Nimefuatilia kwa makini mijadala inayohusiana na vekesheni yako na matokeo ya mijadala hiyo ambayo mwisho wake imekuwa ni mgongano wa mashabiki na wapenzi wa bulogu ya jamii na forum ya jamii.
Nasikitika sana kuwa kwa namna fulani mijadala hiyo imeelekea katika kumshambulia mtu.

Kwa sisi wengine ambao tumeingia mambo haya ya kutumia kalamu siku za karibuni mbele yako sisi ni chekechea na hatuwezi kwa kipimo chochote kujiweka au kujikuza kwa namna yeyote mbele ya uzoefu, utaalamu na umahiri wa fani ya habari na picha ambao unao kwa miaka mingi.
Uzoefu ambao kwa kipimo chochote kile haiwezekani kuuwekea bei au kipimo cha fedha.
Ninaamini JamiiForums (na forum nyingi yoyote) zinaweza kuwepo na kutoa mchango wake kama vile bulogu mbalimbali zilivyo.
Malengo na makusudio yao yanaweza yasifanane na wanachama wanaweza wasiwe wale wale lakini katika seti kubwa tunajikuta sisi sote tuko kwenye seti ya "Watanzania".
Hii ni seti inayotuunganisha sote zaidi kuliko seti ya itikadi, vyama, mwelekeo wa kisiasa, kabila, dini au vitu vinavyoweza kututofautisha.

Ni kwa sababu hiyo basi, naunga mkono kwa asilimia 101 juhudi zako za kutuhabarisha, kutuburudisha na kutupa nafasi ya kutoa mawazo yetu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu.

M. M. Mwanakijiji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Blogu ya Bw. Michuzi ni chanzo kimojawapo cha habari kwa watanzania ndani na nje ya nchi.
    Idadi ya watu wanaotembelea blogu ni uthibitisho tosha ya umaarufu wa blogu.

    Badala kumjadili Bw. Michuzi, nadhani sisi kama wasomaji na wadau tujikite kuchambua hoja na kutoa mawazo mbadala yenye mtazamo wa kujenga jamii na taifa letu kwa ujumla.

    Bw. Michuzi usikate tamaa, endelea kutuhabarisha.Wanaopendezwa na kazi yako ni wengi kuliko wanaochukizwa.

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2009

    msimamo umetulia Mwanakijiji.

    Michu, vekesheni kama kawa.

    Mwanakijiji na Michu, wenye wivu wacha wajinyonge.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2009

    Acha unafiki wako wewe Mwanakijiji, huo mjadala sasa hivi ndiyo mnaona kuwa unamshambulia mtu? kwani nini hukuhoji day one huko JF? baada ya kuona kuwa Michuzi ni mtu wa watu sasa unakuja na lugha yako ya kinafiki.

    Michuzi, tuwachie hii kazi ya kuwaumbua na unafiki wao, wanajua kabisa walilotaka kulianzisha, chokochoko kamchokoe pweza, binadamu hutomweza.

    Hakuna mwenye haja ya kukutafuta na siku nyingine muingie hizi anga. Hatuna haja na malumbano yenu huko sisi tunathamini kwa DHATI kabisa mchango wa Mh Balozi kwani anajituma kwa ajili ya wananchi kweli.
    Nyie mnaotaka madaraka ya nchi kwa kupitia mlango wa uani endeleeni na kazi yenu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2009

    Who are you anyway? Mijitu mingine inachekesha kweli kweli. Unaogopa kivuli chako mwenyewe hakuna hata mtu mmoja ambaye ana mpango na wewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2009

    Hahahahahaha eti haogopi mtu! Weka jina lako la kweli kama wewe mwanaume. Usituzuge hapa. Utakua lini? Eti M. M. Mwanakijiji.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2009

    Miye namuunga mkono kaka michuzi na ni mmoja wa wasomaji wazuri wa blog yake, hata niliwa busy namnagani au ninamtihani lazima niisome maana najua nitapata habari toka home.
    Lakini kama kweli umekuja USA kwa kikazi basi si sahihi kuiita vekesheni yaani wewe umekuja kutanua tuu kwa hele ya walipa kodi it does not sound good at all, hii inamaanisha umekuja kutanua tuu, au umebebwabebwe tuu kuja kutanua kwa hela ya walipakod.Ifike wakati tuwaheshimu walipa kodi wetu.
    We kaka michuzi kuwa muunwana wewe kama ulikuja kikazi kubali yaishe omba msaha sema wewe ni mtu wa mizaha na ulikuwa unatania tuu. Basi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2009

    WEWE MNAFIKI,MARA NGAPI UMEMTUKANA MICHUZI? JAMII FORUMS NI MALI YA WACHAGGA NANI HAJUI KUWA YULE JAMAA WA KICHAGGA,ANAEPENDA HURUMA ZA WANANCHI AMBAYE ANAMILIKI VYOMBO VYA HABARI ANAWALIPA NYINYI?

    WEWE KILA SIKU UNAMKANDIA ROSTAM KWANI KAKUFANYA NINI?HAIWEZEKANI BLOG YENU KILA ANAYEINGIA KUMTUKANA JK,ROSTAM LAKINI WACHAGGA HAWATUKANWI.

    KAMA HUOGOPI KITU KWANINI HUTUMII JINA LAKO MWAKYANJALA KAMA WANAVYOFANYA WAANDISHI WENGINE?

    KAMA HUOGOPI KWANINI UTUMIE LULA MWANA NZELU KWENYE RAIA MWEMA?KWANINI UKIPIGA SIMU KWA KINA MANUMBA HUSEMI KAMA WEWE NI SEHEMU YA JAMII FORUMS? NA UNAFICHA JINA LAKO.

    KWANINI UWE NA MAJINA ZAIDI YA MIA MOJA KWENYE FORUM YENU YA CHADEMA-JAMII FORUMS?

    UKO MAREKANI SASA MWAKA WA SITA HUJAWAHI KUTOKA, UNAMDANGANYA NANI KUWA UNA UWEZO WA KUSAFIRI?

    KAMA UNAWEZA NJOO TANZANIA TAREHE TATU MWEZI WA SITA KWENYE MECHI YA TAIFA STARS NA NEW ZEALAND AU NJOO KWENYE KAMPENI ZA CHAMA CHAKO BIHARAMURO. MWEZI WA SABA.

    LINI MBOWE ULIMUANDIKA VIBAYA?

    UMEMSIMANGA MAREHEMU WANGWE AKIWA HAI HADI AKIWA MAREHEMU, MTU AMEKUFA BADO UNASIMANGA KWA KUTUMIWA NA WACHAGGA.

    HAPO DETROIT UNAISHI KWA MFINANGA UMESHANDWA HATA KUPANGA CHUMBA?

    KWA HIYO UNATEGEMEA KUPATA MAKARATASI BY DECEMBER? AU ULE MSAMAHA WA WATU WASIO NA MIGUU(VIBALI VYA KUISHI) WA OBAMA UTAKUWA TAYARI HADI MUDA HUO?

    ITAKUWA VYEMA UMETESEKA SANA NDUGU YETU.

    MISIBA,HARUSI ZINAKUPITA NA MIAKA YOTE HIYO UMEKOSA HATA KUWA NA DIPLOMA?AMA KWELI MAREKANI SIO MCHEZO,MTU UNAIONA KWENYE PICHA UNAJUA MAMBO MEPESI KUMBE WENGINE HADI WATOKE MISHIPA.SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUKUFUATA HUKO MICHIGAN KWANZA HUNA PESA, PILI HUNA ELIMU NA TATU HUNA MAKAZI,MATESO ULIYONAYO UNAMALIZIA HASIRA ZAKO KWA JK KWENYE FORUMS ZAKO ZA CHADEMA-JAMII FORUMS.

    NAKUKUMBUSHA MATANGAZO YAKO KUWA KLH NEWS NI ZAIDI YA CNN NA MICHUZI ULIKUWA UKISEMA SANA AU UMESAHAU?
    ,MWENYEZI MUNGU SI ATHMAN BLOG YA MICHUZI IKO JUU NA WEWE KILA UNALOFUNGUA HALIPATI BARAKA KIASI UMBAKI KUJIBANZA JAMII FORUMS-JUNGU FORUMS AU JF.


    PIA USITUMIE MAANDISHI YA KIISLAM KWANI UNAYAKOSEA KUANDIKA NA UNAONDOA MAANA YOTE.

    WATU KAMA HAWA LAZIMA WAWE NA WIVU KWA MICHUZI WAKIMUONA ANAKWEA PIPA KILA DAKIKA UTAFIKIRI ANABADILI NGUO YA NDANI.

    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2009

    KUNA MDAU KAHOJI KWENYE JAMII FORUMS, KWANINI MTU FULANI MKUBWA AMEKWENDA KUTIBIWA UINGEREZA HALAFU AKAAMUA KUWA MUHUBIRI WA DINI KWENYE MIJI MBALI MBALI YA UINGEREZA,WAKATI ANATUMIA KODI YA TAIFA?

    HAWA JAMAA KINA MWANAKIJIJI WAMEKUJA JUU KUWA ASIKUGUZWE MSTAAFU TENA YULE ALIYEANZISHA MJADALA WA MICHUZI AKAJA JUU KUWA NI WIVU,HUSUDA NA WIVU LAKINI ALIPOULIZWA JEE NA NYINYI ILIKUWA NI KIJICHO,HUSUDA NA WIVU KWA BALOZI MICHUZI?PITIE KULE MUONE UNAFIKI WA HAWA WATU.

    MICHUZI ASIJE KUKUPIGIA SIMU HUYO MWANAKIJIJI KUWA KUNA CHAKULA WAMEKUALIKA,USIKUBALI WANAWEZA KUTUUMIZIA MTU WETU,USIENDE MIMI KAMA MDAU WA BLOG HII NAOMBA UWAOGOPE KAMA UKOMA HAWA JAMII FORUMS.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2009

    Kwa taarifa yenu JK anapoenda nje hatumii kodi zenu. Hizo ni hela ambazo akienda nje kuombaomba anakata panga na kutumia kwa safari nyingine. Michuzi huna haja ya kuomba msamaha kwa kutumia hela za wazungu. Na nyie ombeni kwa hao wazungu au kizungu hakipandi?

    ReplyDelete
  10. Field Marshal ESMay 27, 2009

    Hawa watu ni wanafiki tu. kama hawaogopi mbona hawataki kutoa majina yao?
    Hakuna aliye na haja nao, wakafie mbali. Kazi zao ni kulalamika tu na kusengenya watu pamoja na majungu yao. Kusema kweli wengi wao ni ma losers in the US and UK huku yanajiita misomi wakati yanaosha makalio ya wazee kwenye ma nursing homes?
    Benjamin Mwalukasa aka mm mwanakijiji kila kitu kwake ni kosa, jaribu kuweka mada kuwapinga ndani ya jamii forums, wanakufungia. Waende zao huko na ushambenga wao wa kusema watu wakati wenyewe nyumba zao za kifisadi zimejaa harufu mbaya. mimi naendesha lori langu hapa NY sina shida na mtu lakini mwanakiji na kundi lake kila siku wako kwenye maneno ya watu

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2009

    MWANAKIJIJI UNAMUABUDU MBOWE LINI ULIMKOSOA? HATA ALIPOKOPA PESA NSSF NA KUKATAAA KURUDISHA ULIMTETEA.

    KUOGOPA UNAOGOPA KAMA UNGEKUWA HUOGOPI UNGETUMIA JINA LAKO HATA KAMA MAMBO YAKO YA MAKARATASI HAYAJAKAA VIZURI.

    WASIOGOPA WANATUMIA MAJINA YAO KAMA SAEED KUBENEA HAO NDIO WAANDISHI WASIOGOPA SIO KAMA WEWE KUNGURU.

    WEWE MUOGA SANA HATA IKILAZIMIKA KUWEKA JINA LAKO UNAMINYA BENNY HUWEKI LOTE AU LA UKOO WAKO MWAKYANJALA AU KUSEMA KUWA WEWE UMESOMA SANGU SEKONDARI MBEYA UNAFICHA SANA.

    WEWE HUONI HATA KIBANDA MHARIRI WA TANZANIA DAIMA AMEKUWA AKISHANGAZWA KUONA UNATUMA HABARI AU MAKALA KWA JINA LA BANDIA NA HABARI ZAKO NYINGI HAZINA UKWELI KIASI CHA KUMWAMBIA MBOWE KUWA HAFURAHISHWI NA STYLE HII YA MTU ASIYEJULIKANA KUPELEKA MAKALA ZA UTATANISHI,SIKU HIZI AMEKUBANA SANA NA HABARI ZAKO ZA KILA JUMATANO NA WAKATI MWINGINE KUWAINGILIA KAZI ZAO,

    MFANO ILE ULIYOANDIKA KUWA JK NI MDINI KAPELEKA MAHUJAJI MIA TATU MAKKAH KWA PESA ZA TAIFA,

    WALIOKWAMA UWANJA WA NDEGE.WAKATI MAHUJAJI WALE WALIKUWA ZAIDI YA 1600 NA WALIKUWA NA MKATABA HALALI NA ATCL SIO KAMA JK ALIWABEBA KWA AJILI YA FAVOUR YEYOTE.

    KUMBUKA MAHUJAJI WALE WALIKUWA NA HAKI YA KUISHITAKI ATCL KWA KUDHALILISHWA.

    HABARI KAMA ILE TANZANIA DAIMA LINGEPELEKWA MAHAKAMANI HALAFU JAJI AKAMUULIZA MHARIRI MWANDISHI GANI ALIANDIKA.AKIJIBU NI MWANAKIJIJI JAJI ATAMSHANGAA KWANI KILA MTU NI MWANAKIJIJI HATA MICHUZI NI MWANAKIJIJI.

    JAJI ANGEENDELEA NAOMBA AJE ATUELEZE ALIKUSUDIA NINI. KIBANDA ANAJIBU SIJUI ANAISHI WAPI NA JINA LAKE KAMILI SINA.NINA EMAIL ADRESS YAKE NAYO ANAIBADILI KILA SIKU,

    MARA MWANAKIJIJI@JAMIIFORUMS,MARA MWANAKIJIJI@KLHNEWS.COM MARA MWANAKIJIJI@PODOMATIC.COM MARA LULA MWANZELU@YAHOO.COM LAKINI ZOTE HIZO SIO PHYSICAL ADRESS YAKO,NADHANI HUKO MBELE MAGAZETI YATIZAME SHERIA YA WATU WANAOLETA MAKALA.

    MTU KAMA JENERALI ULIMWENGU MASIKINI HAJUI KAMA MTU ANAYEJIITA LULA MWANANZELU HAYUPO DUNIANI.

    WAKATI JAMIIFORUMS ILIPOFUNGWA KWA SIKU MOJA MWANAKIJIJI ULIPIGA SIMU KWA KAMISHINA MANUMBA NA UKAJIFANYA KAMA SIO MTU WA JAMII FORUMS,UNGEKUWA MKWELI NA HUOGOPI UNGESEMA WEWE NI MEMBER,MODERATOR NA UMEAJIRIWA KULE JAMII FORUMS NA MBOWE NA TAJIRI ANAYEMILIKI VYOMBO VINGI VYA HABARI TANZANIA.

    ACHA UNAFIKI.NADHANI WENGI WAMEKUJUA KUWA NI MNAFIKI NA UNA UMA NA KUPULIZA.

    JAZA KWENYE JAMII FORUMS KUNA MJADALA ULIANZISHWA UKISEMA KUWA MWANAKIJIJI NI RAIA WA MALAWI MBONA ULIUFUTA HARAKA SANA? KAMA NI ENEO LA DEMOKRASIA MBONA HUKUACHA WATU WAJADILI KAMA MLIVYOFANYA KWA MICHUZI?
    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2009

    UNAJUA HUYU MWANAKIJIJI ANATUKATISHA TAMAA YEYE NDIYO SIMBA WETU NAMNA HII INAONEKANA KAMA AMEKUBALI KULA MAJANI AU MFA MAJI. KITU NI KIDOGO SANA JAMII NDIYO TASWIRA KUBISHANA NAYO NI KAMMA KUBISHANA NA KIOO KWAMBA SIO WEWE AU KAMA NDEGE KUNG'ANG'ANIA KUPITA KWENYE KIOO.
    NI MIMI CHAPOMBE HAPA ASANTENI

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2009

    Duh Mswahili,
    Una bahati hayo maoni yako unayatoa hapa katika globu hii ya jamii ambayo haina unafiki watu wametulia.
    Nina kuhakikishi kuwa JF wasingekupa uhuru wa kujieleza hivyo, wangekufungia haraka sana kwani kwao wao kukosolewa ni msamiati ambao haupo duniani.

    Endelea kuwachana hao jamaa mpaka waombe radhi kwa ile post ya kumdhalilisha Mh Balozi.

    Michuzi, tupo bega kwa bega hawezi kukudhalilisha wakati sisi tunaothamini mchango wako tupo hapa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 27, 2009

    Wanga wanajitokeza wenyewe
    Wanaogopa comments yangu ya kuwaloga
    Tutawaloga kweli
    Na dua tulianza
    Mich-use juu zaidi

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 27, 2009

    MICHUZI FUNGA HUU MJADALA KWANI HAKUNA LOLOTE LA MAANA LINALOJADILIWA! MIMI SIONI TATIZO LIPO WAPI KWA KUTUMIA NENO VEKESHENI, NEXT TIME KAMA NI VEKESHENI KWELI INABIDI UWEKE PICHA YA MY WIFE WAKO ILI KWELI WATU WAONE MPO VEKESHENI. AU UNAPOSAFIRI KWENDA NJE WALA USITUMIE NENO LOLOTE WEWE CHA KUFANYA LETE HABARI KATIKA PICHA KWA WADAU. NAONA WACHACHE IMEWAUMA SANA KWA WEWE KWENDA VEKESHENI NJE YA NCHI HUSUSAN MAREKANI.
    WAVIMBA MACHO NI WAPO NA HATUWEZI KUWAKWEKA KWANI NDO KIPAJI CHAO KUWATOLEA WATU MACHO HASA WANAOFANIKIWA KIMAISHA. MUNGU NDIYE MGAWA RIZIKI NA HAKUNA MTU YEYOTE ATAKAYEWEZA KUZUIA RIZIKI YAKO.

    FUNGA HUU MJADALA NA TUENDELEE NA MAMBO MENGINE USIKUBALI KUPOST UJUMBE WOWOTE TENA UNAOHUSIANA NA SWALA HILI LA VEKESHENI! PLEASE

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 27, 2009

    mwanakijiji amewashinda ndo maana mnampigia makelele

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 27, 2009

    Huyo anaejiita Mwanakijii ni Mnafiki sana tena sana!Huwezi kumlinganisha na Michuzi hata siku moja!Anajifanya anaijua Tanzania kama vile yupo Manzese kumbe yupo Marekani hujifanya anaijua nchi na siasa kama vile yeye superman!mie huwa nikisoma makala zake namshangaa sana!Mdandiaji tu!hujifanya mzalendo sijui MTanzania safi!kumbe mnafiki sana!

    ReplyDelete
  18. MugereziMay 27, 2009

    Ukitoa walichosema watu kama wawili wa mwanzo nadhani hawa waliofuata wengi wao wameandika pumba.

    MMK anafanya part yake na Michuzi anafanya part yake (kama watu huru kutoa maoni waonavyo wao)mbona hatusemi kuwa michuzi anapendela CCM?

    Acheni ushabiki. Mmeandika ujinga tu ningekuwa mimi mwenye hii blog mawazo ambayo hayajengi mimi nisingeyaweka hapa. Maana mtu anamlaumu mwanakijiji kuwa hajitambulishi anatumia aka kwanini na wewe usiweke jina lako unajiita mswahili?

    Kila mtu na maisha yake kama analala njaa sidhani kulala njaa huko kunamfanya asitoa mawazo yake!! Kama huko wherever USA or UK anaishi kwa kudunduliza hainihusu mimi nataka watu tuongelee nchi hii nini cha kufanya kuitoa hapa kwenda mbele.

    Unasema blog ya JF ni ya wachaga sidhani hapa kama ni mahali pake. Nenda JF Kawambie ili wajue kuwa watu wanasema blog inafadhiliwa na fulani. Usisahau pia kuwa kuna watu pia wanasema hii nayo inafadhiliwa na watu fulani kwenye chama cha kijaji!!

    MMK KATOA MAWAZO YAKE KUWA MARA NYINGI MIDAHARO IMEKUWA IKIPOTEZA MWELEKEO KWA KUWA WATU HAWAFIKILII VIZURI WANAKURUPUKA NA KUTANGULIZA USHABIKI.

    MIMI NAHESHIMU SANA MAWAZO YA WATU. LAKINI MAWAZO HAYO YAWE NA MASHIKO. Mfano umesema Mbowe kagoma kurudisha mkopo NSSF, issue hii ilitolewa maelezo kwenye public na magazeti karibu yote yaliandika sasa wewe kama unadata kuwa jamaa alikimbia deni tushushie siyo kulalama kuwa MMK anamtetea tu mbowe wakati huna data. Weka data watu tuzichambue.

    TUACHE USHABIKI VINGINEVYO NCHI HII ITAZIDI KUYUMBA.

    ReplyDelete
  19. Net Force CommanderMay 27, 2009

    Kauli za VIREMBA VYA UKOKA haziwezi kupewa nafasi.. VITA imeshatangazwa na sasa ni MAPAMBANO kwa kwenda mbele.

    Ni hadi hapo Amiri Jeshi wetu Mkuu Mtukufu ISSA MUHIDIN MISUPU a.k.a nanii OBAMA atakapo TOA AMRI ya kusitisha MASHAMBULIZI ya KUJIBU MAPIGO na KUMTIA NGUVUNI kiongozi wa kikundi kidogo cha KIJIJI FORUM a.k.a AL QAIDA, Bw. MWANAKI-JAMII a.k.a OSAMA.

    MISUPU BLOG FOREVER..haterz forum DIE SOON!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 27, 2009

    Mdau Mswahili nakupa tano zidi kuwachana hao JF- NGO ya CHADEMA wamezidi majungu wenyewe kila linalofanywa na serikali ni baya tu kazi yao ni kuikashifu serikali na viongozi wake hata pale pasipostahili, na kuisifia chadema na huyo dj wao, sasa wanataka kuhamishia majungu yao kwa michuzi madaraka hayatafuti kwa njia hiyo watu wameshawastukia nyie na hao wafadhili wenu, na kumbukeni aliyepandishwa na mungu binadamu hawezi kumshusha, Michuzi uko juu JK uko juuuu mungu atawalinda na jicho la mahasidi

    ReplyDelete
  21. Advocate JashaMay 27, 2009

    Umesema kweli mwanakijiji na nakubaliana nawe na namuunga mkono na kutoa shukurani kwa mbunge wa naninhi kwa kazi kubwa anayoifanya .wakati wote anatumia nafasi kiduchu kila inapopatikana kuwasiliana na watanzania anapokua kwenye msafara wa rais au wakati wowote anapopata nafasi ujitahidi kuua ndege wawili kwa jiwe moja.Mbali na kupiga picha matukio ya rais ujitahidi kuwasiliana na watanzania na kupata picha mawazo na vidio mbalimbali kuhusu shughuli zao huko ugahibuni au kwingineko.Hali ambayo ni tofauti na waandishi wengine ambao wao kamera au video kamera zinachukua picha au video ambapo yupo rais.HONGERA KAKA MICHUZI USIFE MOYO MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 27, 2009

    JAMAA ANAYEJIITA MDAU MSWAHILI INAONEKANA ANA SHIDA NA MWANAKIJIJI. USILETE MATATIZO YAKO HAPA. UNAMLAUMU MWANAKIJIJI KWA KUTUMIA MAJINA BANDIA JE NA WEWE MDAU MSWAHILI NDILO JINA LAKO? AMA KWELI NYANI HAONI KUNDULE

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 27, 2009

    MUGEREZI.
    MICHUZI NI JINA LAKE SIO JINA LA BANDIA KAMA MWANAKIJIJI.

    MIE MSWAHILI NIKIPELEKA HABARI KWENYE GAZETI LOLOTE MAKINI KAMA HABARI LEO,MTANZNAIA,MWANANCHI AU RAI WITH EXCEPTIONAL OF TANZANIA DAIMA HAWAWEZI KUITOA HABARI YANGU KWA JINA LA UBABAISHAJI KAMA MWANAKIJIJI AU WAKATI MWINGINE ANAANDIKA KWA JILA LA MPAYUKA HOVYO KWENYE TANZANIA DAIMA.

    MAADILI YA UANDISHI HAYAKUBALI NA HAYARUHUSU.KIBANDA AMEKUWA AKINUNGUNIKA SANA.

    MWANAKIJIJI SIO MWANDISHI BY PROFESSIONAL LAKINI AMEKUWA AKIPIGA SIMU TANZANIA DAIMA NA KULAZIMISHA HABARI IKOTE AU ISIHARIRIWE.
    KISA YUKO KARIBU NA MBOWE.LAKINI MBOWE SI MWANDISHI.AWAACHIE WATALAAM WAFANYE KAZI ZAO.

    LIKITOKEA LOLOTE ANAYEJULIKANA NI KIBANDA SIO MBOWE.

    MIMI MSWAHILI NIKIJIFANYA MWANDISHI NA NIKITAKA KUANDIKA LAZIMA NITUMIE JINA LANGU LA ASILI SIO PEN NAME.

    SIO SIRI JAMII FORUM NI MALI YA WACHAGGA.

    NA MAKALA YA MWANAKIJIJI KUTETEA WIZI AU UFISADI WA MBOWE KUIBA NSSF YAPO KULE HADI SASA.

    NI DENI TOKA 1990 LINA MIAKA 19 NA HATAKI KULIPA AMA KWELI HAKUNA MCHAGGA MUAMINIFU,YULE MWINGINE TOKA ACHUKUE MKOPO NBC 1986 HADI BENKI IMEKUFA HATAKI KULIPA.

    ANAMTETEA SANA MENGI KUWA NI MZALENDO KWA VILE TU ANAIFADHILI JF.

    MWANAKIJIJI HUYO HUYO KILA SIKU ANAFUNGUA MABLOG YANAKUFA NA KUANZISHA MAPYA KWA KUKOSA WATU,

    HIVI SASA ANATUKA KIGAZETI CHA CHECHE KWENYE EMAIL ZA WATU KILA JUMANNE KUMPONDA JK NA SERIKALI YAKE.

    KAMA HANA PAKULALA AU ANAISHI KWA SHIDA DETROIT KWA KINA MFINANGA HAWEZI KUWA NA MAWAZO HURU,KWANI KILA ANACHOANDIKA ANAWAZA ASIMUUDHI MBOWE NA MZEE WA KUTAKA SYMPATH KWA WANANCHI KWANI NDIO WAFADHILI WAKE,

    HUJUI KUWA MTIKILA NJAA YAKE ILIMPONZA KWA ROSTAM AZIZI?UKIWA NA NJAA UNAKUWA MTUMWA,UMASIKINI NI UTUMWA.

    LAKINI HAJACHELEWA KWANINI ASIRUDI NYUMBANI HARAKA AKAWA PA WA MBOWE? AU CHADEMA WAMPE AWE AFISA UHISIANO WAO.AKIFIKA MAKAO MAKUU YA CHADEMA NDIO ATAJUWA KUWA LILE NI ENEO LA WACHAGGA,WATAMNYANYASA ATABAKI KUJUA.
    KUNA MTU KASEMA MWANAKIJIJI NI SIMBA MIE NASEMA NI FISI KAMA ANGEKUWA SIMBA ANGETUMIA JINA LAKE HALISI KAMA KINA KUBENEA.

    MWENYEZI MUNGU MBARIKI RAIS OBAMA AWAPE AMNESTY WOTE ILLEGAL IMMIGRANTS WALIOKO MAREKANI WAWEZE KUJA NYUMBANI,KUONA NDUGU ZAO,KUWAONA WAFADHILI WAO USO KWA MACHO,KUSHIRIKI KAMPENI ZA VYAMA ZAO WAKIWA KWENYE GROUND KULIKO KUSHINDA KWENYE MABLOG KUWATUMIA WANACHAMA WENZAKE.

    PIA WAWEZE KUONA MAKABURI YA NDUGU ZAO AMBAO KILA INAPOTOKEA MISIBA BASI WAO UWEZO WAO NI KUTUMA UBANI WA DOLA HAMSINI KUPITIA WESTERN UNION TU. NI MAISHA MAGUMU YAKUJITAKIA.


    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 27, 2009

    hawa akina mwanakijiji ndio ndumila kuwili!
    wanauma na kupulizia!

    na nina wasi wasi ndio mabingwa wa habari mbofu mbofu kuhusu balozi na mkuu wetu wa wilaya ya tegeta.

    wape kisogo bro Mich-use!

    hawana lolote.
    kwanza wapo nje ya inzi hawajui chochote kuhusu tanzania.
    hata uchungu wanaojifanya wanao hawana hata sudusu/punje!

    kama wanao waje tuwapeleke muhimbili wodi la wazazi.

    wanapenda watoto na ndugu wa masaki na oBay ndio wafanikiwe au wawe na maisha poa!

    mtoto wa Nzese au tandika aki--WIN unawasikia..
    ohoooooo jamaaa kaanza kuuza unga!
    ..jamani KAZI ni kichwa chako tu!
    Bidiii na maarifa hata watoto wa Manzese tunazo!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 27, 2009

    mwanakijiji utajuuuuta kumuandikia michuzi. ona sasa mashambulizi haya. kila anaetoka anatoka kivyake. hasa huyo anayejiita mswahili kakuchanachana vibaya.
    dah pole mzee. Kwani jina lako halisi ni nani na unaishi wapi??

    ReplyDelete
  26. Ndugu mwanakijiji, ikiwa hauna uoga wowote, basi weka jina lako. kwani waandishi wenye nia njema kama kubenea siku zote tunaona majina yao......

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 28, 2009

    Wakuu wote Michuzi Blog, ninapenda kuweka marekebisho kidogo, huko juu kuna mtu ametumia jina langu la bandia kule JF, yaani Field Marshall Es, ukweli ni kwamba sio mimi Mkulu mwenyewe, kuna mtu anayejaribu sana na kwa muda mrefu kuharibu hilo jina langu la bandia,

    - Sina noma na Mkulu Michuzi maana tunatoka mbali sana, enzi za YMCA disco toto, la Born City na Dj Kali Kali na Nigger Jay, pamoja na Mkulu Shebby B, John Peter Pantalakis, kina Choggy Sly, Chris Phaby, Jerry Koto, Seydou hawa wote ni ndugu zangu sana na hata siku moja siwezi kuwa na noma na mmojawapo.

    - Naomba niombe radhi kwa yoyote aliyesumbuliwa in any way or form na maneno ya huyo mkuu, aliyetumia jina langu, otherwise tupo pamoja wakuu, na karibuni sana JF.

    Respect.

    Field Marshall Es, Original!

    ReplyDelete
  28. mzuri kukuu anataga mayaiMay 28, 2009

    japo nina machungu ya kufungwa na barca
    mdau mswahili nakupa tano la nguvu...endelea kumchana, and you need not display your real name coz these are just forumites but when you post issues kwenye magazeti then by all means !heheheh mdau nakupa hi 5 huyo mwanakijiji kama kidume aseme jina lake... haangaliwi mtu usoni... heheh

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 28, 2009

    michuzi iz a nice guy...

    sema tatizo lako ni kula na mafisadi tuuuu....

    zikitolewa habari za mafisadi lazima ubanie michuzi vibaya hivyooooo

    ccm ni wizi mtupuuu!

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 28, 2009

    JAMANI TUJIFUNZE SASA TUWE MAKINI TUSIJE TUKAPUNGUKIWA NA WAGEMA WETU HODARI. TUPUNGUZE KUWASIFIA ILI UBORA WA TEMBO WANALOTUGEMEA UWE WA NGUVU ZAIDI.
    PAPA WAMBA DIA WAMBA

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 29, 2009

    PEOPLE ARE OBSSESED WITH MWANAKIJIJI, THE GOOD THING MWANAKIJIJI NIMJUAYE HAWEZI KUJA KUBISHANA NA LOW PEOPLE KAMA MSWAHILI, NI WATU WAWILI TOFAUTI KABISA! FOR ME MWANAKIJIJI IS A HEROE AND A ROLE MODEL

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 29, 2009

    MSWAHILI UKO OBSESSED NA MWANAKIJIJI DUH, MARA BEN MWALUSAKA NAKUMBUKA ULISHAWAHI KUJA NA HOJA KWAMBA MWANAKIJIJI NDIYE JOHN MASHAKA, POOR MSWAHILI

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 30, 2009

    mwanakijiji ni hero na role model...hahahahah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...