KOCHA WA TAIFA STARS MARCIO MAXIMO AKIWA NA RODRIGO STOKLER (KOCHA WA VIJANA, KATI) NA MARCELO GUERREIRO (KOCHA WA MZAOEZI YA VIUNGO, KULIA) WOTE KUTOKA BRAZIL MARA BAADA YA KUTUA USIKU HUU DAR TAYARI KWA KUANZA KAZI.
MAKOCHA HAWA WATAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI JUMATATU KUELEZEA MIKATABA NA MIKAKATI YAO.
WAMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA WANAFURAHI KUTUA BONGO NA PIA WAMEISIFIA HALI YA HEWA YA BONGO WAKISEMA NI KAMA YA KWAO BRAZIL NA NDIO YENYEWE KWA KUTANDAZIA BOLI.
KOCHA STOKLER KASEMA HII SI MARA YAKE YA KWANZA KUKANYAGA AFRIKA, KWANI ALIWAHI KWENDA SAUZI NA KWAMBA HIVI SASA KATOKEA CHINA ALIKOKUWA AKIFUNDISHA VIJANA KWA MIAKA MITATU.
MWENZIE KASEMA HII NI MARA YA KWANZA KUTUA AFRIKA NA AMESIFIA UKARIMU WA WABONGO ALIOANZA KUUONA TOKA ALIPOTUA.
KWA KUWA WAMECHOKA KWA WAMEOMBA WAPUMZIKE HIVYO STORI HAZIKUWA NDEFU SANA...
KOCHA STOKLER ATACHUKUA NAFASI YA KOCHA WA VIJANA WA ZAMANI TOKA BRAZIL PIA, MARCUS TINOCO, ALIYETIMKA MWANZONI MWA MWAKA HUU, WAKATI GUERREIRO ATAJAZA PENGO LILILOACHWA WAZI NA ITTAMAR AMORIM , MBRAZIL MWINGINE ALIYEKUJA NA MAXIMO WAKATI ULE, NA SASA ANAINOA AZAM FC BAADA YA NEIDER DOS SANTOS KUTIMULIWA BAADA YA PAFOMANSI YAKE KUTORIDHISHA KATIKA LIGI KUU. HAYA TENA WADAU, HABARI NDIYO HIYO....
MAKOCHA HAO WAKIONGEA NA GLOBU YA
JAMII MARA BAADA YA KUTUA DAR LEO
Mwalimu wa mazoezi ya viungo ana kitambi!!!! Kasheshe.
ReplyDeleteLakini hata nyusi zake ni nene. Labda ni genes zake.
bwana haya mambo ya kuchemka.kucheza mpira na kufundisha mpira vitu viwili tofauti.brasil wazuri kwa kucheza ila sio sababu ya kila kocha mtafute toka brasil..ni sawa na kusema kenya ni wakimbiaji wazuri basi kama mnataka kocha wa mbio lazima atoke kenya.fungua macho
ReplyDeleteMakocha wa kibongo hapo wataanzisha bifu tena... hivi kuna kocha yeyote mbongo anaweza kazi?
ReplyDeletekwa hiyo hapa pasu la maximo sh. ngapi kwa kuwaleta hawa jamaa?
ReplyDeleteKwa ubinafsi na ubishi wa maximo hawa nao hawatakaa sana! Utasikia wamechukuliwa na African Lyon!!! halafu CV zao zikoje?
ReplyDeleteWanotoka wapi hawa wote!? mamaaaaaaaa! Ishakua kasumba sasa!
ReplyDeleteNjaa kali
ReplyDeleteMaximo "Rodrigo na Marcelo njooni huku kuna ulaji. Mwenyewe kalala hata akiamka hana noma"
ReplyDeleteWauza Nyunga Tu Hao
ReplyDeleteMaximo sio kocha hivyo ataleta watu kama yeye wasiojua kitu.
ReplyDeletehadi sasa hajafanikiwa kitu chochote kwenye timu ya taifa.
first coach....mbwiiiiiii sijui kamalizaje safari yake bila kudakuliwa. angekuwa katua EU WAUNYA WANGEKULA NAE SAHANI MOJA
ReplyDeleteHee, huyo Kocka mmoja wapo hapo mbona BONGE kiasi hicho? Mchaka-mchaka wa soka atauweza? Tuombe hivyo!!!
ReplyDeleteUkocha ni kazi ya kitaaluma kama ilivyo uanasheria au udaktari. Huwezi kusema kwamba Brazil haitoi makocha wazuri. Ni sawa na kusema Tanzania haitoi madaktari wazuri. Kuna madokta wa kibongo kibao wanafanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi. Kuna madokta kibao wa kibongo wanaitilia aibu fani. Huwezi kutaka kupewa timu ya taifa uifundishe kwa kudai tu nipeni timu muone. Makocha wetu waimarishe wasifu wao. Unaweza kuchukua ubingwa wa Afrika na klabu yoyote. Unaweza kufanya alivyofanya Jamhuri Kihwelo na kutafuta mafanikio nje ya bara la Afrika. Ukifanya hayo halafu ukadai upewe timu ya taifa walau unaweza kutetea hoja yako.
ReplyDeleteWewe uliyeona kama kuna mtu ana kitambi nakushauri ukamuone daktari wa macho.
ReplyDeleteHIVI HAWA MAKOCHA TFF NDIO WANAWATAFUTA AU MAXIMO MWENYEWE? ASIJE AKAWA ANAWALETA NDUGU ZAKE KULA ULAJI.MANAKE KOCHA WA MAZOEZI ANA MWILI MKUBWA HIVYO AU ANAFUNDISHA MAZOEZI DARASANI?
ReplyDeleteKWELI YULE MZUNGU ALIYESEMA "TANZANIA NDIO NCHI PEKE YAKE DUNIANI UNAWEZA KUINGIA NA DOLLAR 5 UKAONDOKA MILIONEA".
KINACHOBOA NI UBRASIL..UBRASIL..KAMA WATU WAWILI WALIVYOSEMA HAPO JUU.TAFUTA KOCHA YEYOTE MWENYE CV MLIPE UNAJUA UNAMLIPA MTU UNAYEJUA ANAFAHAMU KITU ANACHOKIJUA
ReplyDeleteLugha tu yenyewe shida, atawafundishaje sasa, duh bongo kwa kuvizia mizoga hawajambo, mh kazi ipo!!
ReplyDeleteyani jinsi wanavyoongea tuu wanaoneka ni wasaniii.. hakuna makocha hapo!! wizi mtupu
ReplyDelete