Nicheke ninenepe!
wakati mjadala unaendelea kuhusu vekesheni ya balozi wa nanihino ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Nanihii, Kaka braza kakimbilia studio kufyatua wimbo mpya uliobeba jina la "Kizabi Zabina" si mtu Mwema!
Kizabi zabina huyo alitajwa kwa jina la Binti Pazi au Mzee pazi, analalamikiwa na kiongozi wa bendi ya ngoma africa ras makunja kwa kuigombanisha jamii na kuwa sumu ndani jamii.
Wadaku walioshuhudia madongo makali yalikuwa yakirushwa na mwanamziki huyo katika studio huko ughaibuni.wamebaki midomo wazi kutokana na uzito wa madongo na hoja zilizojaa ukweli ukweli kuhusu "Kizabi Zabina", huyo Bint Pazi aka Mzee Pazi.
Kiongozi wa Ngoma Africa Ras Makunja kamshitaki kwa jamii "Kizabi Zabina" kwa kosa la kuichonganisha jamii, tena kampa Shua kwa kumwambia "atafute la kufanya" na "kuwekeza mda mwingi katika maendeleo".
Watafiti wa mambo wanadai kuwa Ras makuja na kitu kipya hiko "Kizabi Zabina" kinaifanya bendi ya The Ngoma Africa yenye maskani ughaibuni kuonekana kuwa karibu sana na jamii ya Uswahilini kwa tungo zake ambazo mara nyingi zina elimisha,au kuishauri jamii ,wakati mwingine ni mwaliko wa malumbano ya hoja .
-MDAU MSEMAKWELI
KIZABI ZABINA NI BENEDICT MWAKYANJALA MAARUFU KAMA MWANAKIJIJI AU KADA WA CHADEMA TAWI LA JAMII FORUMS.
ReplyDeleteMDAU MSWAHILI.
Yusuph mzee wa jahazi modern Taarab aliimba wimbo unaitwa two in one au MPEKEPEKE.
ReplyDeletehivyo tumbatize Mwanakijiji kuwa ni MPEKEPEKE. na jamii forums yake.
haya jamaa sasa huyu ras makunja,anatuacha hoi na hii mpya yake! lakini sidhani kama anamlenga
ReplyDeleteMwakyanjala.Lakini makunja hizi ndizo
zake akawizi mambo.
Kinachonishangaz ni wimbo huu wa kizabi zabina,mbona yeye mwenyewe watu hawamlalamiki kwa tabia zake za kuwarushia watu madongo.
mdomo wa kaka bro ras makunja kweli haukawizi mzozo,ukisikia uwanamziki ndio huu!? ndogo juu ya madongo.Kaka rusha madongo
ReplyDeletehiiiiii!!!!!!te te! kamanda Ras makunja,nakukubali kazi zako ni muhimu kwa jamii hii ya wabongo,siku hizi fitina,majungu yapo mpaka kwa watu tunaowaita WASOMI,badala kuleta maendeleo wao ndio wapo mstari wa mbele katika fitina na majungu,bora ulivyohamua kuwafungia kibwebwe
ReplyDeletehapa braza kaka ras makunja !!!!!!unanipa kigugumizi na kazi yako ya Undewa au mjumbe wa kuhamua maswala ya jamii!!!! hule ugomvi wa wafanyibiashara juzi tu ulichomoa kibao kipya FURAHA YA MAISHA IKO WAPI? sasa hili soo la vakasheni ya misupu naona unarusha dongo jingine! ninakupigia saluti.
ReplyDeletemmmmmmmmmm!!!vakasheni ya balozi kweli imezua mambo.sasa kesi hipo kwa jamii? mungu wangu,nangoja nimsikilize ras na ffu wake wanapompiga virungu kizabi zabina.
ReplyDeletekweli ngoma inogoge
hiiiiiiiiii leo ! Kizabi zabina mzee Pazi kakumbana na ffu..........sasa kazi hipo,ras rusha mawe yamfikie huyo kizabi zabina
ReplyDeleteRas Makunja kwa nini? kesi hii msipeleka mahakamani badala yake mnaanza zogo kwa kuwapa waswahili wahamue?wakati wewe mwenyewe unajua wazi huku uswahili Vizabi zabina ndio kwao.Kaka naona umedhamiria kuleta zogo uswahilini.
ReplyDeletelakini we haya tutafika tu
hii imekaaje? tulisikia nyie ngoma afrika siku hizi mna adabu na hakuna tena kurusha mawe?sasa huyu mzee pazi mbona anatupiwa matofali?jamani msalieni mungu
ReplyDeletehii bwana nzee kizabi zabina na bw.kichwa ngumu hili ni soooo la kukata na mundu,sasa tuone nani ?mwenye haki.ngoma afrika mna mdomo!haki ya mama
ReplyDeletehili bifu la nguvu ffu na mzee pazi,mie yangu masikio.
ReplyDeleteMdau wa msondo,Buguruni.
kizabizabina si mtu kabisa kwa nini? Michuzi unakaa meza moja na kizabizabina na kula naye msosi.
ReplyDeletesasa unaona maneno yamefika kwa afande na kamanda anayepeleka adharani.
mzee kizabizabi na kaka mwenye gubu kubwa,ngoma uwanjani
ReplyDelete