
Marehemu Kanda Abdallah
Habari zimeingia sasa hivi toka Sao Paulo, Brazil, kwamba mdau Kanda Abdallah Haule hatunaye tena baada ya kupigwa risasi 3 na watu wasiojulikana wa Brazil jioni ya siku ya jumatano hii iliyopita.
Inasemekana baada ya kudondoka chini akatokea mtu mwingine akammalizia kisu cha chembe tena kwenye sehemu ambayo wabongo hupenda kukutana ila sema siku hiyo wadau wengi walikuwa wanaangalia gemu la Barca na Chelsea sehemu nyingine.
Hiyo sehemu ya maafa ni katika mtaa ujulikanao kama Rio Branco na inasemekana palikuwa na wabongo watatu tu akiwemo marehemu na wakazidiwa nguvu.
Wadau waliowasiliana na globu ya jamii wametoa ombi kwa serikali kupitia ubalozi wetu uliopo Brasilia kuharakisha upatikanaji wa pasi za kusafiria za Tanzania kwani wengi wameshajaza fomu na kulipia lakini hadi sasa mwaka umepita haajapatiwa pasi, na wao wanaishi kwa kutembea na risiti mfukonu, jambo ambalo halisaidii endapo kunatokea shida.
mr.michuzi ubarikiwe sana,
ReplyDeletehuyu kijana namjuwa masikini alikuwa swaziland alikuwa mcheshi masikini na mpenda utani yaani nimesikitika jamani famili yake poleni sana jamani pamoja na marafiki zake poleni sana
bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe
poleni, ila unatuchanganya, kutokuwa na pasipoti ndio sababu ya mauaji au unamaanisha hakuna wa kumsindikiza marehemu nyumbani Tanzania kwa sababu ya ukosefu wa Pasi?
ReplyDeletepole sana marehemu pamoja na familia ya haule huko songea wabongo tuliopo nje jamani tujitahidi sana kutembea kwa makundi tusipende sana kujiamini nyakati za usiku pia tuwe waoga kuanzisha ugomvi tukiwa wachache kingine tabia za ulevi nazo sio nzuri kama watu mkiwa wachache hasa kwenye sehemu za starehe kwasababu ubaguzi bado upo sana tu popote pale duniani watu tupo ulaya ila kwakweli tunahitajika sana kuishi kwa tahadhari sana!!!ama kweli tanzania ni kisima cha wapenda amani sababu sie hatunaga kabisa tabia za kibaguzi hapo nchini lakini tunapokuwa huku nje inauma sana mara utasikia mnigeria kachomwa kisu mara m Ivory coast kapigwa risasi na vyote hivyo vinafanywa na watu wasio julikana kwa serikali zao na mkiulizwa mnaambiwa utafanywa uchunguzi ambao matokeo yake huwa hatuambiwi!!hakuna ujanja tunatafuta maisha lakini cha moto tunakipata!mzee michuzi imeniuma sana hiyo isho na kitendo alichofanyiwa marehemu mbongo unapigwa risasi unakufa bado wanaona haitoshi wanamalizia na kisu!!!ubinadamu gani huu???mungu amlaze pema peponi marehemu!amen!
ReplyDeletePoleni sana ndugu wa marehemu.
ReplyDeleteSwali dogo, pasi za kusafiria za TZ zinatolewa ubalozini Brasilia? Ina maana wa-TZ walifika huko bila pasi? Au safari zilikuwa ni zile za 'ghafla' sana?
Mh lakini inawezekana mtu kuuliwa ki hivyo...Achapwe risasi tatu bado aongezewe na kisu juu!!!Kwani roho yake ilikuwa ngumu kama ya paka kutoka? Ni kisasi au?!!Yaelekea alikuwa na bifu na makomandoo huyo....Mh walimkusudia vibaya...Poleni sana jamani..Kila mmoja atarejea huko....Tumuombee Mungu amlaze maali pema peponi...
ReplyDeleteHaya nahisi mwashuhudia wazalendo..wale wasiopenda nchi yao ya amani na kwenda ughaibuni kuweka makazi mambo hayooo...Hebu tulieni nchini kwenu mujitahidi muiendeleze...Kutangatanga huku huku utafikiri huna kwenu mnafikiri hao wazungu wanawapenda sana? Wangekuwa wanawapenda wasinge watawala na kuwatesa kuwachapa bila huruma..Hawaja sahau hao mlivyo wanyang'anya nchi ya Tanzania...Hebu jitulizeni Tanzania Nchi ya amani, nchi ya upendo haibagui Mweupe wala mweusi..Mtaishia kuuliwa hivyo hivyo kama kuku.
ReplyDeleteHii inaonyesha dhahiri White people hata wafanye nini bado wanachuki na Waafrika kama jinsi ilivyo jionesha mwanzo mwa karne ya 19C walivyo tunyanyasa. Ila watanzania tumekuwa tukiwakumbatia kwa upendo woote, hatuwatofautishi tena kuwapa kipaumbele katika mambo yetu...Je Watanzania wangewafanyia hivi wangechukua hatua gani? Rais/Mabalozi wetu wanafikiri nini kuhusiana na matukio ya Watanzania kuuliwa kinyama katika nchi za Ughaibuni? Ni kwanini watanzania tukienda nchi za watu hatuthaminiwi kama ilivyo wao wakija nchi zetu...? WATANZANIA TUAMKE KUTETEA HAKI ZA WENZETU KWANI HATA WAO WAKO NCHINI KWETU NA WANAISHI KWA AMANI NA UPENDO KAMA ILIVYO SISI WAZAWA...
ReplyDeleteBrazil, ni nchi yenye mchanganyiko wa watu, wenye asili ya kiafrica, waliochukuliwa Africa kama watumwa, wenye asili ya indiana, na wenye asili ya european, na wenye asili ya mchanganyiko wa makundi yote hayo matatu, na hao wenye asili ya kiafrica na mchanganyiko ni hatari sana, na wana makazi yao, kiasi kwamba watu wanapewa tahadhali kutembelea huko, makazi yao ni kama ya uswazi, au kwa lugha nyingine uwanja wa fisi, fujo fujo, ualifu, umejaa tele.
ReplyDeletePoleni sana na msiba ndugu zetu wa Brazil.
ReplyDeleteWewe annoy uliotoa maoni wa Tarehe May 08, 2009 12:23 PM, una uhakika kama ameuwawa na wazungu au unafikiria tu kuwa nje ya Tanzania kuna wazungu? Brazil ni mchanganyiko wa watu kama alivyosema mdau hapo juu!!
Pole kwa wafiwa na Mungu amuhifadhi na kumsamehe makosa yake.
ReplyDeleteHivi wanaopost Humu wanafikiria nini haswa? kama huna cha kuandika sio lazima uandike upuuzi unaondika, kuna mtu kauliza kuwa walisafiri bila pasi, inaonyesha ni jinsi gani hujaelimika, tanzania ilibadilisha pasi za kusafiria miaka michache iliyopita, ukiwa nje ya nchi unaenda kubadilishia ubalozini, sasa hapo ndio kunaucheleweshwaji. halaf kuna Mpuuzi kaandika utumbo sijui watu wabaki nchi yao, We una akili timamu kweli?? kama hujawahi kusafiri ni wewe na umasikini wako wa fikra. Inaboa sana kuona nalazimika kuandika maneno haya chini ya Post ya msiba.
Michuzi usibanie wapate ujumbe.
tusiweke ubaguzi mbele mpaka tujue chanzo kilikuwa ni nini? na wliofanya uhalifu ni wa tabaka lipi? huwenda ni wabongo au waasia au waafrica au wabrazil weusi coz sometimes waafrica au wabongo huku huwa tunachapana wenyewe
ReplyDeletemay God rest his soul in peace.AMEN
Anonymous wa 12.23 pm huna point, taarifa ya mauaji haikusema kauawa na watu weupe au weusi, Kama alivyosema mmojawapo ya wachangiaji ni kwamba Brazil ni nchi ya watu mchanganyiko, hivyo kushutumu weupe kwamba ndiyo wauaji ni upotoshaji, inawezekana kuna sababu nyingine iliyopelekea mauaji, wabaguzi wapo kila mahali na kutoka kila rangi au kabila na si weupe pekee, je unakumbuka mauaji yaliyotokea South Africa hivi karibuni dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika yalifanywa na watu wa rangi gani?.
ReplyDeletePOLENI FAMILIA
ReplyDeletendugu zangu watanzania kwa mtu aliyewahi kumjuwa kijana huyu atawaeleza alikuwa pande la mtu hivyo wale waliofanya unyama ule walijuwa wazi endapo atapona mziki wake ni mkubwa ndiyo maana wameanza na risasi kumpunguza nguvu kisha kisu kwa uoga wao.
ReplyDeleteila ninachoweza kusema watanzania tupunguze ulevi na kuvuta mabangi, kwani ni hatari ktk maisha yetu
WATU HATA KAMA NI WABAGUZI JARIBUNI KUWAEPUKA SIO NYIE WAGENI MNATAKA MVUME KUZIDI WENYEJI UJANA USITUTAWALE, ONA SASA ALIKUWA KIUNGO MUHIMU KTK FAMILY YAKE SASA UNAWATESA WAZAZI NA NDUGU WALIOTEGEMEA MSAADA WAKO.
NINGEPENDA SISI WABONGO TUWE WASTAARABU UKIONYESHA UNYONGE KWA MWENYEJI HATOKUDHURU PIA MSIWANYANG'ANYE WANAWAKE ZAO KUWENI WAPOLE IMENIUMA SANA KWANI KIJANA NAMJUWA
POLENI SANA FAMILY YAKE
Jamani hapa marekani asilimia 75 ya watanzania niwahindi nawaarabu. Lilitokea kasheshe la passport hapa.wengiwnatokea tabora sheshe
ReplyDeleteMICHUZI, UMEANDIKA HII STORY VERY EASILY, SIDHANI KAMA UNAFIKISHA UJUMBE KWA WATU WALIOFIWA KWA KUWEKA MANENO KAMA ''AKAMMALIZIA KISU'' (hapa unaonyesha ushabiki)MANENO KAMA WATU WALIKUWA WANAANGALIA ''GEMU''(yaani una value muda wa tukio easily).
ReplyDeleteIF YOU WILL CONTINUE KEEP THIS KIND OF REPORT SIMPLE utaondoa maana inayojengeka katika blog yako ya umoja na Utanzania KATIKA MAAFA YANAYOWAPATA WENZETU,
HABARI KAMA HIZI ZITOE KWA HESHIMA NA LUGHA INAYOENDANA NA HABARI YENYEWE.
Poleni ndugu na jamaa wa marehemu. Mungu ampumzishe pema, amina.
ReplyDeleteTarehe May 08, 2009 11:59 AM, Mtoa Maoni: Anonymous huwezi kupima uzalendo wa Mbongo kwa kuondoka au kutoondoka nchini. Fisadi aliyebaki nchini ni mzalendo kuliko mpiga boksi wa ughaibuni? Si bora mpiga boksi walau ameachia nafasi ya ajira kwa aliyebakia nchini? Kila sehemu ina majanga yake. Bahati mbaya Mtanzania mwenzetu ameshambuliwa na kuuawa kwa risasi na kisu lakini kama angekuwepo Mbagala tunajuaje kwamba asingejeruhiwa na mabomu? Kama angekuwa anakatiza mtaa wa Swahili leo tunajuaje kama asingekumbana na risasi ya majambazi ya leo?
Isitoshe Wabrazil sio wazungu.
MICHUZI, UMEANDIKA HII STORY VERY EASILY, SIDHANI KAMA UNAFIKISHA UJUMBE KWA WATU WALIOFIWA KWA KUWEKA MANENO KAMA ''AKAMMALIZIA KISU'' (hapa unaonyesha ushabiki)MANENO KAMA WATU WALIKUWA WANAANGALIA ''GEMU''(yaani una value muda wa tukio easily).
ReplyDeleteNakubaliana na wewe, Michuzi apologize!
((Jamani hapa marekani asilimia 75 ya watanzania niwahindi nawaarabu. Lilitokea kasheshe la passport hapa.wengiwnatokea tabora sheshe))
ReplyDelete-> HUYU JAMANI ANAONGEA NINI?!! NISAIDIENI?!!
R.I.P. NDUGU YETU, POLENI SANA WANAFAMILIA.
Jamanieeeeeeeeee.....!! Kuuwawa ni bahati mbaya tu. Hiyo ni ajali iliyotokea .. lakini sio kuwa kauawa kwa kuwa yuko nje ya nchi yake jamani. Kuna sababu tu za kawaida za kijamii ambazo zinaweza kupelekea ukauawa hata ukiwa nchini mwako na hata ukiwa mtu yeyote. Kinachotakiwa ni kuzingatia mbinu za kuepukana na mazingira ya uhalifu yatakayopelekea aina yoyote ya madhara (hata ikiwa ni madogo kama kuibia pesa mfukoni)..na haijalishi uko wapi.. hata nyumbani kwenu, nchi kwenu, nyumbani kwako, maisha yako, maisha ya watoto wako, maisha ya ndugu zako, marafiki zako, usalama wa nchi yako, n.k. Hili ni jukumu la kila siku ktk maisha yetu hapa duniani kwa kila mtu.
ReplyDeleteHapa hapa Tanzania.. hapa hapa Dar, juzi usiku wa kuamkia jana kauawa kijana mmoja.. mwili wake umeokotwa baharini ufukweni umetupwa.. yuko uchi, kachomwachomwa kisu mwilini, kakatwa sehemu zake za siri na masikio.. Kijana huyu , MacDavid, hakuwa na makuu na mtu yeyote, kijana hakuwa hata na mwili wa ukatili na ubabe, kijana mwenye kisauti kidogo.. na alikuwa ni a very humble and popular guy. Kauawa nae kikatili tuu.. Na ni mtanzania. MUNGU AZIWEKE ROHO ZA HAWA VIJANA MAHALI PEMA PEPONI.
Michuzi naomba habari hii iwafikie watu wote wanaomfahamu kijana huyu pia.. Maafa hutokea kila mahali. Vijana tujihadhari zaidi katika safari ya maisha hapa duniani.
We mdau wa 12:23 usikimbilie fikra za weupe kubagua weusi - ukae ukijua kuwa Brazil ina watu weusi kuliko weupe na huna ushahidi kuwa waliomuua ni weupe. Chances are aliuawa na weusi...
ReplyDeletewadau nilipoangalia picha hii kwa haraka nilidhani ni mchezaji wa arsenal adebayo.
ReplyDeletepoleni wafiwa na wote
ReplyDeletejaman hii newz ni msiba ila...hahahaaaaaaa yan kuna annons akili zenu zina stress za kubeba box na kula vumbi kwa sana
annons:
aya wee unaesema "adebayo",wee unaesema 75% ya watanzania usa ni waarabu/wahindi mbona hueleweki ulitaka kusemaje?nyie eti kauwawa sio na weupe sasa ni waTz ndo walimuua??aya watu wakirudi bongo then inakuweje wee annon?
ila jaman aya matukio nje ni mengi sana afu yanaleta hasara sana na costs za kusafirisha mwili na family ya mhusika inaingia kombo mana mtu alikua msaada
asanteni
Mungu akulaze mahali pema.
ReplyDeleteNa muache kujihusisha kwenye uuzaji wa madawa ya kulevya, ona mtu unavyokuja kufa kifo kibaya.
It does not matter where you are going and where you are coming from,it matter when you are going to die and be burried that is alpha and omega people of God.Hatukuja kuota mizizi duniani wote tutarudi mavumbini even those people from a loyal family like Diana.
ReplyDelete