mikaa na mafuta. Acheni wivu na kuomba msaada kama unahitaji kuja kuosha sura nintakutumia barua ya mwaliko na kukutambukisha ubalozi wa states hapo bongo. Ndiyo maana hatuendelei! Wivu umewajaa kibao mtachakaa huko bongo na vumbi lenu sisi huku tunapeta!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Kila la kheri Flavi..nakuamini unaweza fanya mambo mengi mazuri..endelea tupo pamoja..

    God bless u

    ReplyDelete
  8. Walter MoyoMay 28, 2009

    Wakuu heshima zenu,

    Kupiga box ni "cover" tu hata wale wenye kazi zao wanasema "wanapiga box", sasa hapo ambao wanapiga box kweli na wapo ambao ni really working professionals.

    Kuna mtu kauliza kuwa niko Bahamas vacation ua napiga box, naweza kusema vyote (Kazi+vacation), kwani huku kila siku ni sawa na vacation, ni one of the biggest tourist destination. Zile Tanzanite zetu zina soko kubwa sana hapa, lakini wengi wa wanaouza hawajui inatokea wapi!

    Well, topic ni Flaviana, kama umeshafika, jisikie huru kuwasiliana, vinginevyo tutaonana/tutakuona hiyoo siku ambayo wewe utakuwa Judge

    Walter Moyo
    Nassau, Bahamas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...