Balozi Mohamed Maharage Juma akimpongeza Mwenyekiti mpya wa jumuiya Bw Muhamed Shariff katikati ni Consul General Ali Ahmed Saleh
Baada ya mkutano kama kawa palikuwepo maanjumati ya kukata na shoka na juisi na soda kwa wingiiii...
ze fulanazzz na kapelozzzz za jumuiya ya wabongo UAE
Mgeni wa heshima Mhe. Mohamed Maharage Juma, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu aliyeongozana na Bw. Ali Ahmed Saleh Consul General wa Tanzania Dubai na Emirate za Kaskazini za UAE wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wapya wa TAE. Mhe Balozi aliupongeza uongozi uliomaliza muda wake kwa kazi nzuri walioifanya ya kuasisi Jumuia na kuifikisha ilipo sasa na kuupa chanagamoto uongozi mpya kufanikisha malengo ya Jumuia na akaahidi kwamba Ofisi za Ubalozi na Consulate zitaendelea kufacilitate shughuli za Jumuia kwa kadri ya uwezo wake.

Tarehe 5 Juni 2009 Jumuia ya Watanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (Tanzania Association in the Emirates, TAE) ilifanya uchaguzi wa viongozi wapya watakaoiongoza jumuia hiyo kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
Mkutano huo ulifuatiwa na shuhguli za kutunisha mfuko wa jumuia kwa Mhe Balozi kunadi kadi nambari 01 hadi 05 za Jumuia uuzwaji wa fulanazz na kapelozzz za Jumuia pamoja uzinduzi tovuti ya Jumuia hiyo ambayo ni www.watanzania-uae.com
Viongozi wakuu wapya wa
jumuia ni kama ifutavyo:
-Bw. Muhammed Shariff Mwenyekiti
-Bw. Mbarak Ahmed Naibu Mwenyekiti
-Bw. Shabir Damji Katibu Mkuu
-Eng. Issa Majid Maggidi Naibu Katibu Mkuu
-Bw. Mohamed Manji Mweka Hazina
-Bw.Hassan Ally Abri Naibu Mweka Hazina
-Bw Abdulrahman Hassan Mkurugenzi, Kurugenzi ya Jamii na vijana
-Bi Rahma Buheti Mkurugenzi Kurugenzi ya Wanawake
-Bw Isaac Peter Mkurugenzi Kurugenzi ya Mawasilano na Uhusiano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    Huko sisi wengine hakutufai.Hata kinywji kikali kimoja hakuna !!
    Nitashindwa kupata ile kitu roho inapenda !!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    Hivi wtz waliopo huko ni waislam watupu?? Hata kama ni Uarabuni.... Enzi za mwalim safu hiyo ingepanguliwa!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2009

    Du hizo 7ups! !!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2009

    Haya Ndo Mambo Ya Kuigwa Sio Matawi Ya CCM Ughaibuni Aibu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2009

    ANONYMOUS WA PILI, TARATIBU NDUGU YANGU, WEWE MTU MZIMA NA TUNAKUHESHIMU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2009

    www.watanzania-uae.com vipi washikaji huko hakuna nafasi za kazi mbalimbali ambazo wabongo tunaweza kuja kufanya UAE kama walivyojaa wapakistani, wa-misri n.k

    Vipi kuna uwezekano wa kuongeza ktk webusaiti yenu masuala ya kazi, vyuo n.k ktk UAE?

    Maana Tanzania na nchi za ghuba tuna uhusiano wa jadi, hivyo Mh. Balozi Maharage na Wadau waliopo UAE tuunganishieni michongo kwa technohama tuweze kusaidia uchumi wa bongo.

    Mdau
    Bosco
    DSM.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2009

    Mdau wa Dar es salaam, Bosco,
    Salaam wazo lako ni zuri na lina fanyiwa kazi.Ahsante sana
    Ubalozi/AbuDhabi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2009

    uongozi kavua nyani anapewa ngedere!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2009

    duh...wadosi hapo pia wamo...jitahadharini mifuko yenu,manaake mbongo bado mnyonge!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2009

    annon wa#2,,swali lake zuri tu tena saaaana

    wee annon unaesema eti "taratibu tunakuheshimu" wee ndo nyamaza
    mana apo ukiangalia kuanzia balozi "simply"ni nchi ya kiislam au??na mwenyekiti sijui na nani

    ivi udini utaisha lini?dini zenyewe sio asili yetu waafrika afu tumekalia izo imani ambazo practicability yake ni F
    tufanye kazi,tusome weee,tutunza familia zetu...full stop

    me nafikili uhuru wa kuabudu wengine unafinywa sana na utafatiliwa weee adi urudi kwenu

    afu mijumuiya ya nini,ivi nyie nanyi hamjifunzi kwa wezenu kule kwa waosha vizee?

    ni hayo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2009

    mnalia sahani gani izo???

    kazi kweli,na nyie pia jumuiyazzz??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...