JAJI Mkuu Mh. Augustino Ramadhani (pichani juu) leo ameongoza maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam katika mazishi na maziko ya Wakili maarufu nchini, Moses Maira (65) .
Wakili huyo aliyeaga dunia nchini Marekani na alizikwa leo katika makaburi ya Kinondoni. Alifariki Aprili 21 mwaka huu katika Hospitali ya Bentab Memorial ya mjini Houston, Texas Marekani.
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambacho kiliandaa shughuli ya kumuaga Maira kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, kilimwelezea mwanasheria huyo kuwa alianza kazi ya uwakili wa kujitegemea mwaka 1980. Maira alikuwa wakili wa 102 kati ya mawakili 1,075 ambao wamesajiliwa Tanzania Bara na Mahakama Kuu.
Maira alikuwa na Shahada ya Uzamili katika sheria aliyoipata nchini Uingereza. Alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1970 katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki ambacho sasa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wasifu wake unaonyesha kuwa Maira alizaliwa katika Kijiji cha Makojo, Majita katika Wilaya ya Musoma Vijijini mwaka 1944.
Poleni sana wafiwa! Mwenyezi Mungu awape nguvu kipindi hiki cha huzuni.
ReplyDeletemsomi, wasomi, ...
ReplyDeleteRIP advocate Maira.. Namkumbuka Arnold mtoto wa marehemu, we were 2gether miaka ile pale TAMBAZA! Pole sana Arnold..
ReplyDeletePumzika, yego wa Maira awe!
ReplyDeleteTangu tukiwa Tabora School
Hadi Mlimani kutoka
...rest in PEACE!
BAP
RIP Maira
ReplyDeleteJamani Arnold pole sana . Sijakuona sikunyingi. Nitajitahidi kuja kukuona .Dororosa
ReplyDeleteJamani Arnold pole sana . Sijakuona sikunyingi. Nitajitahidi kuja kukuona .Dororosa
ReplyDeleteMungu awape nguvu wafiwa kwenye kipindi huki kigumu RIP advocate maira
ReplyDeletePoleni sana jamii ya wasomi. katika fani ya sheria jamaa alikuwa kichwa. Ila nimesikitika kwamba hawakumfanyia haki zombe. Alitakiwa awepo hata kwa kutoa heshima za mwisho na kisha arudishwe gerezani. Ni mtu wake jamani
ReplyDeletePoleni ndugu na majamaa. Kwa watoto wa marehemu , kumbukeni nyakati mlizokuwa na mzee wenu mrafarijika. Mungu amrehemu.
ReplyDeletemichuzi hufai kuwa blogger kwa nini unapost comment zinazokufurahisha wewe tu na kila siku unadai blog ya jamiii...hamna lolote ufisadi tu.....democracy zero
ReplyDeleteBy the way i wish my condolences to the entire Maira family
Jamani poleni na msiba huu. Arnold na mkewe Binti wa kavishe poleni sana.Tambaza yooooooo
ReplyDeletePole Dofi Maira (Adrofina).Tulisoma wote Nganza high school,Bwana alitoa na bwana ametwaa.May your father's memories guide you forever. Dofi, i'm with you in prayers.
ReplyDeleteMdau GJ(someone)
New York.
Pole sana nancy na scott moses maira kwa msiba wa baba yenu . Hamkuweza kurudi kwenye msiba lakini nilimpa pole mama yenu. You had a good daddy. I remember when i came to visit you all at boston university. Mlikuwa mnakwenda. Likizo kumuona baba yenu. God took him to rest in peace. I will call you
ReplyDeleteanonymous wa mwisho you could have written an e-mail or phone the wafiwas,wanakujua unawajua why hide yourself under anonymous? i think if they are your friends/relatives this is the time to show your sympathy openly and not hide,
ReplyDelete