KOCHA WA TAIFA STARS MARCIO MAXIMO AKIWA NA RODRIGO STOKLER (KOCHA WA VIJANA, KATI) NA MARCELO GUERREIRO (KOCHA WA MZAOEZI YA VIUNGO, KULIA) WOTE KUTOKA BRAZIL  MARA BAADA YA KUTUA USIKU HUU DAR TAYARI KWA KUANZA KAZI. 

MAKOCHA HAWA WATAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI JUMATATU KUELEZEA MIKATABA NA MIKAKATI YAO. 

WAMEIAMBIA GLOBU YA JAMII KWAMBA WANAFURAHI KUTUA  BONGO  NA PIA WAMEISIFIA HALI YA HEWA YA BONGO WAKISEMA NI KAMA YA KWAO BRAZIL NA NDIO YENYEWE KWA KUTANDAZIA BOLI. 

KOCHA STOKLER KASEMA HII SI MARA YAKE YA KWANZA KUKANYAGA AFRIKA, KWANI ALIWAHI KWENDA SAUZI NA KWAMBA HIVI SASA KATOKEA CHINA ALIKOKUWA AKIFUNDISHA VIJANA  KWA MIAKA MITATU.

MWENZIE KASEMA HII NI MARA YA KWANZA KUTUA AFRIKA NA AMESIFIA UKARIMU WA WABONGO ALIOANZA KUUONA TOKA ALIPOTUA.

KWA KUWA WAMECHOKA KWA WAMEOMBA WAPUMZIKE HIVYO STORI HAZIKUWA NDEFU SANA...

KOCHA STOKLER ATACHUKUA NAFASI YA KOCHA WA VIJANA WA ZAMANI TOKA BRAZIL PIA, MARCUS TINOCO, ALIYETIMKA MWANZONI MWA MWAKA HUU, WAKATI GUERREIRO ATAJAZA PENGO LILILOACHWA WAZI NA ITTAMAR AMORIM , MBRAZIL MWINGINE ALIYEKUJA NA MAXIMO WAKATI ULE, NA SASA ANAINOA AZAM FC BAADA YA NEIDER DOS SANTOS KUTIMULIWA BAADA YA PAFOMANSI YAKE KUTORIDHISHA  KATIKA LIGI KUU.  HAYA TENA WADAU, HABARI NDIYO HIYO....

MAKOCHA HAO WAKIONGEA NA GLOBU YA
 JAMII MARA BAADA YA KUTUA DAR LEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2009

    Mwalimu wa mazoezi ya viungo ana kitambi!!!! Kasheshe.

    Lakini hata nyusi zake ni nene. Labda ni genes zake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2009

    bwana haya mambo ya kuchemka.kucheza mpira na kufundisha mpira vitu viwili tofauti.brasil wazuri kwa kucheza ila sio sababu ya kila kocha mtafute toka brasil..ni sawa na kusema kenya ni wakimbiaji wazuri basi kama mnataka kocha wa mbio lazima atoke kenya.fungua macho

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2009

    Makocha wa kibongo hapo wataanzisha bifu tena... hivi kuna kocha yeyote mbongo anaweza kazi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2009

    kwa hiyo hapa pasu la maximo sh. ngapi kwa kuwaleta hawa jamaa?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2009

    Kwa ubinafsi na ubishi wa maximo hawa nao hawatakaa sana! Utasikia wamechukuliwa na African Lyon!!! halafu CV zao zikoje?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2009

    Wanotoka wapi hawa wote!? mamaaaaaaaa! Ishakua kasumba sasa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2009

    Njaa kali

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2009

    Maximo "Rodrigo na Marcelo njooni huku kuna ulaji. Mwenyewe kalala hata akiamka hana noma"

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2009

    Wauza Nyunga Tu Hao

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2009

    Maximo sio kocha hivyo ataleta watu kama yeye wasiojua kitu.
    hadi sasa hajafanikiwa kitu chochote kwenye timu ya taifa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2009

    first coach....mbwiiiiiii sijui kamalizaje safari yake bila kudakuliwa. angekuwa katua EU WAUNYA WANGEKULA NAE SAHANI MOJA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2009

    Hee, huyo Kocka mmoja wapo hapo mbona BONGE kiasi hicho? Mchaka-mchaka wa soka atauweza? Tuombe hivyo!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2009

    Ukocha ni kazi ya kitaaluma kama ilivyo uanasheria au udaktari. Huwezi kusema kwamba Brazil haitoi makocha wazuri. Ni sawa na kusema Tanzania haitoi madaktari wazuri. Kuna madokta wa kibongo kibao wanafanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi. Kuna madokta kibao wa kibongo wanaitilia aibu fani. Huwezi kutaka kupewa timu ya taifa uifundishe kwa kudai tu nipeni timu muone. Makocha wetu waimarishe wasifu wao. Unaweza kuchukua ubingwa wa Afrika na klabu yoyote. Unaweza kufanya alivyofanya Jamhuri Kihwelo na kutafuta mafanikio nje ya bara la Afrika. Ukifanya hayo halafu ukadai upewe timu ya taifa walau unaweza kutetea hoja yako.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 03, 2009

    Wewe uliyeona kama kuna mtu ana kitambi nakushauri ukamuone daktari wa macho.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 03, 2009

    HIVI HAWA MAKOCHA TFF NDIO WANAWATAFUTA AU MAXIMO MWENYEWE? ASIJE AKAWA ANAWALETA NDUGU ZAKE KULA ULAJI.MANAKE KOCHA WA MAZOEZI ANA MWILI MKUBWA HIVYO AU ANAFUNDISHA MAZOEZI DARASANI?
    KWELI YULE MZUNGU ALIYESEMA "TANZANIA NDIO NCHI PEKE YAKE DUNIANI UNAWEZA KUINGIA NA DOLLAR 5 UKAONDOKA MILIONEA".

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2009

    KINACHOBOA NI UBRASIL..UBRASIL..KAMA WATU WAWILI WALIVYOSEMA HAPO JUU.TAFUTA KOCHA YEYOTE MWENYE CV MLIPE UNAJUA UNAMLIPA MTU UNAYEJUA ANAFAHAMU KITU ANACHOKIJUA

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2009

    Lugha tu yenyewe shida, atawafundishaje sasa, duh bongo kwa kuvizia mizoga hawajambo, mh kazi ipo!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 04, 2009

    yani jinsi wanavyoongea tuu wanaoneka ni wasaniii.. hakuna makocha hapo!! wizi mtupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...