Muhula wa Pili wa WaPi Zanzibar umewadia....
WaPi ni tamasha la sanaa linalofanyika kila mwezi. Tukio hili linakusudia kutoa nafasi kwa wasanii wanaochipukia kushiriki na kuthibitisha vipaji vyao.
Katika Muhula huu tunakusudia kuanza kulipeleka tuko hili katika baadhi ya shule ili kuchochea ushiriki wa wanafunzi zaidi katika mijadala na sanaa.
Tunatarajia pia kushirikiana na baadhi ya taasisi mbalimbali ili kutoa nafasi za kujiendeleza kitaaluma na kisanii kwa wale watakaoonyesha juhudi na mwelekeo mzuri.
Tukio jingine jipya katika muhula huu ambalo litawezeshwa kama kawaida na BRITISH COUNCIL ni ubunifu na usanifu mitindo.
Mada ya safari hii katika WaPi ni USHIRIKINA...maafa kwa Maalbino... Tunatarajia kushirikisha wadau mbalimbali katika kujadili namna Ushirikina ulivyochangia katika ongezeko la maovu na pia kuangalia kama una manufaa au la.
PROGRAMU ITASHIRIKISHA:
Waongozaji wa tukio kutoka WaPi Zanzibar
DJ Cool Para
Jukwaa la sanaa za Mikono
Matona kutoka DCMA atatoa ufafanuzi wa awali juu ya nadharia ya muziki wa Mwambao kwenye Kona ya MAARIFA
JAMBO CABARET katika uchezaji na sarakasi
Mjadala wa mada
USHINDANI WA MAEMSII
Mtaalamu wa kupiga Qanun Nasor atakuwepo pia
Ngoma asilia
Shindano la vichekesho
PAMOJA NA SIZA MAZONGELA WA SEGERE
Mengineyo ni pamoja na Tenzi, Upambaji, Uchezaji na upigaji wa ala mbalimbali...
MAHALI NI NGOME KONGWE
Jumapili tarehe 03-05-2009 kuanzia saa 9 alasiri hadi 2 usiku
Hamna kiingilio
Zafara...you guys are doing such a good work...well done all the people involved. It's been long time coming...
ReplyDelete