JAJI Mkuu Mh. Augustino Ramadhani  (pichani juu) leo ameongoza maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam katika mazishi na maziko ya Wakili maarufu nchini, Moses Maira (65) .

Wakili huyo aliyeaga dunia nchini Marekani na alizikwa leo katika makaburi ya Kinondoni. Alifariki Aprili 21 mwaka huu katika Hospitali ya Bentab Memorial ya mjini Houston, Texas Marekani.
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambacho kiliandaa shughuli ya kumuaga Maira kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, kilimwelezea mwanasheria huyo kuwa alianza kazi ya uwakili wa kujitegemea mwaka 1980. Maira alikuwa wakili wa 102 kati ya mawakili 1,075 ambao wamesajiliwa Tanzania Bara na Mahakama Kuu.

Maira alikuwa na Shahada ya Uzamili katika sheria aliyoipata nchini Uingereza. Alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1970 katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki ambacho sasa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wasifu wake unaonyesha kuwa Maira alizaliwa katika Kijiji cha Makojo, Majita katika Wilaya ya Musoma Vijijini mwaka 1944.

mawakili kibao walijitokeza kumuaga na baadaye kumzika msomi mwenzao
Jaji Mkuu Mh. Augustine Ramadhani akiwa na Jaji Mkuu mstaafu Mh. Barnabas Samatta na Mh. Jji Damian Lubuva na Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama kuu wakiwa msibani
wasomi wenza wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni Mh. Mirambo (kati) akisoma wasifu wa Hayati Maira
Mh Pius Msekwa (kulia) na Mh. John Cheyo (shoto) wakitoa heshima zao za mwisho
watoto wa marehemu wakitoa shukrani kwa waombolezaji

Mjane wa marehemu (wa pili shoto) na ndugu wa karibu
mawakili wakitoa heshima zao za mwisho
heshima za mwisho
mawakili toka kila pembe ya nchi walikuwepo kumuaga msomi mwenzao
baadhi ya mawakili
mawakili na marafiki wakingoja zamu zao kuaga

waombolezaji walikuwa wengi sana
waombolezaji wakiwa katika foleni ya kutoa heshima za mwisho
waombolezaji



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2009

    Poleni sana wafiwa! Mwenyezi Mungu awape nguvu kipindi hiki cha huzuni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2009

    msomi, wasomi, ...

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2009

    RIP advocate Maira.. Namkumbuka Arnold mtoto wa marehemu, we were 2gether miaka ile pale TAMBAZA! Pole sana Arnold..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2009

    Pumzika, yego wa Maira awe!

    Tangu tukiwa Tabora School
    Hadi Mlimani kutoka

    ...rest in PEACE!

    BAP

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2009

    RIP Maira

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2009

    Jamani Arnold pole sana . Sijakuona sikunyingi. Nitajitahidi kuja kukuona .Dororosa

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2009

    Jamani Arnold pole sana . Sijakuona sikunyingi. Nitajitahidi kuja kukuona .Dororosa

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2009

    Mungu awape nguvu wafiwa kwenye kipindi huki kigumu RIP advocate maira

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2009

    Poleni sana jamii ya wasomi. katika fani ya sheria jamaa alikuwa kichwa. Ila nimesikitika kwamba hawakumfanyia haki zombe. Alitakiwa awepo hata kwa kutoa heshima za mwisho na kisha arudishwe gerezani. Ni mtu wake jamani

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2009

    Poleni ndugu na majamaa. Kwa watoto wa marehemu , kumbukeni nyakati mlizokuwa na mzee wenu mrafarijika. Mungu amrehemu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2009

    michuzi hufai kuwa blogger kwa nini unapost comment zinazokufurahisha wewe tu na kila siku unadai blog ya jamiii...hamna lolote ufisadi tu.....democracy zero
    By the way i wish my condolences to the entire Maira family

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2009

    Jamani poleni na msiba huu. Arnold na mkewe Binti wa kavishe poleni sana.Tambaza yooooooo

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2009

    Pole Dofi Maira (Adrofina).Tulisoma wote Nganza high school,Bwana alitoa na bwana ametwaa.May your father's memories guide you forever. Dofi, i'm with you in prayers.
    Mdau GJ(someone)
    New York.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2009

    Pole sana nancy na scott moses maira kwa msiba wa baba yenu . Hamkuweza kurudi kwenye msiba lakini nilimpa pole mama yenu. You had a good daddy. I remember when i came to visit you all at boston university. Mlikuwa mnakwenda. Likizo kumuona baba yenu. God took him to rest in peace. I will call you

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 05, 2009

    anonymous wa mwisho you could have written an e-mail or phone the wafiwas,wanakujua unawajua why hide yourself under anonymous? i think if they are your friends/relatives this is the time to show your sympathy openly and not hide,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...