Ali Kiba
Mdosi na Dmk Global inakukaribisha Zanzibar at the water front jumamosi june 13 upate marashi ya bongo flava kutoka kwa Ali Kiba akishirikiana na madj waliobobea Afrika mashariki ndani ya kapitali,Washington,Dc Dj Banti na The mix oldskool master dj Luke.

Fika uburudike,upate raha,utikise kichwa,rusha mikono na kujiachia achia ili mradi si fujo wala patashika bali ni jazba la burudani litakalo kuacha hoi. itakua mshike mshike nguo chanika, Ali Kiba na Cinderella, Mac Muga na nyingine nyingi na ukipoa sana ni magwiji wa kuzungusha chapati Afrika Djs Banti na Luke watakupa dozi za oldskool,genge,bongo flava kwa zamu address ya Zanzibar ni:
700 water st. Sw,
Washington DC

KARIBUNI
------------------------------------
ANGALIZO:
Wadau kunradhi. Globu ya jamii inapenda kuwatoa shaka wadau wa Washington DC kwamba ile ilani ya kusitisha matangazo ya kutoka jiji hilo linahusu shughuli za jumuiya ya/za wabongo huko na si watu binafsi - kwa mfano shoo zinazojitegemea kama hii ya Ali Kiba.
Matangazo ya wadau wa Washington DC ya aina yoyote yataendelea kama kawaida mradi yasitoke kwenye upande wowote katika uongozi wa jumuiya hadi hapo mambo yatapokuwa mswano. Hatua hii inatokana na kuwepo kwa kile kinachoitwa pande mbili katika uongozi wa jumuiya hiyo ambapo Globu ya Jamii inaendelea kuwa nyutro huku ikiwasihi wamalize tofauti zao kuruhusu libeneke liendelee kama zamanai.
Matangazo ya watu binafsi na vikundi huru ruksa!
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    TutaKUWEPO TUNamsubiri kwa hamu huyo gwiji wa Bongo Flava,safari hii Dc mmejitahidi kwa kupata ukumbi wenye hadhi ya juu hapa Dc na marekani kiujumla.
    Kamau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    ein Kiba bitte!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2009

    Hahahaa LOL, wewe uliyeongea kijerumani umenichekesha sana.
    Kiba ni kinywaji kinachochanganywa na cherry na ndizi.
    Ni kitamu hata hivyo
    Natamani kuja tena Ujerumani.

    Jamani watu wa Hamburg miss germany africa ametoka nchi gani?
    Kwani niliona picha ya mbongo mmoja kwenye hilo shindano.
    huyo naona kwenye top ten atakuwepo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2009

    mh mtoto anakula shushu uyu mwe kazana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...