BAADHI YA WAALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI ZA BUNDA DAY, MAKONDORO NA KWIRAMBA WAKIFURAHIA MSAADA WA KOMPYUTA 20 ZILIZOTOLEWA KWA SHULE HIZO NA VODACOM FOUNDATION
BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA BUNDA DAY,WAKIFURAHIA MSAADA WA KOMPYUTA 10 ZILIZOTOLEWA KWA SHULE HIYO NA VODACOM FOUNDATION
MBUNGE WA WILAYA YA BUNDA MH STEPHEN WASSIRA AKIKABIDHI KOMPYUTA KWA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA BUNDA DAY BI. BERNADETHA MAINDA(KUSHOTO)JUMLA YA KOMPYUTA 20 ZILITOLEWA NA VODACOM FOUNDATION KWA SHULE 3 ZA BUNDA DAY,MAKONDORO,KWIRAMBA

MENEJA WA VODACOM FOUNDATION AKIKABIDHI MSAADA WA KOPYUTA KWA MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MH.STPHEN WASSIRA(KULIA)ALIYEPOKEA KWA NIABA YA SHULE 3 ZA SEKONDARI ZA BUNDADAY,MAKONDORO NA KWIRAMBA ZILIZOPO WILAYANI HUMO.(KATIKATI)MKUU WA MKOA WA MARA KANALI MSTAAFU ERNOS MFURU.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    picha ya pili naona dole....
    inanikumbusha bali mjomba...
    na litakua la second master... hahahaha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    Haya makampuni ya simu Nchini Tanzania ni wezi tu. Wanajifanya kutoa misaada wakati wanawaibia wananchi wazi wazi katika uduma za simu. Tanzania ni nchi pekee inayoongoza kwa makampuni binafsi ya simu kuwatoza gharama za juu sana wateja wake. Kwanini uduma zote ni pre-paid. Nchini marekani prepaid service hipo kwa ajili ya wale wasioweza kupewa uduma kwasababu credit history ni mbovu na badala yake wateja hao upewa uduma kwa gharama za juu sana(pre-paid phone)

    Haya makampuni ya simu yanajua kuwadanganya wananchi wetu kama watoto wadogo na kuwaibia kila kukicha kwa kuwatumia watanzania wenzao walioajiliwa na hayo makampuni.

    Napendekeza serikali hiingilie kati swala hili sio tu kuwaacha wageni wakiwaibia wazawa eti kwa vile hawana watu wa kuwatetea.

    Kampuni ya simu ikiwa na wateja 2,000,000 na ikamuibia kila mteja mmoja sh.10 za kitanzania, kwa dakika moja inajipatia shillingi za kitanzania 20,000,000.00 kwa dakika moja. Je kampuni hiyo hiyo inajipatia shillingi ngapi kwa siku(24hours) kama dakika moja inaiba shillingi 20,000,000?

    Watanazania wenzangu, maesabu haya yanaweza kufanywa na mtu yeyote mwenye elimu kuanzia darasa la kwanza ilimradi ajue kusoma na kuandika.

    Makampuni yote ya simu kwenye nchi zote yanatakiwa kuwa chini ya uangalizi mkali wa serikali. Sio tu natoa maoni kuwaaribia biashala wenye makampuni ya simu bali ninaelewa ninachokisema kwasababu nimefanya kazi katika kampuni ya simu (T-Mobile) kwa mda usiopungua miaka saba hapa nchini Marekani na kitengo chetu kilikuwa ni cha uduma ya wateja na kila siku ilikuwa lazima tutoe taharifa katika ofice za IRS na kuonyesha jinsi gani tuna lipa kodi. Form tulizokuwa tunazijaza zinavipengele kibao vingi vyake vikiuliza jinsi uduma tunazozitoa zinavyoendana na malipo tunayowatoza wateja.

    Inaniuma sana ninapoona wananchi wenzagu wanaibiwa kwa kiasi kikubwa sana katika nchi yangu


    Mdau
    usa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Nimekupata mdau hapo juu, mimi nalia na garama za sim hapa bongo, kwakweli voucher ya 2,000/= inatumika kwa dakika chache tu hata kama ukiwasiliana na mtu wa mtandao mmoja.

    Angalau leo nimepata picha jinsi gani tunavyokamuliwa. Ukija katika suala la sms nalo balaa tupu, garama ni kubwa mno.

    Sijui tukimbilie wapi sie walala hoi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2009

    Haya na mkoa wa MARA unapendelewa, Semeni tena.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2009

    Wadau, hadi tuje kuamka nchi hii tumemalizwa, sio simu tu mbona hata madini yetu yanaibiwa tunajengewa barabara za vumbi na madarasa yasio na walimu!!,zahanati zisizo na wataalam. tutaendelea kuibiwa hadi basi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2009

    Nampenda sana misupu kwa kazi yake nzuri lakini itafikia wakati awaulize wote wanaotuma matangazo au ujumbe kama kweli wanatenda haki. Huu mtandao umekamata dunia nzima ndio maaana watu wengi wanaochangia wana akili zilizoenda shule.

    Mchangiajia uliyepinga swala la makampuni ya simu kuwaibia wananchi kwa kiwango cha juu mno namuunga mkono.

    huu ni ushenzi mtupu. Naona huyu mtumumishi wa serikali tena amewai kushika nazi za juu anaona sifa kukabizi compyuta kwa wananchi wakati anaelewa wananchi wanaibiwa. Mh. Rais mfukuze kazi mpumbavu huyu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2009

    Haya yote ni ya kweli. tuanakushukuru sana mdau. Mimi imebidi nitupe simu yangu kwasababu matumizi ya simu yangu yalikuwa yapo juu kuliko hata kodi ya nyumba yangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...