Mdau Amos Matali Cherehani akifurahia baada ya kubundila nondozzzz ya masters ya Business Administration katika chuo kikuu cha University of District of columbia sherehe ambazo zilifana sana mitaa ya Washignton DC Mdau Amos na prof wake baada ya kuvuta nondozzz lake
akiwa kama kiranja mdau amos aongoza wala nondozzz wenzie kuingia ukumbini



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Ngosha, haya wakati umefika wa ku-"Panda Hadi Darini" Naomba nikupe changamoto kuwa huu siyo wakati muafaka wa kurudi Bongo, malizia kabisa na hiyo PhD na ukiridi uje uwe mkuu wa chuo Changu hapa Peramiho. Kazi yako inakusubiri.
    Mhagama, Songea

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    Hongera Amos ila bado anambaduko uleule wa Mantale Sumve!!!! Msukuma ni msukuma hata kama yuko Dc

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    Congrats. Amos utarudi tena TTCL au ndo ntoleeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2009

    Amos hongera lakini hii shule itakuumiza sana hapa Marekani, labda uende Tanzania.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2009

    Kaka mithupu hembu nithaidie,
    hicho chuo kipo afilika nini??
    maana naona woooooote blak.
    But this is your time NGOSHAAAA))

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2009

    michuzi huwezi kusema chuo kikuu cha university ,please ulisoma shule gani bwana?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2009

    Maana ya UDC - university of dumb children na ukitoka hapo kazi za kutunza wazee zinakusubiri na nondo zako kibao.UDC ni noma tupuuu

    ReplyDelete
  8. Huyu jama alioandika eti UDC ni University of dumb children ni mpumbavu sana. Kama wewe uko hapa Washington-DC na hiki chuo unakijua umuhimu wake huwezi sema hivyo. Tatizo letu sisi WA-TZ tuna mambo bado ya kutaka kutoka chuo na kupata kazi saa hiyo hiyo, eti kwa elimu yetu ya Masters. Ndio maana tunashindwa kubadilika.
    Wanafunzi wenyewe wa-marekani wakati wanasoma chuo kikuu huwa wanafanya kazi za ajabu ajabu tu, na ndio maana at the end wakipata degree zao wanakuwa na akili ya misha na nini cha kufanya. Utawakuta hapa DC wanafyeka majani wakati wa spring na summer, wanaosha vyombo mahotelini, na wengi wao wanauza bar au restaurant hapa DC, usiku na asubuhi.Ni wachache sana ambao wanakuwa hawana kazi kabisa.
    sasa leo MTZ akifanya kazi ya kishenzi hapa MD au DC au Virginia maneno mengi mtaani. Mi naona huu ni wivu kwa waliosoma, amabo hauna msingi.
    Pia waliosoma nao hapa DC au MD waache dharau kwa wasiosoma maana wote ni WA-TZ na kila mtu anajua analaofanya ki-maisha.
    Ndugu yangu uliyeandika pumba hapo juu kuhusu dumb university ngoja nikupe data:
    Kama una degree hongera , na kama huna kwa sasa ila bado unasoma hongera pia, na kama huna degree, husomi na uko huku nje unafanya kazi hongera pia kwani ndo chaguo lako na kila mtu anaheshimu hilo.
    Elewa tu kwa hao wanaofanya hizo kazi unazosema za kubeba boksi au kuosha wazee DC au MD ni WA-TZ na WA-TZ wanaoishi marekani tu (pekee yao tu)yaani (USA) kwa data za kutuma fedha nyumbani TZ, mwaka jana pekee (2008) walituma USD 100,000,000.00 (dola za kimarekani millioni mia moja).
    Kwa ujumla unatakiwa kushukuru sana sana tena sana hao unaosema wanabeba maboksi hapa US, Maana wanazidi kuwatumia fedha angalau kiasi cha kufikia millioni mia moja dola za kimarekani, ndugu zao TZ.
    Huo ni mchango mkubwa sana tena sana katika uchumi wa TZ kwa kila mwaka. Sasa wewe ulitaka warudi TZ halafu walete mchango upi, ambao wewe unautaka hapo utakaoweza kuleta hizo fedha zote kila mwaka.
    Wakenya tu walio nje tena hapa USA tu na tena ndo wanaofanya hizo kazi unazosema zaidi ya waTZ na kwao wasomi wa kumwaga mpaka wanakuja TZ kutafuta kazi wanatuma 400 million USD kila mwaka. Wa-Nigreria 2008 walioko hapo USA peke yao tu walituma US-Dollar million 900. Na Wa-Mexico wanaongoza kwa hizo kazi unazozikandia wewe hapo USA, mwaka jana tu 2008 walituma USD billioni 3. Na kwa sasa ndio wanategemewa na nchi yao kama kii-ngizio cha kipato kikuu cha tatu kwa uchumi baada ya mafuta,na utalii au Viwanda
    Kwa taarifa waliomaliza hapa USA , wanajifunza shida, na wanajikamua katika shida kila siku inavyokucha na wengine weshaanza kula sukari walioisomea siku nyingi zilizopita.
    Kuna states hapa USA, WATZ karibu 3/4 wanaoishi hapo wana degree zao, pia kuna states watu wanapenda kufanya kazi na wote- at the end wanamalengo kwamba mafanikio yako njiani. Tusianze kudharauliana sasa eti UDC ni University of Dummb children. Maana tukianza hivyo tutaona mara msomi chuo kikuu Dar anamdharau msomi Tumaini, na mara Msomi MTZ wa Makerere atamdharua msomi wa UDSM, na mara msomi MTZ wa CapeTown University atamdharau wa Makerere na mara wa India atamdharau wa Cape , then wa China atamdharau msomi MTZ wa India, Then msomi MTZ wa Russia atamdharau msomi wa China, then Sweden atamdharau msomi Russia, then Msomi MTZ wa Canada atamdharau Msomi aliyesoma Sweden, then msmi MTZ ,UK atamdharau msomi wa Canada, na hapo ndipo Msomi MTZ wa US atamdharau msomi mwingine wa chuo kingine hapa USA, kama huo mjinga hpo juu then msmi MTZ aliyesoma UK na wasomi wengine popote duniani as far as hawakusoma US.
    wasomi tuache hizo na wasiosoma pia tuache hizo, wote ni WATZ na mafanikio ya aliye nje au aliye ndani awe amesoma au la , kama haku-fisadi basi Hongera kwake mara elfu mbili.
    Naomba uache dharau kwa walio nje, wewe endeleza mambo yako hapo ulipo na shukuru kila kitu kinakwenda.Ninaona wewe unataka tu kuwasifia hao wezi wachache hapo TZ wanaoua sifa za wasomi wengi wasiotaka kuiba.
    Pia elewa kurudi TZ ni hiyari ya ntu akiona anachokihitaji hajakipata huku DC au MD. Alifuata Elimu alipotoka TZ na dio hiyo amepta tu hapo UDC. Kama ilimchukua miaka sita kuja hapa na kusoma hadi kupata Masters yake sawa, hilo la kazi ni mtihani mwingine nalo pialinahitaji kujiweka sawa, tena ngangari kweli.
    Hongera Amos, endeleza kuruka hapa Potomac River na ogelea ukitaka maana kazi ilikuwa kubwa hiyo.
    UDC oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2009

    Sasa hiyo picha akiwa na fimbo pamoja na mavazi ya black,red,gold and green anaonekana kama yule Mjamaica muimbaji mashuhuri anyeitwa " Luciano".Yaani copy-right!

    ReplyDelete
  10. Kichwa Kigumu-DCMay 12, 2009

    Angalia kurasa zaidi ya 200 za jarida, taarifa,au data za kutoka "World Bank's Migrations and Remittances Factbook 2008".Soma zaidi upande wa remittance kwa uelwa wa fedha kiasi gani zinatumwa au unaweza pia tembelea tovuti(website) yao ukiandika maneno hayo hapo juu("World Bank's Migrations and Remittances Factbook 2008".)
    uone manufaa yanoyeletwa na watu walio nje ya nchi zao na wanaofanya kazi za kiajabu-ajabu, halafu oanisha maneno ya kusema eti walio nje au wanaosoma au kufanya kazi nje ni washenzi tu.Na hasa wewe uliyeandika eti UDC is the university of Dumb Children. "Think outside the box and look from the big picture stand-point".

    MEXICANS- 2008
    The remittances from Mexican citizens working in the United States account for only 0.2% of Mexico's GDP[96] which was equal to US$20 billion dollars per year in 2004 and is the seventh largest source of foreign income after oil, industrial exports, manufactured good, electronics, automobiles and food exports.[97] According to Mexico's central bank, remittances fell 3.6% in 2008between $25bn and $ 30bn .

    KENYANS-2008
    Remittances are Kenya’s single largest source of foreign exchange. Remittances rose from U.S. $338.3 million in 2004 to U.S. $1.3 billion in 2007, equivalent to 5.3% of the GDP, but there was a significant decrease in 2008. Remmitance from Kenyans living in USA,alone in 2008 decline from U.S. $752.1million to U.S. $ 428.2 million.

    UGANDANS-2008
    Uganda is among those countries who benefit a lot from her citizens working abroad as the country receives $900 million per annum in form of private capital inflows and they are projected to rise to $1.2 billion.

    Tunataka Wa-TZ wengi wawe nje ili waweze fikia uwezo wa wenzetu kwa kutuma fedha na faida ikaonekana na sio kusema mambo kama sio msomi.
    Pia angalia ni kwa nini watu wengi duniani wanakuja US na sio kwingine duniani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2009

    kinee wawejha looolo, walahi siku ya PHD wazungu watakutia pingu wakidhani umepatwa kichaa kumbe mizuka ya niiimbe hata mzee wetu mmoja mashuhuri sana Dar ilimpata hii Kilimanjaro htl akaenda kuimbia chooni.Hongera ndugu yangu umefurahi na unastahili furaha, kindumbwendumbwe cha dissertation na courseworks si mchezo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2009

    He he he he he Strayer University, Montgomery College ,University of District of Columbia ..hehehehe wale wale tu ...... Hongera lakini , maana ume smile kinoma, ukitoka hapo wape Hi kule Fresh Fields Supermarket (Hivi bado zipo) , kwa wabongo walio bobea kubeba box.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2009

    wewew anony wa trh 12/5/2009 saa 8:52 umejitahidi kuelezea kwa upana ila umesahau jambo moja na hatimaye ukajikuta unacho ki-reflect hapo ni dharau ya kimtindo sio direct ila inderect kuonyesha kuwa mtu aliyesoma US basi anahaki ya kujisikia ana quality education kuliko sehemu nyingine zone.
    kumbuka kwamba nchi kuwa na uchumi mkubwa haimaanishi pia kwamba vyuo vyake vyote vinatoa elimu iliyo ktk standard ya juu. hivyo kama ulikusudia kueleza habari ya wasomi kudharauliana bora hata ungetumia mfano wa concrete universities zinazo tambulika kuwa super giants ktk elimu fulani duniani ndipo uzilinganishe na nyingine bila kujali ni za nchi gani.maana hata UNESCO inapo pima ubora wa elimu inazingatia vigezo vyake.
    swala la kusema wa uganda amdharau wa tz,wa south africa amdharau wa uganda,wa india amdharau wa south africa,wachina amdharau wa india etc kwa ufupi umecreate wewe kwa kufuata sifa za mataifa hayo kiuchumi n.k ila unashindwa kutambua kwamba kunavyuo viko africa na vinatoa elimu bora kuliko hata baadhi ya vyuo vya hapo US AMBAVYO HATA NDANI YA US pia havitambuki.
    safari nyingine ukiandika vitu fikiri sana usije ukatia pumba ktk mchele wako mzuri.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2009

    As long as baba yako ni fisadi unaweza kwenda kusoma hata Harvard. Lakini kama ni kwa mwendo wa kujisomesha kwa maana ya kufanya kazi huku unajilipia, na ukiwa mtoto wa mkulima kutoka TZ vyuo kama community colleges vinaweza kuwa poa kabisa. So wewe uliyekandia UDC inaonekana ndio wale wale watoto wa baba fisadi ambao hamjui shida ni nini.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2009

    Mdau aliyechangia kuwa wote ni WaTZ nadhani yupo sahihi kabisa. Lakini nadhani mdau mwingine aliyechangia juu ya chuo hiko ni kweli, chuo hicho kipo chini sana. Let us face it, kuna vyuo hapa Marekani kama utamaliza kupata kazi ni rahisi sana. Kwa Washington DC and MD vyuo hivyo ni kama Maryland University, Georgetown University, Howard University, Catholic University, American University na vingine....kumbe hivyi ni vyuo ambavyo vina rank ya juu sana. Lakini naungana na mdau aliyesema kuwa tuache kudharauliana juu ya Elimu na kazi ambazo watu wanafanya, at the end sisi wote in Watanzania

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2009

    wewe mlupalupa unayejitahidi kutetea baadhi ya vyuo vya US usifanye watu wajinga ukidhani kuwa kwakuwa ukipata degree USA basi tayari unaweza kuwa mkali kishule kuliko wa UK,RUSSIA,SWIDEN,CANADA,CHINA n.k
    tambua kwamba ubora wa elimu unategemea wataalam wanaoitoa,vifaa/nyenzo zinazohitajika kuitoa hiyo elimu,na namna inayotumika kufuatilia uelewa wa msomaji ktk nadharia na vitendo kuhakikisha kuwa amiva na sio mbabaishaji.
    unaiweka nchi mfano sweden kwamba kiwango chake kwa mtizamo wako kikochini ya cha USA,lakini nakupa mfano mzuri tu angalia karolinska medical university ya sweden unaweza kuilinganisha na baadhi ya vyuo vya hapo US? au baadhi ya vyuo vya russia unaweza kuvilinganisha na vya huko US? hapo umechemka sana tu,kwa taarifa yako kuna wavyuo wengi tu wa USA tena wazawa waUSA sio wewe wa kwenda wako huku nchi za watu tunachimbuka nao,ni kwasababu wanajua kwamba vyuo vyenye kiwango cha elimu kinacholingana na kinachotolewa ktk nchi kama hizi wanazokuja kusoma kwa USA hawawezi kumudu gharama zake,ila ktk nchi hizi wanapata kiwango cha juu kinahitajika na kwa gharama wanazoweza kulipa. kama wewe pia ungeweza kulipia na sio kulipia tu bali na entry qualification pia inamata ukizingatia compatition inayokuwepo kuingia,mfano california medical university,yale medical university jaribu hapo hata kama wewe ni mzaliwa wa USA na pesa unayo lakini uone mdundo wake!au jaribu cambridge ya UK,au Moscow medical academy 1&2 au st.petersburg pavlov medical university vya russia,au karoliska medical university ya sweden uone kama utanusa mlango kirahisi hata kama unapesa yako mkononi,na hata ukiingia pia mlango wa kutoka ukowazi 24hrs kutemwa out kama kitabu hakiendi ipasavyo,mbona huko wamejaa wamarekani,wakanada,waswis si nikwasababu wanajuwa wanachokipata nisawa na kinachohitajika kwao?
    andika vitu vya maana,kama unasoma ktk chuo kikuu hakikisha kinakupa elimu inayokubalika ktk kiwango kinachostahili kukusaidia wewe na wale unaowapa huduma kwa kutumia elimu yako. sio unapata gamba tu kisha ukiingizwa mzigoni unaanza kujinyeanyea huku maneno kibao vitendo kidogo na gamba unalo mkononi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 14, 2009

    Kwa taarifa yako ukisoma chuo chochote nje ya USA ukija hapa wala kazi hupati maanake vyuo vya nchi nyingine hawavitambui. Wenyewe wanaelewa tu vyuo vyao na kuona kila kitu chao ndio bora.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 14, 2009

    mdau unaesema ukisoma chuo kingine nje ya USA huwezi kupata kazi USA angalia pia ni field gani unazungumzia,mimi kuna watu nawafahamu wamemaliza hapa ninaposoma na wengine ni ma-director ktk vitengo fulani hapo USA, na kwa bahati nzuri imefanyinya international symposium na wame attend pia hapa officially kama wawakilishi. na istitoshe hadi hivi sasa nasoma baadhi ya wamarekani hapa na swali unalozungumzia wewe nimewauliza pia,lakini kinacho eleweka ni kwamba vyuo kuna vinavyo tambulika na visivyotambulika,kwa vinavyo tambulika kinachohitajika ni kutoa mitihani yao ya bodi zao,sasa hili ni jambo la kawaida ktk nchi nyingi,maana hata hapa ukimaliza USA ukija lazima pia upigwe paper ya kukuthibitisha kuwa hujabumba cheti na mambo unayaweza sio kuegesha egesha tu kwa ajili ya mitihani.au unadhani ukitoka USA ikifika nchi yeyote basi kazi unapa tu kirahisi?sio kweli hata kidogo kila nchi inalinda kwanza maslahi ya vyuo vyake,ila inahitaji wataalam wenye uwezo wa juu kikazi toka mahali popote duniani ilimradi wao hawana mtaalam anayeweza kuichukua nafasi hiyo kwa wakati huo.
    kuna wakorea,warusi,wajerumani,wachina n.k wamesoma nchini kwao na wanapiga mzigo USA kama kawaida ilimradi tu wamekidhi viwango vinavyohitajika ktk field hiyo,na wana onyesha ubora wa hali ya juu hata kuliko wamarekani wenyewe.wanaosota ni waliosoma ktk vyuo vinavyotia mashaka,hata mitihani pia wakiisikia jasho linawatoka,sio kwa sababu ya gharama bali kwa sababu wa shule za kuchovya.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 14, 2009

    wewe mdau wa dc na kichwakigumu mbona hamna point!!! ni kujitetea tu mwanzo hadi mwisho. hicho chuo kiko chini!!!
    halafu wewe muhitimu mbona una kitambi sana???
    ulikuwa unasoma kweli wewe???? au ulikuwa ukiuza mchana kwenye migahawa yenye burgers, KFC na kujipigilia makuku, alafu usiku ukiuza baa na kujipigilia budlights na cools kimtindo???
    nhee bhagosha umependezaga kwakweli.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 15, 2009

    Mimi nimesoma Strayer University, Na nakula Sukari yangu sasa. TENA SIO SUKARI GURU.

    Shule ni shule , cha muhimu je unaweza kuproduce ? . Wabongo mnapenda sana kuangalia madigirii Masters, PHD, PHZ ,PHDZ.

    Wenzetu hawaangalii hayo, kwanza PHD ni kwa walimu au researchers , be careful.

    Kazi ni kazi bwana cha muhimu ni kwamba kuwa na elimu kwanza kabisa ni personal achievement kwa hiyo haters swallow it.

    Kwa kweli kuna nchi ukisoma basi hakuna atakae kusumbua . katika nchi hizo ya kwanza ni USA.
    Nionyeshe mtu yeyote awe daktari, engineer , muhasibu ambaye alisoma USA na kwenda Tanzanzania akaambiawa lazima arudishule ili aweze kupewa kazi.

    Lakini KILA MTU AKITOKA NCHI YEYOTE kwenda Marekani nilazima arudi shule kama anataka kutumia elimu yake. TUACHE UBISHI.

    Kama unamifano tupe sitaki namjua jamaa fulani.
    Muacheni Amosi he deserves it, mwenzetu kajitahidi jamani hata haibu hamna?


    Nimekuwekea wewe mswiden (May 13, 2009 10:58 PM), , Ulisema chuo chako kinatwaje eti ? karolinska medical university ? Hebu kitafute hapa (hii ina nchi tofauti na fields tofauti)

    Nakubaliana na wengi kwamba USA si nchi ya kwanza kielimu. Lakini Wasomi wake ni wa kwanza kukubalika ulimwenguni kote.

    World's Best Colleges and Universities: Top 200- (2008)
    http://www.usnews.com/articles/education/worlds-best-colleges/2008/11/20/worlds-best-colleges-and-universities-top-200.html

    Siku hizi Bongo naona watu wengine wanaamua kuongopa , eti wamesoma USA halafu wanapewa udirector? Yaani hata hawaangali documents basi .

    Cha muhimu hata kama huna elimu ijuwe field yako vizuri.

    You get paid for what you produce and not for how many degrees you have.

    Ndio maana Wazungu na Waasia wanatushinda.

    Wenu
    Mzee wa Ununio

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...