Mwenyekiti wa Jumuiya ya wabongo nchini Malaysia Mh. Pius Mikongoti akitoa hotuba kabla ya sherehe kuanza rasmi.
Kwa mara nyingine tena Jumuiya ya Mabalozi toka Africa walioko Malaysia wamefanikisha ile siku ya African Day katika Hotel ya Marriott hapa Kuala Lumpur Malaysia iliyofanyika jana.
Ni siku ambayo inakutanisha waafrika walioko Malaysia na kusherehekea na kubadilishana mawazo. Balozi wa Tanzania hapa Malaysia Mh. Abdul Sisco Mtiro hakuhudhuria sherehe hizo kwani yuko nchini Cambodia alikokwenda kuwakilisha hati zake za utambulisho wa Ubalozi kwani Mh. Cisco anawakilisha Malaysia, Singapore, Cambodia, Laos, Philipines na Indonesia.
Kulikuwa na maonyesho ya vitu tofauti tofauti kutoka mataifa tofauti na nchi mbali mbali zilikuwa na meza zao ambapo walitambulisha nchi zao ama kwa utamaduni au kwa vivutio vya aina mbali mbali ukiwemo Utalii,
Sherehe hizi huwa zinaandaliwa kwa pamoja na mtandao wa Mabalozi wa Afrika waliko Malaysia na kugharamiwa na mtandao huo pia bila kiingilio kwa kinywaji au kilaji, ambapo waafrika hukutana na chakula toka kila pembe ya Afrika huwepo pia.
Mh. Pius akiwa na Balozi wa Swaziland Malaysia akiwa na mkewe na mwanaye kwenye sherehe hiyo iliyofana kupita kiasi.
palipambwa na kupambika



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2009

    jamani uheshimiwa si mchezo. siku hizi cv yake si kulala makaburini na kuamkia watoto wadogo tu bali kuna kuzomewa pia.
    haya, mh. pius mikongoti wa malaysia, uheshimiwa huu umeutoa wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...