Dk. Joyce NdalichakoBaraza la Mitihani Tanzania (Necta)

SEMINARI zimeendelea kuongoza katika matokeo ya kidato cha sita ingawa ufaulu umeongezeka kwa ujumla wake.

Pamoja na ukweli huyo ukweli mingine ni kuwa shule za vipaji maalum nazo zimefanya vizuri sana na kuendelea kuonyesha umuhimu wa shule hizo kuendelea kuwapo.

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) ambalo limetangaza matokeo leo limesema kwamba kiwango cha ufaulu kwa wasichana kimeongezeka ikilinganishwa na wavulana huku katika wanafunzi 10 bora kitaifa, akijitokeza msichana pekee, Sophia Nahoza kutoka Sekondari ya Wasichana ya Marian iliyopo mkoani Pwani.

Hata hivyo pamoja na matokeo ya kuridhisha Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 25, wakiwamo wanane wa shule na 17 wa kujitegemea kwa kufanya udanganyifu katika mtihani huo.

Dk. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa Necta, aliwaambia waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam kuwa jumla ya watahiniwa 53, 758 walisajiliwa kufanya mtihani mwaka huu na kati yao 51,563 walifanya na 45,716 sawa na asilimia 89.64 wamefaulu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2009

    KWA KIWANGO KIKUBWA MATOKEO YA MITIHANI YA ELIMU YA JUU TZ HUNILETEA BINAFSI MAJONZI TU WALA SI CHENGINE.
    NA HILO LINATOKANA NA UKWELI KUWA PAMOJA NA TAIFA LETU CHANGA KUTOA MELFU YA WASOMI KILA MWAKA, BADO AJIRA INAENDELEA KUPOROMOKA, NASI HIVO TU, BALI SERIKALI KUU HAIJAWA NA PLANI YA KUWAANDALIA MAISHA WASOMI WANAOMALIZA MASOMO.
    MATOKEO YAKE, KWANGU MIMI MATANGAZO YA MATOKEO YA MTIHANI NI RUNGU NYINGINE KWA JAMII, KWANI KUNDI JENGINE LA WAZURURAJI NA WEZEMBE LIKO TAYARI KUVAMIA MITAA NA SI YA VIJIJINI, BALI YA MAKAO MAKUU YA MKOA WA PWANI WA ZAMANI, YAANI DAR.
    HIVI NI KWELI SERIKALI NA VIONGOZI WAKE WANASHINDWA KUWAANDALIA VIJANA HAWA MAISHA YA BAADAE? SIAMINI.
    NILIFIKA NYUMBANI HIVI KARIBUNI, SAFARI MOJA TU NILIYOIFANYA BAINA YA DAR-MOSHI NIMESHAWISHIKA TUNAZO RASILMALI ZA KUTOSHA KUTUFANYE TUTAMBE SI TU NDANI YA AFRIKA, BALI HATA ULIMWENGINI.LAKINI JE, TUNAO VIONGOZI WANAOJALI MASLAHI YA WENGI? MAENEO MENGI MNO YAPO KUWEZA KUINUA KIPATO CHA WANANCHI WENGI, MIONGONI MWAO WASOMI.
    LAKINI TAIFA LIMETAWALIWA NA UMIMI, NA VIONGOZI WAMEPOTEZA MWELEKEO.
    NI MSIBA KUWA UCHUMI TULIONAO TUNAENDELEA TU KUUKALIA.
    SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA ILISHINDWA KUMWENDELEZA MTANZANIA KISAYANSI KUTOKANA NA KUPONDA PATO DOGO TULILOPATA KWA KUENDEKEZA UKOMBOZI WA AFRIKA KWA KUPELEKA MISAADA YOTE NAMIBIA, AFRIKA KUSINI, ANGOLA, MSUMBIJI, SASA HIVI WOTE HAO WAKO HURU, IWEJE TUENDELEE TU KUSHINDWA KUYABADILISHA MAISHA YA KIJANA WA KITANZANIA?
    FEDHA ZA NCHI ZINAPOTELEA WAPI?
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2009

    Habari kaka michuzi,

    Nina mdogo wangu, alimaliza na combination ya HKL lakini cha kusikitisha katolewa matokeo ya HGE na amepasi. Naona hii inadhihirisha kuwa kuna matatizo mazito pale kwenye baraza la mitihani ukiunganisha na miskendo ya kuvuja mitihani ndo nabaki hoi kabisa.... manyangumi mpaka huku jamani tutafika kweli ...ngoja ntafute visa nikajilipue ulaya tuu

    KK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...