mwili wa mmoja wa wafu waliofariki kwenye ajali hiyo Mei 29, 2009

Uongozi wakampuni ya meli ya Fatih Express ya mjini hapa umeandaa hitma ya kuwaombea watusita waliopoteza maisha katika ajali ya meli hiyo iliyotokea hivi karibunikatika bandari ya Zanzibar.


Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Said Abrahman Juma alisemamjini hapa jana kuwa, hitma hiyo itafanyika katika msikiti wa Ijumaa wa Malindi baada ya swala ya Alasiri na itahudhuriwa na wananchi mbalimbali wakiwamo masheikh mbalimbali.


“Tumeamuakufanya hitma kwa ajili ya ndugu zetu waliopatwa na matatizo, sisi tumeguswa sanana maafa hayo, hivyo tunaomba wananchiwote wanaoweza kuhudhuria wafanye hivyo ili tuwaombee wenzetu” alisema Juma.


Meli ya MV Fatih ilizama katika bandari ya Zanzibar Mei 29 na watu sita walipoteza maisha na mali nyingine mabalimbali zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Dar zilizama majini.


Kazi ya kuopoameli hiyo ilifanywa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Shirika la BandariZanzibar, Mustapha Aboud Jumbe na kushirikisha vikosi kadhaa vya ulinzi nausalama pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).


Hata hivyokazi hiyo ilichukua muda na kusababisha hofu kwa baadhi ya wananchi kwanikutokana na hofu ya kuwepo kwa miili zaidi ya watu waliopoteza maisha.


Serikali yaMapinduzi Zanzibar tayari imeunda tume kwa jili ya kuchunguza ajali hiyo, nataarifa zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni ili kuweza kutambua kiini cha ajalihiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2009

    umasikini ni kitu kibaya maanake wenzetu huwa wanalipwa fidia ya mamilioni sisi tunaambulia Hitma

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2009

    wewe mtowa maoni wa mwanzo ni nani alokwambia kuwa hapatakuwepo na fidia? wacheni kuruka ruka na kila mnalosoma. khitma ni suali moja nafidia nisuali jengine kabisa na linashuhulikiwa na watu wengine kabisa.

    ReplyDelete
  3. Hivi ni watu wangapi walipoteza maisha ktk hii ajali.Mara ya mwisho nilisikia maiti chini ya sita ndizo zilizoopolewa na idadi kubwa ya watu kutojulikana walipo.Michuzi naomba unipe jibu.
    Anon wa kwanza umesema la maana. Unajua bongo nashindwa kuelewa bima(insurance) huwa zinafanya kazi gani.Waliokumbwa na maafa haya wangewasue waendeshaji boti/insurance ya meli afu wangepata fidia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2009

    hivi jamani hii boti ilishiaje ilizama kabisa au iliopolewa, au ndio imeachwa hivyo ilivyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...