'Mziray na Mkamia wasitufanye vipofu'
Habari kaka Michuzi,
Nikupongeze kwa kua mstari wa mbele kwa kunyambulisha mambo mbalimbali kwa manufaa ya walio wengi.
Mi nimeona nipitie kwako kufikisha ujumbe wangu kwa jamii.Kichwa cha habari kinawaongelea watu wawili ambo ni maarufu sana katika medani za michezo hususani 'soka' hapa tanzania. Kocha Syllesaid Mziray na 'Kocha mtangazaji' Juma Mkamia.
Katika mechi ya juzi 3.6.09 wao ndio walikua watangazaji na watoa maoni mpira ulipokua ukiendelea kwa kweli walitaka kuturudisha zama za kale.
Kwa ufupi wameonyesha wazi kwamba hawawezi kukubaliana na chaguo la mwalimu wa sasa Maximo kwa sababu naweza sema hazina nguvu.
Kati ya vitu walivyokua wakilalamika ni kama ifuatavyo:Timu iemeundwa na wachezaji wageni na wachanga katika michezo ya kimataifa.
Kwa mfuatiliaj mzuri anaweza ona hawa jamaa ni vihiyo hata kama waswahili walisema 'kuishi kwingi ni kuona mengi" Unajiuliza Dihile,Nadir,Nyoni,Tegete,Ngasa,Mgosi,Nizar n.k ni wageni? au kwa kujumuishwa Kazimoto na Boko?
Tido Mhando ana kazi sana kwa bw Nkamia. Nilitegemea yeye asiwe na upande katika hili na kuwa na rekodi sahihi, lakini ndio kwanza atapata.
Mziray ameshafundisha Taifa Stars mara nyingi na hata vilabu Je timu yake ishawahi kufanya kama sasa? au atalalamika hakua na nguvu toka serikalini?
Kweli timu inahitaji kufanya marekebisho lakini si kuwakatisha tamaa wachezaji kukaa na mpira eti ni udhaifu. Je bila kuwa na uwezo wa kumiliki mpira unategemea timu iweje?
Waache maneno ya "kiswahili" na kutaka kuwaaminisha watanzania wote eti Athumani Idd ni bora sana. Mpira ni mambo mengi,kama hana nidhamu akae alipo.
Kwa kweli kwa mtindo huu watakua wanatufanya tuangalie mpira bila sauti kwani wanakera sana. Watoe maoni ya kitaalamu na si majungu ooh sasa Ngasa ameoa hali tena vigengeni...TBC wanapaswa kuangalia ni namna gani watapata watangazaji kama kina Jongo.
Asante
Mdau Perez

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    Mziray au A.K.A MDAU WA KISIJU!Ni mnafiki sana, yeye ameshazoea mipira ya ndumba, siku hizi watu hatuko huko ndio maana soka la tanzania limepanda, acha unafiki.

    MDAU MASHARIKI YA MBALI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    Naunga mkono hoja Mziray ana wivu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2009

    Mdau mtoa hoja na wewe unachekesha eti Mziray atoe maoni ya kitaalamu kwani ana utalaamu gani wa kutoa? Hayo majungu yake ndiyo utaalamu alionao.
    Siamini kama walikaa kwenye TV ya taifa na kuongea hizo pumba. JK naomba mwambie Tido atoe huo uchafu.

    ReplyDelete
  4. Mdau, umanganiJune 06, 2009

    Sijui niseme nakuunga mkono au miguu kabisa katika hili! Hawa makocha wetu kwa kweli hamna kitu kabisa, na ndio maana wanakuwa wanawategemea masuperstar. Hata ulaya unaona, mchezaji kama hana nidhamu timu inaweza kumuuza kwa kuwa nidhamu ndo kila kitu.
    Sasa nadhani macho yamewashuka baada ya dogo kazimoto kufunga goli la kimataifa.
    Bila hao madogo kupewa nafasi, lini watakuwa wazoefu? Waache majungu, timu ilishawashinda, wake kimya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2009

    Kaka Michuzi habari yz kazi pole na majukumu ya kurekebisha tabia ya wananchi wa nchi hii kama akina Mkamia na Mziray,hawa watu ni wapotoshaji na wanatuharibia mudi ya mpira,timu zote duniani zinakuwa nzuri zinapokuwa na uwezo wa kukaa na mpira,na huwezi kukuaa na mpira kama huna wachezaji wenye uwezo huo,mfano mzuri tumeona mechi ya Barcelona na Man Utd,Messi,Xavi,Iniesta ni lazima uwe na uwezo huo anachojaribu kukifany Maximo ni kuwapa wachezaji wetu uwezo wa kukaa na mpira na siyo kupiga pasi hata kama hujaona mtu aliye katika nafasi nzuri,waache majungu,mdau Osu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2009

    ...Nimemsoma huyu jamaa aliyetoa hii hoja yake...Ni vyema angefikiri kwanza kwa undani...halafu ndo atoe hoja yake kwa "evidence" na si kukurupuka tu...tutake tusitake soka letu la bongo ni kama "Homa ya vipindi" najua kwa wale wadau wa soka mnanielewa...ukitafiti sana toka maximo amekuja bongo (bahati nzuri nimeshuhudia mechi zake nyingi tu)utagundua si kocha wa timu ya wakubwa ya taifa ni kocha wa taifa ya vijana wanaohitaji majaribio kila mara....Katika nchi yeyote ile hakuna majaribio katika timu ya Taifa ya wakubwa kama anavyofanya huyu maximo kwa kisingizio(kila siku toka amekuja anasema kwa kuwapoza wadau eti) bado timu changa....timu ya taifa inatakiwa idadi ya wachezaji kwa asilimia 80 wawe "matured" yaani waliokomaa.pili;jamani huyu jamaa aelewe kwamba kocha ni kama mlezi na si kufundisha tu..kuna vitu vingi unatakiwa uwajenge wachezaji...ukikaa na wachezaji vizuri watacheza vizuri...lakini ukiwa na visasi kwa kisingizio eti hawana nidhanu hadi wakupigie magoti...kila siku utabadilisha timu usiku na mchana....amini usiamini hii timu angepewa kocha "mzawa"....tungekwenda Ghana mwaka jana...najua wengine mtapinga hili...fahamu kwamba timu tayari ilikuwa katika morali ya ushindi...lakini ubadilishaji wa namba za wachezaji na pia kubadilisha wachezaji kila mara ndiko kulikotuponza hata mechi ya msumbiji siku ile pale uwanja mkuu wengi tulihuzunika sana!!ntawapa mfano mmoja siku ile tulipowafunga bukifanaso kwao...hii ni baada ya maximo na mchezaji mmoja wa Stars kupewa kadi nyekundu ikalazimika sasa baadhi ya wachezaji kujipanga katika namba zao rasmi hadi goli likapatikana. Ukiangalia hata nchi zilizoendelea kimpira wachezaji wakorofi hawakosekani...lakini basi "saikolojia" ni kitu muhimu sana!!...sasa nauliza hivi maximo kununa kunamsaidia nini kwa wachezaji kama kaseja, chuji, boban...hawa wametoa mchango mkubwa sana kwa Stars kama mtakumbuka!!najua wengine watapinga hili naloongea...lakini kwa mtindo huu....Tanzania tutacheza CAF au kombe la dunia "labda" mwaka 2070!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2009

    Mtoa mada hapo juu unayosema ni kweli kabisa. Bwana Mziray alianza kumponda Maximo tangu siku za kwanza alipoanza kufundisha. Nadhani Mziray bado ana zile fikra za majina. Yeye mwenyewe juzi juzi aliitwa kwenda kuongeza nguzu Simba matokeo yake Simba ikafungwa... nadhani umefika wakati makocha wabongo wakubali kuwa Stars imebadilika badala ya kuwa na wivu usio na maana.

    ReplyDelete
  8. Wewe dogo wacha ushamba, hv kumfunga newsland ndio unamuona Maximo wa maana, mpira unatathminiwa kwa vikombe akivyochukua hebu nambie amebeba makombe mangapi tangu aje? hata kikombe cha chai kimemshinda!
    letu jicho...

    ReplyDelete
  9. Mziray?? Chazamani huyo. Hamfikii wala hawezi hata kupewa kazi ya kufagia veranda ya Maximo. Maximo ni msomi and modern kisoka. Kabla ya JK kuchukua madaraka si akina Mziray walikuwepo? Walifanya nini hakuna kitu. Ndiyo maana haishangazi soka yetu ni mambo ya ndumba na ulaji tu. Wacheni Maximo atubadilishe. Hofu yangu ni kuwa baada ya 2015 wakati JK kastaafu atakaekuja badala yake atamudu kunyanyua soka?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2009

    Kwa hii hoja nakuunga mkono 100% si hao tu hata baazi ya wengine… na baazi ya waandishi wa habari. Inasikitisha sana kuona watu wanamkandya Maximo na haya majungu yooote asilimia kubwa yameanzishwa na baazi ya makocha wazawa MZIRAY NAMBARI ONE (siwezi kuwaita makocha wa kizalendo maana nitakuwa napoteza maana) kupitia vyombo vya habari na hii ni chuki binafsi kuona mwenzao analipwa pesa nyingi. Wanachokifanya ni kuhakikisha hafanikiwi kwa lolote.

    Wakati Maximo anakabiziwa timu mara ya kwanza kabisa alisema namnukuu “We don have Michael Essien here, Ronaldinho or even E’too. Our team is very young and we need solidality and to work as a team and not individual…” wengi wenye mtizamo wa kuona na kufikiri mbali tulimuelewa. Labda kwa sababu binadamu tunatofautiana kwa uwezo wa kufikiri. Hii ni kutokana na watu kushindwa kutofautisha kati ya mataifa yalioendealea kisoka na mataifa yalio chini Tanzania tukiwemo.

    Maximo alipokuja makocha na baazi ya wadau walisaidia kumchagulia timu kwa sababu ilipaswa iwe vile kwa wakati ule kipindi ambacho alikuwa hajui kitu kuhusu soka la watanzania, ndio maana aliletewa wakina Mwaikimba Kaniki na wengine kibao wa ajabuajabu. Na alishutumiwa sana alipowajumuisha wachezaji vijana kama Jerry Tegete, Nurdin, Kigi, … kwamba amewachukua halafua hawatumii. Lengo la Maximo lilikuwa ni kuwaandaa ili apate kikosi ambacho kinanizamu na committed na baadae kitakuja kutusaidia kwa zaidi ya miaka kumi ijayo.

    Leo hii ukiingalia Taifa Stars wenye akili wote tunafurahi kwa sababu kwanza average ya umri wa wachezaji ni ndogo mno 21 or 22 na wana nizamu ya hali ya juu kila mmoja anajua wajibu wake hakuna star, wanawahi mazoezini tofauti na zamani kama yeye ni star simba au yanga basi anajiendea mda anao taka yeye. Hebu angalia Juma Jabu JJ. Mrisho Ngasa, Jerry Tegete Kigi Makasi, Mwinyi Kazimoto, Mgosi na wengine kibao bado ni makinda na watatusaidia hapo mbeleni na Wanatambua yeyote atakaeleta ujinga Maximo anamdelete na ikiwezekana anamfuata hadi kwenye bin na kumdelete paermanent (muulizeni kaseja maana ya kumdelete mchezaji permanent). Kwa kifupi maximo hazitaki BANGI, MIRUNGI, POMBE na MADAWA YOYOTE YA KULEVYA hata kama una kiwango ambacho wajinga wengi wanazani ni kizuri ukajifananisha na Rooney na kusahau kuwa Rooney mwenzio yupo nchi zilizoendelea kisoka na haitaji kwenda nje ya nchi kutafuta timu.

    KASEJA: kuna comment niliwahi kuisoma ikisema hili ni BOMU la kutupa kwa mkono. Exactly this is true. Watu wanamshutumu Maximo hajataja sababu za kumuacha kaseja. Ukifuatilia nyuma huyu kipindi kile cha hali ya sintofahamu ktk klabu ya Simba alihusishwa sana na migogoro kati ya viongozi kwa viongozi, wachezaji kwa wachezaji, na wachezaji kwa viongozi na kuigawa timu. Huyu hafai msikitini wala kanisa hata Bangi inaelekea anavuta. Aliuvua utaifa na kudiliki kushangilia IVO alipofungwa goli SABA, Nne Senegal na Tatu Angola akiwa na Yanga huku akisahau Enyimba walipom’buruza SABA Nje Ndani na alipokuwa Taifa hata yeye aliwahi kuchomwa Nne na Kenya au anafikiri tumesahau. Kama ni bora si angezuia…sio kila kitu maximo akupe sababu fikiria!

    Hizi ni baazi ya BANGE; Athuman Iddi Chuji, Haruna Moshi Boban, Gaudensi Mwaikimba Crouch au Joseph Kaniki Golota sihitaji kuzijadili na hazihitajiki.
    MAKOCHA WAZAWA: hawa hawana jipya ni mabingwa wa sababu na majungu ndio maana hata leo hii England Wamemuhire CAPELO baada ya kuona wazawa hawana jipya kama mi muongo waulizeni kuhusu Steve Macraren. Walipokuwa wakinamziray wananoa Timu ya Taifa tukifungwa tu utasikia aah Mvua imenyesha uwanja umejaa matope, Maandalizi duni, posho hatujapewa , refa katuuwa. Sababu zao ukiziziunganisha ni kutoka Mtwara hadi Mwanza. Leo hii ndio wanajifanya wataalamu wa soka wanayaona mapungufu. Sawa na mwanafunzi akiziangalia past papers anaziona nyepesi kweli na kujifanya yeye ndio ticha wakati yeye bado ni mwanafunzi. MZIRAY UTAKE USITAKE WEWE BADO NI DENT KWA MAXIMO.

    Lumbo
    Ars

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2009

    kwanza mziray siyo kocha kama ni professional yake yeye ni mtaalaam wa viungo physical education sasa ukocha kauanza wapi huu ni wizi mtupi. alipewa klabu nying hazifundishe ila kaishia wapi? taifa stars alishafundisha ilifika wapi mwacheni maximo kuja yeye angalia timu yetu au nchi ilivypanda chat kwenye kimataifa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2009

    wewe anony wa june 6, saa 8.01 uwe unaelewa unachokatazwa acha kulinganisha mataifa yalioendelea kisoka na na mataifa machanga. usijifananishe na nigeria ambao wachezaji wake wote wanacheza ulaya ambako kuna makocha wataalamu sio kama wazawa wakwetu wanaofundisha kwa nguvu ya KALUMANZILA... eti unasema wazawa wangeifikisha timu Ghana kutokana na hamasa iliyopo pu?,<;vu wee kuna timu yenye hamasa kama England hapa duniani waulize mzawa aliipeleka wapi.. timu haishindi uwanjani kwa hamasa timu inashinda kwa utaalamu.. eti angetumia wazoefu kama CHUJI BOBAN na KASEJA eti wanahitaji saikolojia si waende kinondoni ambako kuna ENGO's zinazojihusiha na saikologia ya mateja taah/<,"-ra wee unatetea BANGI si waende wakaimbe leggae kwani huo sio mchezo? kama ulikuwa unakwenda uwanjani huku ukiwa na jazba bora uache kwenda...
    Timu ya taifa itajengwa na Vijana ambao lazima tuwaandae sasa kama Juma Jabu, Mrisho Ngasa, Mwinyi Kazimoto, Jerry Tegete,Nurdin Bakari, Kigi Makasi na wengine kibao ambao ni hazina ya baadae na sio hizo scrap ambazo zote ziliamua kucheza soka baada ya kuona kubeba mizigo stand kumewashinda...
    toka mwaka 1982 mpaka maximo anaichukua timu hatujawahi kushiliki mashindano makubwa na hao hao wazawa wako lakini juzi juzi tu tumeenda Ivory Coast... huoni huo ni mwanzo mzuri... wapuuzi wenzio wanamfananisha na wenger kutumia chipukizi na kumlaumu ndio maana timum inafanya vibaya... yaah fine! unapoona huna resources you have to use alternative for the betterment of the future... Wenger Hana uwezo wa kununua wachezaji kwa gharama kubwa kama ManU, Chelski, Liver au Madrid ndio maana juzi alisema atakuwa mjinga akishindwa kununua mchezaji bora wakati anazo zaidi ya GB100mill bank. hata Maximo angekuwa mjinga kama Kuna Wachezaji wazoefu na Wanacheza soka la kulipwa barani ulaya sio hapa kwetu simba na yanga ambapo upeo wako ndio umeishia.
    leo hii unasikia Ngasa ameenda kufanya majaribio WH hayo ni matunda ya program za Maximo huoni hapo nuru imeanza kufunuliwa au ulitaka aende uarabuni ulipozoea.
    Tunajifunza historia ili kuelewa yaliopita na tuweza kufanikiwa baadae. hao wazoefu tumewatumia sana tena sana lakini hawajatufikisha popote zaidi ya sababu kila mechi. tunatakiwa tujenge kizazi ambacho kitatusaidia siku za usoni.
    Roma haikujengwa kwa siku moja

    Nondo
    Ars

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2009

    mziray hana tofauti na bendi ya shikamoo jazz. mie sku hz naipenda taifa stars sababu soka linatandazwa eti. hata kama wanafungwa lakini ukweli ni kwamba soka lipo. kina mziray wanaturudisha nyuma shauri ya mawivu yao tu. sie na maximo wetu tunasonga mbele na mie namtia moyo aendelee kujenga timu chipukizi yenye discipline na tutafika tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2009

    Anon..June 6, 11:16 AM, Ngasa kwenda kufanya majaribio WH ni matunda ya Maximo au Kondic wa Yanga?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 06, 2009

    ..Nimesoma kwa umakini... watu wengi wamechangia hii hoja kwa ama kwa jazba tu!! au kwa ushabiki wa namna fulani hivi!!...na hasa huyu "Nondo" hapo juu...hah! hah! hah!..wabongo bwana!!mkishinda maneno meeengi!!sifa nyingi kwa maximo!!! mkifungwa!! mnageuka kama bendera na kuanza kumponda!!!....eti maximo kabadili mpira wa bongo!!...wapi?....kama nilivyosema hapo awali wengi wao wanatoa comment tu kwa kukurupuka....tunaponda makocha wetu na kusifia wa nje!!...hii inashangaza sana!!...ukweli ni kwamba kinachomsaidia maximo kue-exist ni mazingira tu. Miaka ya nyuma kulikuwa hakuna hamasa na support kwa wadau kuhusu soka kama ilivyo sasa..na ndoo maana makocha wazawa waliopita...hawakuwa na uwezo wa kuifikisha mbali Tanzania katika ramani ya soka.Kama utafuatilia vizuri hutapinga hili naloongea.ntawakumbusha mfano mmoja tu..zamani timu ikiingia kambini eti inaenda JKT Mgulani...chakula ugali na maharage...hii ilikuwa soka au mafunzo kwa ajili ya kujenga taifa! Kama "mashimo" asipobadili staili ya kufundisha na kukaa na wachezaji...nawaambia itakuwa ndoto kwa Tanzania kufikia kule tunakoelekea!!! labda baada ya miaka 60!!!ijayo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2009

    ...wanaongea kwa ushabiki tu...Tanzania ni ndoto za mchana tunaota...kama bwana maximo hatobadilika katika ufundishaji wake!jinsi ya kukaa vizuri na wachezaji wake! na pia kila mara kubadilisha wachezaji!...timu ya maximo ni kama ya Aseno!! kila siku kocha anasema"wamecheza vizuri" mara hoo "bado wachanga"...jamani timu ya taifa si ya kufanyia majaribio!!...kocha gani hadi leo hii huna "first eleven!! hii inashangaza sana! kwa mtindo huu timu itaendelea kuwa kama "Homa Ya Vipindi"

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 06, 2009

    OOOHHH Kula tano..Nondo Ars.
    Umepigila msumari mu kichwa mmm I mean umehit target.
    BAELEZEEEE BANA MZIRAY MWENYEWE KESHAJIZEEKEA ANATAFUTA PA KUMALIZIA AVUTE PENSION.
    MDAU WA LONDON.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 06, 2009

    TATIZO LILIPO KWA NDUGU MZIRAY TFF AWAKUMPA ULAJI ANGEPACHIKWA SEHEMU YA ULAJI WALA KELELE ZAKE TUSINGE ZISIKIA,KATIKA SWALA LA UFUNDI WA SOKA MZIRAY HAMFIKII MAXIMO KWA LOLOTE.KAMA YE ANAUCHUNGU NA NCHI HUU MWAKA WANGAPI HATUNA TIMU YA MIELEKA YA TAIFA SI ELEKEZE NGUVU NA UTAALAMU WAKE ALIOSOMEA KATIKA JUDO KWANI MPAKA SOKA,TENA ATUKOME SIJUI KAZUKIA WAPI ENZI YAKINA KILAMBO,DILUNGA,MUCHACHO,CHUMA CHA NTWARA,MZIRAY ALIKUWA DABAGA ATA VIATU AJUI KUVAA.

    ReplyDelete
  19. Baba UbayaJune 06, 2009

    Tanzania bora iendelee kunolewa na wageni.si lzm awe Maximo bali yeyote lkn hao vichwa vya wendawazimu(makocha wazawa waliopo) hakuna kitu.kwanza wengi wamesomea kozi zile za soka la zamani.bado wanatumia vitabu vyenye mbinu za kina Pele.
    cha muhimu ni kwamba,vijana wapenda soka wajue kwamba elimu si mpaka uwe daktari ama mchumi.vijana waende wakasomee soka jamani ili waje waisaidie Staz.ama wakasomee michezo tu kwa ujumla maana michezo iko mingi TZ ambayo inahitaji sana walimu wenye utandawazi na teknolojia ya sasa.Badala ya Business MGT,wengine wachukue Sports MGT.hiyo pia itasaidia kuongoza vilabu vya soka kwa kufuata karne inayokuja.how abt that!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 06, 2009

    NO! NO! NO! NO! JAMANI HIYO SIYO KLABU NI TIMU YA TAIFA IKIWA NA MAANA YA WOTE; UWE MTANGAZAJI, KOCHA, MCHEZAJI WA ZAMANI WA SASA KILA MTU ATASEMA ANAVYOONA. NDIYO MAAANA KUKAITWA UHURU WA ....
    KAMA WATU HAWAAFIKI MAONI YA MKAMIA AU MZIRAY NI WAO NA WATOE DUKUDUKU LAO. SIYO KUWASHAMBULIA WATU KWA CHUKI.
    NILIKUWA NASIKILIZA ENGLAND IKICHEZA NA KAZAKHSTAN. ALAN GREEN NA MWENZAKE WA BBC RADI 5, WALIIPONDA TIMU LEO LICHA KWAMBA IMESHINDA 4-0 LAKINI HAWAKURIDHISHWA NA KIWANGO CHA TIMU YAO YA TAIFA. NA HAO WALIKUWA WANATANGAZA LIVE KUTOKA KAZAKHSTAN.
    NI WAJIBU WA MTU YOYOTE BILA CHUKI, JINSIA AU VINGINEVYO, KUTOA MAONI YAKE BINAFSI YANAWEZA KUPINGWA AMA KUKUBALIWA.
    HIYO ITAONGEZA CHACHU NA JUHUDI KWA WALE WANAOKANDIWA NA KUONYESHA UWEZO ILI KUWABADILI MAWAZO HAO WAKANDIAJI!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 06, 2009

    madu June 06, 2009 12:53 PM, Ngasa amekuzwa na Maximo siyo vinginevyo. Unakumbuka mara ya kwanza alipomchagua timu ya taifa wenye midomo walivyosema? Kama unahudhuria mazoezi ya taifa, umeona muda ambao Maximo anachukua kuongea na Ngasa na kumuelekeza ili awe mchezaji bora?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2009

    Ukitaka kujua Mziray&co ana mapumba kichwani check hapa...
    Italy also had an inexperienced line-up with Gennaro Gattuso and Fabio Grosso the only survivors from the 2006 World Cup final win over France for the game played in front of only 8,000 spectators.
    Italy wana kikosi kipya cha wachezaji chipukizi kabisa.na mazuzu wengine wacheck hapa.....
    But the young side will take heart from a solid, if not inspiring, performance against their hosts who could see under-fire coach Berti Vogts sacked following the defeat.Mziray hana jipya ni mzee aliyejizeekea bado anwaza ndumba na ngai katika sports..

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 07, 2009

    Napenda kuunga mkono hoja ya kutokuridhishwa na watangazaji Nkamia na Mwenzake Mziray. Nadhani siyo sahihi kwa wao kuikosoa timu ya taifa kupitia televishin ya Taifa ambayo inalenga kuwahudumia watanzania wote. Nasema siyo vizuri kuikosoa timu ya taifa wakati inacheza kwa sababu athari zake ni kukatisha tamaa WATANZANIA ambao kimsingi walitakiwa kuishangilia kwa nguvu zote kuanzia mwanzo wa mchezo hadi mwisho hata kama imefungwa. Moyo huo unatakiwa upatikane kutona na upenzi, mchezo mzuri, matarajio/matumaini, vyombo vya habari hasa vile vinavyo lipiwa na kodi zetu.
    Mimi bahati mbaya sikuuona huo mchezo kwa sababu niko nje ya nchi, lakini nilipigiwa simu na mtoto wangu akiwa na mama yake baada ya mchezo. Simu ilionyesha jinsi walivyofurahi na hasa goli la pili lilivyofungwa. Hii ina maana mke wangu na watoto walikuwa wanaangalia. Nyumbani kwangu kuna cable, DSTV na station mbalimbali, lakini kwa siku hiyo walikuwa wanaangalia TIMU YAO YA TAIFA, siyo Manchester United au Real Madrid. Lakini kinanisikitisha kama kulikuwa na comments za watangazaji wanaolipwa na sisi na kuweka maneno ya kuhuni, kibabaishaji, kikukosa maadili. Maneno kumhusu ndoa ya Ngasa na Kula gengeni, hayatakiwi kusikiwa na mtoto wa miaka chini ya 14 ambao ni wengi watakuwa walikuwa wanaangalia siku hiyo. TBC hawana code of conduct! yaani Nini kisemwe na wakati gani!.
    Unajua huu mtindo wa kuiga iga huu una madhara makubwa sana. Na haya nimeyaona kwa TV yetu, kuna mambo wanajiingiza kwa lengo la kutaka kuboresha, lakini wanachefua kwa sababu sisI walipa kodi hatuyahitaji kabisa. TBC haishindani na DSTV au ITV, kwa sababu wao hawafanyi biashara. Kutokana na hili ndiyo maana wanakuja kina Mziray na kufanya ukosoaji mahala pasIpo husika kabisa. Na ndiyo maana mtoa hoja anasema ina chefua.
    Ningukuwa mimi ni TBC siku yoyote timu ya taifa inapocheza ina kuwa ni kuisifia na kuhamasisha tu period. Hakuna kitu kingine, Mbona wakati wa magwaride ya kitaifa huwa ni kusifia tu hata kama kuna mahala msitari haujanyoka, kwa nini wasiseme afande fulani hanyayui vizuri miguu. Kwa hiyo kuikosoa Timu wakati inacheza ni kukosa Uzalendo! kutokuwatendea haki wenye timu yao! Kutokuwatendea haki wachezaji na Maximo wao, kwa sababu ilitakiwa wao na wao wawepo ili kutoa tathmini chanya, kutokujua wanalolitenda nk nk nk nk nk.
    Timu ya taifa ni kitu pekee kinachowaunganisha watanzania kwa sasa, asitokee, mhuni tena kupitia TV yetu kutusambaratisha na kutuharibia watoto wetu na mada zilizokosa uzalendo na maudhui finyu au ya kihuni.
    Maximo namheshimu, anajaribu kurejesha heshima yetu iliyokuwepo enzi za kina Tostao, Adolf Rishard. Muulizeni Mziray na Mkamia kama walikuwepo kipindi hicho.
    MUNGI IBARIKI TAIFA STARS, MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 07, 2009

    MAXIMO HANA JIPYA.ANAISHI KWA MAJUNGU TIMU YA NEW ZEALAND HAINA UWEZO WA KIMPIRA.
    NGASSA ANAWIKA SIKU NYINGI SIO MAXIMO ALIYEIBUA KIPAJI CHAKE NA ALIKUWA AKIMKATAA MWANZO.
    MZIRAY AMETULETEA KOMBE LA CHALLENJI 1994.MAXIMO KALETA KOMBE GANI? LA MAJUNGU?
    MDAU KISIJU.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 08, 2009

    Wadau, tunagalie pande zote za shilingi Maximo ana matatizo japokuwa wadau wengine humu ndani mnaona ndivyo sivyo, swala la yeye kugombana na wachezaji na wasaidizi wake linaonyesha kabisa kuwa huyo mzee ana matatizo, kwa hiyo ingekuwa bora sana watu wengine mkaangalia na upande huo pia, mimi mwanzo alipoumuacha Kaseja nilikubaliana naye kabisa kuwa huenda Kaseja ana matatizo ya kinidhamu lakini kadri siku zinavyokwenda mbele niliona kuwa huyu bwana ana matatizo baada ya kuendelea kuwa analumbana na wachezaji wengine zaidi na kuanza kuwagawa wachezaji waziwazi sidhani hiyo kama kocha ambaye ni kama baba kwa hao wachezaji alipaswa kufanya. Nakumbuka wakati Maximo anakuja bongo kuja kuanza kuinoa taifa stars nilimtafuta Maximo kwenye mtandao ili niweze kujua historia yake ya kimpira kitu kimoja nilichokiona ni kukaa kwake kwa muda mfupi sana katika club moja ya daraja ya kwanza huko Scotland, alikaa kwa miezi minne tu katika mkataba wake uliotakiwa kuwa wa mwaka mmoja, sababu iliyotolewa ni kuwa alijisikia mpweke na kukumbuka sana nyumbani lakini hiyo haiingii akilini kabisa, na ukisoma zaidi kwenye habari hiyo utaona mwenyekiti wa klabu hiyo alimuhakikishia Maximo kuwa sababu za kuondoka kwake zitaendelea kuwa siri, naambatanishi link ya habari hiyo hapa chini. Hayo yote pamoja na mambo ambayo mpaka sasa yametokea yanafanya watu wengine tumuone MAximo kwa jicho lingine zaidi, angalia kuondoka kwa wasaidizi wake na yule kocha wa viuongo baadaye kurudi tena na kufundisha Azam hayo yote yanaoneka kuna matatizo upande wa huyu bwana.
    http://news.bbc.co.uk/sport1/hi/football/teams/l/livingston/3190612.stm

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 08, 2009

    Wengi mnaomponda Mziray hamjuwi historia ya mpira wa tanzania,mmezaliwa kipindi cha maximo! kabla ya maximo tulicheza mataifa huru,kabla yake tumechukuwa challenge! huyo maximo pamoja na gharama za wadhamini zanazozidi bilion na hamasa ya watanzania pamoja na wachezaji.hivi jamani kuifunga new zelland ndio kipimo cha mafanikio,kwanza timu inatoka sehemu ambapo hakuna mpira wa ushindani hata Australia waligundua hilo wakahamia Asia.mashindano huko timu mechi mbili imepata mabao 53! kuweni na uchungu na wazawa hawa kina maximo kwao njaa wamekuja kutunyonya tu. kila siku anataka awape njia ndugu zake wabrazil na si kuendeleza soka.kocha gani ana u simba na yanga? majungu ndio aina ya maisha yake.tusubiri tutakapomtoa na bakora.na TFF wakishaona tumemchoka wanatuletea timu vibonde ili kutuziba midomo,jamani hatuangalii ushindi kwa vibonde,kwa kuanzia hata challenge tushinde basi.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 08, 2009

    baada ya kusoma comment hapa nimegundua kwamba maximo anaanza kufanikiwa kuimarisha nidhamu, kwa sababu wengi wameamua kueleza ukweli kuhusu nafasi ya mziray kwenye soka la tanzania, mziray sio kocha, mtu yeyote mwenye taaluma yeyote ile hawezi kumkandia hadharani mwana taaluma mwenzake bali humrekebisha kwa kumwambia mwenyewe na kama haambilikia basi huanzisha huduma yake ambayo itasaidia kurekebisha mapungufu ya mwenzake. sasa mziray kama una aina nzuri ya ufundishaji wa mpira anzisha timu yako, fundisha, tuikutanishe na ya maximo itakayokuwa bora itakuwa ya taifa! yako ikiwa bora tunamfukuza kabisaa maximo, ukocha wa taifa tunakupa wewe. kitendo chako cha kumkandia maximo mara kwa mara kinaonesha jinsi ulivyokosa nidhamu kama hao jamaa zako akina chuji,boban sijui na nani mwingine sitaki hata kuwakumbuka! nani kakwambia kwamba huyo chuji na bobani ndio taifa stars?? kama wao ni wachezaji wazuri, walipoachwa na maximo si ndio wakati mzuri wa wao kukimbilia ulaya kwenye soka la kulipwa? mziray huna nidhamu, enzi zenu ninyi taifa stars ilikuwa kichwa cha mwendawazimu, aliyesema hivyo bado yupo mzimaa, nenda kamuulize taifa stars ya sasa chini ya maximo bado ni kichwa cha mwendawazimu? atakujibu na jibu hilo litumie kujipima (mziray na wanaomkandia maximo) kiwango. wakati ule wakina mziray mkipewa timu hata kama mlikuwa mnapewa pesa kidogo, zaidi ya robo tatu ya pesa ya wachezaji hamuwapi, mnapeleka majumbani kwenu, sasa nafasi hiyo hakuna mnabaki kuongea fitina tu. ombi kwa mh kikwete akitoka maximo tunaomba kocha mwingine bora zaidi lakini sio akina mziray.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 08, 2009

    Maximo aondoke amekaa miaka mitatu hana first eleven.
    unaweza vipi kumuacha Godfrey Bonn wakati ndio kwanza anawika? eti ana miaka 28 ni mtu mzima. hivi kocha wa ivory coast anaweza kumuacha DROGBA kwa vile ana miaka 31?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...