JK, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Waziri wa Majui Profesa Mark Mwandosya wakizungumza wakati wakikagua mitambo mikubwa ya kusafisha maji iliyopo katika kijiji cha Ihelele Wilaya ya Misungwi jana mchana.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa nmdiye aliyeasisi mradi huo mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga
JK akimtwisha Maji Bi.Janet Fadi Mkazi wa mtaa wa Ndala Shinyanga mjini wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kuchotea maji mjini Shinyanga.Kituo hicho ni sehemu ya Mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga uliozinduliwa na JK jana
JK akifunua kitambaa katika jiwe la Msingi katika kituo cha maji Mjini Kahama jana huku Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya akiangalia.Kituo hicho cha maji Mjini Kahama ni sehemu ya Mradi wa Maji Kutoka Ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga uliozinduliwa na Rais Kikwete jana na kuhudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa.

akimpongeza msanii chipukizi Farida Fadi(7) baada ya kusoma shairi zuri wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kuchotea maji Shinyanga mjini jana.Sherehe za uzinduzi huo ni sehemu ya Mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga.Msanii huyo chipukiizi ni mwanafunzi katika shule ya Msingi Ndala, Shinyanga mjini. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu



HABARI KAMILI
JK amezindua mradi mkubwa wa maji kuliko yote Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Ziwa Victoria ambao umegharimiwa na Serikali ya Tanzania bila ya msaada wa wahisani kwa zaidi ya Sh bilioni 200.


Uzinduzi huo ulionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa,TBC1.
Katika hotuba yake ya uzinduzi uliofanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza jana, Rais Kikwete alisema uzinduzi huo ni sehemu tu ya utekelezaji wa ahadi za serikali yake kwa wananchi .

Alisema mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake za kuwapatia wananchi maji safi na salama.

Aidha alimsifu Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyekuwapo katika uzinduzi huo kwa uthubutu wa kuamua kuanzishwa kwa mradi huo.

“Ndani ya Ilani ya CCM, mradi huu ulipaswa kukamilika mwaka 2010, Rais Mkapa alituachia na akaamini tutaweza na kweli Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha mradi huo kabla ya wakati uliokuwa umepangwa.

“Hii inadhihirisha CCM inaweza. Tumewaweza Busanda na bado tutaendelea kushinda, na mradi huu ni ushahidi,” alisema JK..

Mbali na Mkapa, JK pia alimshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye pia alihudhuria uzinduzi huo, kwa usimamizi mzuri wakati wa uanzishwaji wa mradi huo wakati akiwa Waziri wa Maji.

Pia aliwashukuru mawaziri walioiongoza wizara hiyo katika nyakati tofauti za utekelezaji wa mradi huo wakiwemo Stephen Wasira, Shukuru Kawambwa na Waziri wa sasa wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo unaopita katika mkoa wa Mwanza hadi Shinyanga wilayani Kahama, utafaidisha vijiji 54 na wananchi zaidi ya milioni moja watakuwa wakipata maji kwa saa 24. Rais alikemea tabia ya baadhi ya wananchi ya kuharibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

“Kuna baadhi ya watu hapa wanakwenda kukata mabomba na kuchukua vifaa wakidai vya Wachina.

“Vitu hivyo sio vya Wachina, serikali imegharimia kwa fedha zake halafu nyie mnakwenda kunyofoa kisha mkikosa maji mnalaumu serikali, vitendo vya kuharibu miradi ni upuuzi na inasikitisha,” alisema JK.

Aliitaka mamlaka iliyopewa jukumu la kusimamia mradi huo chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sai, kusimamia na kuendesha mradi huo kwa ufanisi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2009

    kidumu chama cha mapinduzi. Kidumu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2009

    Yani tumesha fikia kuona kua mradi lazima ufaziriwe na watu wa nje.Jamani nchi lazima kuendeleza miladi kwa kodi sio wafaziri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    hahahahha sisiemukweli mnaweza yote, hebu wapeni na wengine basinafasi muone, mtajisifu kila siku kwa kuwa kiti mmekikalia hamtaki kuwappa wengine wakajaribu wanaowezakufanya mabadiliko, hebu kuweni kama nchi nyingine sio chama kimoja kitawale for life!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    Hivi CCM imengiaje kwenye hili? Mimi ninavyofahamu mradi huu umetokana na kodi za wananchi. Halafu kujisifia eti CCM inaweza ni ujinga tu. Mbona kuna mambo mengi tu ya msingi hayajatafutiwa ufumbuzi? Kwa kifupi ni kwamba Uchovu wa Tanzania ya leo umeletwa pia na CCM.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    Tanzania kweli tupo nyuma sana kimaendeleo... nilipofatilia kampeni za Obama niliona mabango meeeeengi sijui "Now We Can", "We Need Change", Bendera, Vipeperushi, n.k. Baada ya kuchaguliwa upuuziiii wooooooote huo sasa siuoni iwe kwenye majanga, shughuli za kitaifa, maendeleo au za kimataifa nikimuona Obama na Serikali yake kweli sioni huo upuuzi ninacho kiona ni Bendera ya Marekani tu labda na ya Nchi nyingine in case of international matter. hii inamaanisha serikali ya Obama ipo kwa ajili ya, na inawawakilisha Waamerica wote wala sio Wademocratic pekee.
    Sasa turudi nyumbani:
    Iwe shughuli za kitaifa raisi akiwepo sare za CCM nyingi hata sometime bendera ya taifa hatuioni, Iwe maafa kama mbagara Sare za CCM, iwe uzinduzi wa Miradi sare za CCM, iwe sherehe za kitaifa Sare za CCM... hotuba ya raisi CCM imefanya hivi vile... mi naona kama inawezekana tubadilishe bendera ya taifa iwe ya CCM hata wimbo wa Taifa uwe wa CCM. huko nchi za nje wakibrouse au kuangalia kwenye TV watu watafikiri bendera ya Taifa letu ni rangi ya kijani na ngao yetu ni jembe na nyundo.
    anyway tusilaumu sana kwa sababu raisi ni wa CCM, wakome wapinzani kwani hakuna aliyewalazimisha kuwa huko... sasa fainali ni kwetu sisi tusio na vyama hatumjui raisi wetu, wala serikali yetu... ingekuwa ni bendera ya taifa tu ndio inapepea au sare zilizoshonwa na zenye nembo ya taifa hapo ningesema raisi ni wa wote na serikali ni ya wote.

    "Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza"

    Lumbo
    Ars

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    duh CCM iko juu! yani hiko kitoto wameshakiteka?!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2009

    JK keep it up kuwasafisha mafisadi Mkapa na Lowassa..Ila ujue kuwa tutapandA ndege kuja kupiga kura 2010 na bado hatujasahau huyo lowassa wako unaejitahidi kumbeba lkn jua habebeki binafsi huwezi kunikomvinsi kama na wewe ni mtakatifu ikiwa unawabeba mafisadi lazima kuna namna hapo nyerere hakuwa mnafiki kama hivyo hata ungekuwa mwanawe ukiboronga kamwe hakubebi kama wewe unavyowabeba mafisadi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2009

    EBANA CHEKI MKAPA ALIVOFUTUKA DUH!!!
    ANAKULA VIZURI KWELI ALICHOCHOTA KWA MIAKA KUMI...KWELI TAMBARARE!
    MUNGU BARIKI TANZANIA..

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2009

    HUYO MTOTO AMEBAKWA, KWANI UMRI WAKE HAURUHUSU KUJUA CHAMA GANI NI SAHIHI KWAKE, ILA WANACCM WAMEMPA SHAIRI NA MAELEKEZO YA NINI CHA KUFANYA, HUU NI UBAKAJI. KAMA KUNA MTU ANAYEAMINI KUWA MTOTO HUYO AMFANYA HIVYO KUTOKANA NA UTASHI WAKE BASI MTOTO HUYO ANAYO HAKI YA KUPIGA KURA. MRADI HUO UMETEKELEZWA KUTOKANA NA WAJIBU WA SERIKALI KWA WALIPAKODI NA SI SERA ZA CCM. CCM LAZIMA IJIFUNZE KUWAHESHIMU WALIPAKODI WOTE NA SI KUONA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI KUWA NI JUHUDI ZA SERIKALI BALI NI WAJIBU WA SERIKALI KWA WANANCHI. HAPA HAKUNA SABABU YA CCM KUJIVUNA KWA HILI KWANI NI SERIKALI IMETEKELEZA WAJIBU KWA WANANCHI NA SI FADHIRA.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 01, 2009

    Akitoka tu huko shinganga huyoo Australia, China na Norway!!! hadi mkome!! bila kusafirisafiri nje nchi haiendi!!!!
    Ni mimi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 01, 2009

    CCM wana matatizo ya ubongo!! sasa hapo wanataka kuwadanganya wananchi kuwa wao ndio wameleta huo mradi!!!

    ReplyDelete
  12. MediaViabilityJune 01, 2009

    Thanks Mr. President for giving compliments to President Mkapa.

    This show how much appreciative you are for people who deserve it.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 01, 2009

    JK bwna, kabisa mradi umejengwa na sisiemu, hhahahhahah sio walipa kodi wangonge masikini watanzania??????

    ReplyDelete
  14. ndugu yangu hapo juu utasisumbua kupanda ndege.tuulize sisi tuliokuwepo uchaguzi uliopita.wenzio wanajua namna ya kushinda uwapigie husiwapigie

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 01, 2009

    huo mradi siyo wa sisiemu.acheni upuuzi wa kujisifia kwa kodi za wananchi.

    ReplyDelete
  16. Mpinzani HalisiJune 02, 2009

    Wafipa tuna msemo "Aliyevaa kanga ya mama yako ndiye baba yako"
    Kubalini kwamba CCM imevaa khanga ya mama yetu na hivyo ndio baba yetu.
    Ni kweli hayo yamefanywa na walipa kodi na serikali iliyochini ya chama tawala CCM
    Tatizo la watanzania ni wafu wa mawazo kwamba hata ukweli ulio wazi hawahukubali kutokana na ugumu wa vichwa vyao.
    na ndio maana upinzani Tanzania ni zero kwakuwa hatujui lipi la kubisha na lipi la kukubali.
    Mimi si mwana CCM wala sikipendi hicho chama na viongozi wake ila tuwe na points na si kukipinga chama hata kwa lililojema
    Busara finyu kelele nyingi. Mtaing'oaje CCM?
    Upinzani wa kweli uko wapi kama sio kuwa wajinga na vichaa?
    "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hili yes CCM japo si chama bora.
    IQ ndogo sana wabongo. Principle ni "Bisha hadi ufe" hata bila kujua unabisha nini.
    Tutafute cha kupinga na kukosoa na sio mradi huu ambao wameufanya, mzuri na manufaa kwa umma
    Ukidhani CCM haikufanya then jihesabu umefanya wewe.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2009

    Katika karne hii bado tunaona kuchona maji ndio maendeleo???? Jamanai raisi wetu tena anaona fahari kumtwisha mtu maji....... Kweli tutafika?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2009

    Kama JK angekua kweli makini na haki/usawa kwa akina mama basi angetafuta jikaka fukani halafu amtwishe maji angalao kwa ajili ya hiyo snepu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 02, 2009

    JK, tunataka bomba iingie ndani ya nyumba yake mama huyo siyo wewe kumtwisha.

    Wamama wa afrika wanachoka saana kusomba maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...