Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa akikata utepe kuashiria uzinduzi maalumu wa maabara ya kisasa iliyojengwa na Abbott Fund kwa msaada wa wananchi wa Marekani,(kulia)Makamu wa Rais wa Abbott Fund Chrity Wistar,(kushoto) Mganga Mkuu wa Hospital ya Amana Willy Sangu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk. Willy Sangu akimpokea Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa,kuja kuzindua rasmi maabara ya kisasa iliyojengwa na Abbott Fund kwa msaada wa wananchi wa Marekani.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa (kushoto)akisaini kitabu cha wageni wakati wa uzinduzi wa maabara ya kisasa Amana Hospital iliyojengwa na Mfuko wa Abbott Fund,(katikati) Makamu wa Rais wa Abbott Fund Christy Wistar,(kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Prof Dafrosa Limo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa,akizungumzia jambo ndani ya maabara ya kisasa mara baada ya kuzindua rasmi Amana Hospital iliyojengwa na Mfuko wa Abbott Fund kwa msaada wa wananchi wa Marekani,Kulia kwake ni Meneja wa maabara Costantine Mzava,Kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Hospital ya Amana Willy Sangu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa,(kulia)Akipatiwa maelezo na Makamu wa Rais wa Abbott Fund Christy Wistar juu ya namna ya vifaa vya maabara ya kisasa vitakavyotumika mara baada ya kuizindua rasmi,(katikati) Meneja wa maabara Costantine Mzava,Kushoto kwake ni Mbunge wa Ilala Musa Azani Zungu,Maabara hiyo ilijengwa na Abbott Fund kwa msaada wa watu wa Marekani





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Hiyo ni asante George Bush.

    Makamamnda wa FBI na CIA walikuwa wametanda juu ya paa siku hiyo wakati Mkuu George Bush anatalii ndani. Naona kaona wagonjwa wanateseka sana akaagiza wasaidiwe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    Sasa muweke camera humo kibao au la tutasikia vifaa vimeingia mtini kama kawaida.Mwe Tanzania nchi yangu nakulilia wapi unaenda? kwa kweli "TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO SAFI"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    afadhali,soi kila siku wawekezaji kwenye mali asili tu,madini etc. lol afya na elimu ndo muhimu. Natumaini wengine wataiga mfano.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2009

    walahi vile vikiibiwa tena kama kawaida yenu, nitaomba search warrant natinga kwa mkuu wa maabara na staff wake wote na safari hii mkirudishia vingine bila uwajibishwaji kama mlivyofanya ocean road Mwakyu utaenda kulima mahindi. we have to be serious n mature

    ReplyDelete
  5. Al MusomaMay 13, 2009

    Abbott Fund. Miaka mingi nyuma, ningefikiri mwandishi wa ile volume ya Physics tuliyosoma mwaka 47 ambayo rafiki yetu Sabas alikuwa kai-hifadhi ukuirasa kwa ukurasa...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2009

    MAABARA HIYO HAITALETA MABADILIKO YOYOTE YALE, MALALAMIKO YA WAGONJWA YATABAKI PALEPALE, VISINGIZIO VYA MASHINE KUHARIBIKA VITAKUWEPO PALEPALE NA WIZI WA VIFAA HAUTACHUKUA MUDA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    mbona kule hamji?????

    sawasawa na masharti mengine yalofata baada ya ilo

    wafadhili oyeeeeee

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    Duh Tanzania sivyo niijuavyo.... Tanzania newz siku hizi fasta...yani zimeshatoka katika blog!!! Kaka michuzi hongera.............

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...