
Picha na mdau Sasja Schulting
Hotuba ya Balozi wa Uingereza nchini Mh Diane Corner Aliyoitoa siku ya kilele cha Kumbukumbu ya Kuzaliwa Malkia Elizabeth II jijini Dar.
Waheshimiwa Mawaziri,
Wana Balozi Wenzangu,
Wageni Waalikwa
Ndugu Mabibi na Mabwana.
Napenda kuanza kwa kuwakaribisha wote, natambua baadhi yenu ni marafiki wa zamani wa nyumba hii namba 1 Kenyatta Drive na baadhi yeni ndiyo mara yenu ya kwanza kufika hapa nyumbani kwangu.
Kama wengi wenu mnavyofahamu, niliwasili Tanzania mwezi February mwaka huu, hivyo ndio kwanza nimemaliza siku 100 kama Balozi wa Uingereza nchini Tanzania. Ujio wangu nchini, umeanza vizuri kwa mapokezi mazuri na pongezi toka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kitu ambacho sio cha kawaida kupata pongezi siku ya kuwasilisha hati za utambulisho na mambo yameendelea kwenda vizuri tangu mwanzo.
Sijakosa mambo mengi ya kufanya, japo nimeshafanya kazi kwenye nchi mbalimbali likini hii ni mara ya kwanza kufanya kazi kwenye nchi ambayo ina uhusiano muhimu wa kihistoria na Uingereza ambapo Uingereza inajishughulisha kwa nguvu kubwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalan, misaada inayotolewa na serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Misaada ya Maendeleo, DFID, ni uthibitisho jinsi Uingereza ilivyodhamiria kwa dhati kusaidia maendeleo ya Tanzania. Katika miaka 5 iliyopita, serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la DFID, limetoa Pauni Milioni 500 za Uingereza ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni 1 kuchangia bajeti ya Tanzania katika juhudi zake za kupunguza umasikini.
Mchango huu, umesaidia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kwa Watanzania na kupunguza kasi ya vifo kwa watoto wachanga kushuka kwa asilimia 40% ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita.Kwa mwaka huu, Uingereza ndiye mchangiaji mkuu kwenye fungu la nchi wahisani kuchangia bajeti ya taifa kwa asilimia 15% ukilinganisha na mwaka jana.
Mchango huu ni sehemu za utekelezaji wa ahadi zake kwa bara la Afrika kuwa itazidisha mara dufu misaada yake kwa Afrika. Ni Uingereza tena ndio imetoa fungu kubwa kwatika mradi wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, unaosimamamiwa na UNDP.
Tukija upande wa ushirikiano wa kibiashara, Waziri wa Fedha,Mustafa Mkulo, katika hotuba yake ya bajeti wiki iliyopita, amesema kuna makampuni mengi ya Uingereza yanayokuja kuwekeza Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote. Hii inatokana na kazi nzuri inayofanywa na UKTI ambacho ni kitengo cha biashara,cha Ubalozi wa Uingereza.
Ila kwa mujibu wa wafanya biashara,Tanzania bado ni nchi yenye mazingira magumu kufanya biashara.
Na hapa pia serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la DFID, inaisaidia serikali ya Tanzania, kujenga uwezo kuhakikisha sekta binafsi inakuwa na kustawi. Tunaamini kwa dhati, njia pekee kwa Tanzania kufikia maendeleo endelevu yatakayoiondoa toka kwenye lindi la umasikini, ni kuendeleza sekta binafsi.
Nayo British Council inaendelea kutoa huduma mahisusi za kitaalamu za programu za kimaendeleo na za kijamii na kiutamaduni kwa lengo la kuongeza ufahamu wa Uingereza kwa Watanzania na kuibua hamasa ya mtazamo na mawazo mapya kwa Watanzania kuchangamkia fursa kwa watanzania kujichanganya na wenzao dunioni kote.
British Council ni kiungo muhimu katika ujenzi wa ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za Uingereza na zile za Tanzania kwa lengo la kukuza mashirikiano ya karibu.
Na hapa ubalozini, tunashirikiana na serikali ya Tanzania. Katika mambo mbalimbali, kuanzia masuala ya haki miliki, uhifadhi wa mazingira, mafunzo kwa jeshi la polisi na vifaa vya kijeshi kwa vikosi vya kulinda amani Darfur.
Mwaka jana, Tulidhamini Watanzania 8 katika skolaship za Programu ya Chevening. Tunatoa viza kwa Watanzania wanaosafiri kwenda Uingereza na kuhudumia Waingereza zaidi ya 7,000 wanaoishi Tanzania.
Ubalozi wa Uingereza kwa kushirikiana na DFID, unafanyakazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na Mashirika yake hapa nchini. Mpango wa UN- Moja, ni kipimo muhimu kitakachotumika kama modeli ya mafanikio kwa nchi nyingine. Chini ya Umoja wa Mataifa.
Pia tunashirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuboresha jumuiya za kiuchumi na masuala ya uhamiaji bila kusahau tunafanya kazi kwa pamoja na wenzetu wa nchi za Jumuiya ya Ulaya katika kipengele Namba 8 kihusucho madadiliano ya kisiasa na Tanzania.
Kwa kifupi, Uingereza inahusika sana Tanzania, ili kufahamu zaidi, nawashauri, kabla ya kuondoka mahali hapa, hakikisha unajipatia machapisho, majarida na vipeperushi kuhusu Uingereza na Tanzania .
Lakini, kitu hasa ninacholenga leo sio mahusiano ya serikali na serikali ila mahusiano kati ya watu na watu wa pande hizi mbili.
Kabla sijaja Tanzania, Umoja wa watanzania waishio nchini Uingereza waliandaa sherehe ya pomoja kwa ajili yangu na balozi aliekuwepo Philip Parham.Waalikwa walikuwa wengi sana karibia watu mia tatu kutoka sehemu mbalimbali za London, mojawapo ya waalikwa waliokuwepo ni pamoja na mke wa waziri mkuu wa Uingereza Sarah Brown, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dr Mwanaidi Maajar, waliowahi kuwa mawaziri katika balaza la mawairi lililopita bila kusahau watanzania wanaosoma na kufanya kazi nchini Uingereza.
Pamoja na watu kutoka sehemu mbalimbali, alikuwepo pia mtu aliekuwa ametoka mji wa mbali sana na Uingereza Glaslow kuja tu kuhudhuria sherehe hiyo.Bila kusahau pia waingereza wafanyao kazi kazi nchini Tanzania na wale ambao waliwahi kufanya kazi hapa either serikalini, kwanye ngo's na kwenye sekta binafsi.
Kati ya waliokuwepo pia alikuwepo mwanamke mmoja ambae binti yake alikuja kutembelea Tanzania na alipofika akaipenda sana nchi ya Tanzania na watu wake..na akaamua kuja Kuishi Tanzania pamoja na kufanya kazi hapa na sasa amefungua NGO yake hapa Tanzania.
Miezi minne niliyoishi hapa Tanzania, imenidhihirishia uelewa wangu wa mahusiano kati ya watu wa nchi hizi mbili.
Kama ukiangalia Serikali na Serikali unaweza kushawishika kuona mahusiano haya si sawa sababu Uingereza ni mwanachama waG8 na ni mojawapo ya nchi tajiri sana duniani wakati Tanzania ni mojawapo ya chi maskini sana duniani.Na katika nyanja nyingi nchi hizi mbili ziko tofauti sana, kiuchumi,kitamaduni,kimaendeleo na hata hali ya hewa.
Ila nafikiri mahusiano haya yamefika mbali zaidi kuliko mtu anavyoweza kufikiria.Hii ni kutokana na tofauti zetu zilizopo ndizo zinazofanya kila nchi ijifunze kutoka kwa mwenzake na hii inatufanya tuweze kusaidiana kimaisha na kimaendeleo pia.
Nimeguswa na uwepo na uwepo wenu hapa na nafurahi sana kuona tukiwa tumejaa kwenye hii bustani tukifurahi kwa pamoja na hii ni kutokana na mahusiano mazuri ya nchi hizi mbili ambapo Uingereza inasaidia Tanzania na kutokana na kusaidia huko Uingereza inaridhishwa na kuona mabadiliko ya maisha ya watanzania kwa uzuri zaidi. Ni ujuzi wa mabadiliko ya maisha kwa pande zote mbili.
Kitu kinachofanania ni uhuru wa mabunge yetu.Tanzania mwaka huu mwezi wa tisa au mwezi wa kumi mwanzoni itaandaa mkutano wa Umoja wa Bunge wa Jumuiya ya Madola, utakaofanyika Arusha. Ni nafasi nzuri kwa wabunge kutoka nchi 53 kukutana, kuongea na kubadilishana mawazo na ujuzi juu ya mambo muhimu yanayoendelea kimataifa.
Ni mwaka ujao 2010 ambapo bunge zetu mbili yani Bunge la Tanzania na Bunge la Uingereza zitakapo kuwa katika mchakato mzima wa uchaguzi. Tanzania imekuwa na milolongo ya uchaguzi toka mwaka huu uanze na itamalizika mwishoni mwa mwaka huu, wakati Uingereza inakaribia kufanya uchaguzi mkuu mwezi june 2010.
Chaguzi kuu zote zina mambo makuu matatu. Zinahitaji matayarisho makubwa, zinahitaji uhamasisaji mkubwa hivyo kuleta hamasa kubwa na pia zina umuhimu wa pekee. Huu ndio muda ambao wananchi wanatumia haki zao za kikatiba kuwachagua viongozi wao wa kuwaongoza. Uchaguzi huru na wa haki unalihakikishia taifa. Utulivu, usalama na amani, hivyo kuheshimu uhuru na kuhamashisha ustawi wa kiuchumi.
Sisi Uingereza, tutaendelea kushirikiana na UNDP na nchi wafadhili wengine katika kuunga mkono sual hili muhimu la Uchaguzi Mkuu.
Ahsanteni Wote
---------------------------------
Kwa Taarifa yako:-
Siku rasmi ya kuzaliwa Malkia ni Aprili 21 ila imekuwa ni kawaida tangu mwaka 1805, siku hii imekuwa ikisheherekewa siku za kazi ili Waingereza wapate siku ya mapumziko.
Malkia Elizabeth II sasa ana umri wa miaka 83 ambapo huu ni mwaka wake wa 58th kwenye kiti cha kifalme. Mpaka sasa ni miongoni mwa watawala wa muda mrefu zaidi duniani kwenye utawala.
Malkia Elizabeth II ndiye Mtawala wa Uingereza na pia ndiye mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Sherehe hizi pia zimehusisha maonyesho ya shughuli zinazofanywa na Waandalizi wa Mbio za Mbuzi, Wonder Welders; Forever Angels Orphanage; TransTanz Mobile HIV Information and Clinic; Sauti za Busara Zanzibari Music Festival; Seas Sense Turtle Conservation NGO; Rhino Wild Dog Conservation; na kazi za Dr Mark Wood OBE, Eye Surgeon CCBRT.
Siku rasmi ya kuzaliwa Malkia ni Aprili 21 ila imekuwa ni kawaida tangu mwaka 1805, siku hii imekuwa ikisheherekewa siku za kazi ili Waingereza wapate siku ya mapumziko.
Malkia Elizabeth II sasa ana umri wa miaka 83 ambapo huu ni mwaka wake wa 58th kwenye kiti cha kifalme. Mpaka sasa ni miongoni mwa watawala wa muda mrefu zaidi duniani kwenye utawala.
Malkia Elizabeth II ndiye Mtawala wa Uingereza na pia ndiye mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Sherehe hizi pia zimehusisha maonyesho ya shughuli zinazofanywa na Waandalizi wa Mbio za Mbuzi, Wonder Welders; Forever Angels Orphanage; TransTanz Mobile HIV Information and Clinic; Sauti za Busara Zanzibari Music Festival; Seas Sense Turtle Conservation NGO; Rhino Wild Dog Conservation; na kazi za Dr Mark Wood OBE, Eye Surgeon CCBRT.
jamani mzee wetu ustaadhi al-haj Mzee Ruhusa ,vipi tena iko kinywaji ni?? Juice au labda povu?
ReplyDeleteHuyu Mama alitoa hutuba hii kwa
ReplyDeleteKiswahili kama ilivyo Au
Mheshimiwa umeing'amua kwa ajiri
yetu sisi wazalendo???
Ufafanuzi plz!!
Asante kaka Michu nilikuwa sielewi hotuba za nje, lakini umenisaidia kweli kuiweka kwa kiswahili,kweli Michu kingereza is richabo, asante kaka. Malkia wa shamba.
ReplyDeletewee anon hapo juu acha utani nasikia kakaetu michu anaongea lugha nyingi
ReplyDeleteKing'eng'e, kimombo, kiswaenglish,kimatumbi ebwanae listi ndefu.. kwa hiyo hiyo hotuba kaitafsiri. tena vizuri!
P.E.D
Kaka Michuzi,
ReplyDeleteUkiangali kwa umakini Utagundua kuna dosari kubwa katika hiyo banner ya Tanzania. bendera yake imewekwa kinyume katika hiyo banner. Ni vyema watu wakawa makini katika kupangilia rangi za bendera za Taifa. Mchirizi unatakiwa uanzie chini kuelekea kulia juu na si kama ilivyopangwa.
nakushukuru kaka.
Mwananchi
Loh!!!! afrika afrika afrika, stupidity beyond pale
ReplyDeletekutawaliwa kiakili ni tatizo baya kweli kweli
ReplyDeleteSasa sisi Waafrika wenye asili ya ngozi nyeusi, sasa inakuaje nashiriki katika kusherehekea siku ya kuzaliwa Malkia wa Uingereza bibi Elisabeth?
ReplyDeleteHivi tunajua kua huo ufalme wa England ndio uliokua muwekeziji mkuu kwenje biashara haramu ya Utumwa, (kuuzwa na kununuliwa kwa muaafrika mweusi).Kwani utii wa mgongo wa uchumi wao umetengemea kwa faida ya biashara ya utumwa.
Kwani baada ya Muingereza kutoka Plymouth Sir John Hawkins mwaka 1556 kufanaya safari yake ya mwanzo ya kuchukua watumwa afrika, akawa anatafuta wafadhili ili waboreshe hio biashara na Ufalme huo wa England chini ya Elizabeth 1 uka jitoleaa kuekeza 100% kwenye hio biashara haramu ambayo ilidunmu kwa zaidi ya miaka 400 , kutoka 1556 hadi 1830's. Waafrika wengi waliteseka na kuuwawa.
Sasa kwa kila muaafrika anayeungana na Elizabeth II, ni mtu aliyekua hayuko huru kifikra ni mateka wa kiakili ( msukule).Utafurahia vipi siku ya kuzaliwa ya mtu anayehusika na makosa haya.
Kumbuka kua Slave trade is one of the biggest crime in the
in the human history and the kingdom of England was economical built on the benefits of this trade, And since then the The Kingdom of England has refused to compensate Africans, they even ignore to do an official apology to Afrikans.For all Black Afrikans who celebrate her majestic birthday shame on you on your face x1000s.
Please search your history and it will shows, Or your lives are doomed in shame.
TUAMKENI WENZANGU!
mnajua kuwa malkia ana besdei mbili??
ReplyDeletewee annon kuhusu bendera ya tanzania...umeona ilo bango limekaa style ipi???acha wehu apa...
ReplyDeletelingelalishwa ingekaa ivo now imesimamishwa
birthday mbili???kivipi
michuzi NATUMAI HOTUBA HII ILITAYARISHWA KISWAHILI NA BIBIE AKAISOMA. MIEZI 3 NA SIKU KUMI MAMA ANABWABWAJA LUGHA KAMA MCHEZO. HONGERA SANKWA KUTHAMINI MAKAZI NA WAKAZI. BALOZI MWENGINE ANGETUACHIA VUMBI WATU TUTAFUT KAMUSI
ReplyDelete