HABARI KAMILI
JK amezindua mradi mkubwa wa maji kuliko yote Kusini mwa Jangwa la Sahara wa Ziwa Victoria ambao umegharimiwa na Serikali ya Tanzania bila ya msaada wa wahisani kwa zaidi ya Sh bilioni 200.
Uzinduzi huo ulionyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa,TBC1.
Katika hotuba yake ya uzinduzi uliofanyika wilayani Misungwi mkoani Mwanza jana, Rais Kikwete alisema uzinduzi huo ni sehemu tu ya utekelezaji wa ahadi za serikali yake kwa wananchi .
Alisema mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake za kuwapatia wananchi maji safi na salama.
Aidha alimsifu Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliyekuwapo katika uzinduzi huo kwa uthubutu wa kuamua kuanzishwa kwa mradi huo.
“Ndani ya Ilani ya CCM, mradi huu ulipaswa kukamilika mwaka 2010, Rais Mkapa alituachia na akaamini tutaweza na kweli Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha mradi huo kabla ya wakati uliokuwa umepangwa.
“Hii inadhihirisha CCM inaweza. Tumewaweza Busanda na bado tutaendelea kushinda, na mradi huu ni ushahidi,” alisema JK..
Mbali na Mkapa, JK pia alimshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye pia alihudhuria uzinduzi huo, kwa usimamizi mzuri wakati wa uanzishwaji wa mradi huo wakati akiwa Waziri wa Maji.
Pia aliwashukuru mawaziri walioiongoza wizara hiyo katika nyakati tofauti za utekelezaji wa mradi huo wakiwemo Stephen Wasira, Shukuru Kawambwa na Waziri wa sasa wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huo unaopita katika mkoa wa Mwanza hadi Shinyanga wilayani Kahama, utafaidisha vijiji 54 na wananchi zaidi ya milioni moja watakuwa wakipata maji kwa saa 24. Rais alikemea tabia ya baadhi ya wananchi ya kuharibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
“Kuna baadhi ya watu hapa wanakwenda kukata mabomba na kuchukua vifaa wakidai vya Wachina.
“Vitu hivyo sio vya Wachina, serikali imegharimia kwa fedha zake halafu nyie mnakwenda kunyofoa kisha mkikosa maji mnalaumu serikali, vitendo vya kuharibu miradi ni upuuzi na inasikitisha,” alisema JK.
Aliitaka mamlaka iliyopewa jukumu la kusimamia mradi huo chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sai, kusimamia na kuendesha mradi huo kwa ufanisi.


kidumu chama cha mapinduzi. Kidumu.
ReplyDeleteYani tumesha fikia kuona kua mradi lazima ufaziriwe na watu wa nje.Jamani nchi lazima kuendeleza miladi kwa kodi sio wafaziri.
ReplyDeletehahahahha sisiemukweli mnaweza yote, hebu wapeni na wengine basinafasi muone, mtajisifu kila siku kwa kuwa kiti mmekikalia hamtaki kuwappa wengine wakajaribu wanaowezakufanya mabadiliko, hebu kuweni kama nchi nyingine sio chama kimoja kitawale for life!
ReplyDeleteHivi CCM imengiaje kwenye hili? Mimi ninavyofahamu mradi huu umetokana na kodi za wananchi. Halafu kujisifia eti CCM inaweza ni ujinga tu. Mbona kuna mambo mengi tu ya msingi hayajatafutiwa ufumbuzi? Kwa kifupi ni kwamba Uchovu wa Tanzania ya leo umeletwa pia na CCM.
ReplyDeleteTanzania kweli tupo nyuma sana kimaendeleo... nilipofatilia kampeni za Obama niliona mabango meeeeengi sijui "Now We Can", "We Need Change", Bendera, Vipeperushi, n.k. Baada ya kuchaguliwa upuuziiii wooooooote huo sasa siuoni iwe kwenye majanga, shughuli za kitaifa, maendeleo au za kimataifa nikimuona Obama na Serikali yake kweli sioni huo upuuzi ninacho kiona ni Bendera ya Marekani tu labda na ya Nchi nyingine in case of international matter. hii inamaanisha serikali ya Obama ipo kwa ajili ya, na inawawakilisha Waamerica wote wala sio Wademocratic pekee.
ReplyDeleteSasa turudi nyumbani:
Iwe shughuli za kitaifa raisi akiwepo sare za CCM nyingi hata sometime bendera ya taifa hatuioni, Iwe maafa kama mbagara Sare za CCM, iwe uzinduzi wa Miradi sare za CCM, iwe sherehe za kitaifa Sare za CCM... hotuba ya raisi CCM imefanya hivi vile... mi naona kama inawezekana tubadilishe bendera ya taifa iwe ya CCM hata wimbo wa Taifa uwe wa CCM. huko nchi za nje wakibrouse au kuangalia kwenye TV watu watafikiri bendera ya Taifa letu ni rangi ya kijani na ngao yetu ni jembe na nyundo.
anyway tusilaumu sana kwa sababu raisi ni wa CCM, wakome wapinzani kwani hakuna aliyewalazimisha kuwa huko... sasa fainali ni kwetu sisi tusio na vyama hatumjui raisi wetu, wala serikali yetu... ingekuwa ni bendera ya taifa tu ndio inapepea au sare zilizoshonwa na zenye nembo ya taifa hapo ningesema raisi ni wa wote na serikali ni ya wote.
"Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza"
Lumbo
Ars
duh CCM iko juu! yani hiko kitoto wameshakiteka?!
ReplyDeleteJK keep it up kuwasafisha mafisadi Mkapa na Lowassa..Ila ujue kuwa tutapandA ndege kuja kupiga kura 2010 na bado hatujasahau huyo lowassa wako unaejitahidi kumbeba lkn jua habebeki binafsi huwezi kunikomvinsi kama na wewe ni mtakatifu ikiwa unawabeba mafisadi lazima kuna namna hapo nyerere hakuwa mnafiki kama hivyo hata ungekuwa mwanawe ukiboronga kamwe hakubebi kama wewe unavyowabeba mafisadi
ReplyDeleteEBANA CHEKI MKAPA ALIVOFUTUKA DUH!!!
ReplyDeleteANAKULA VIZURI KWELI ALICHOCHOTA KWA MIAKA KUMI...KWELI TAMBARARE!
MUNGU BARIKI TANZANIA..
HUYO MTOTO AMEBAKWA, KWANI UMRI WAKE HAURUHUSU KUJUA CHAMA GANI NI SAHIHI KWAKE, ILA WANACCM WAMEMPA SHAIRI NA MAELEKEZO YA NINI CHA KUFANYA, HUU NI UBAKAJI. KAMA KUNA MTU ANAYEAMINI KUWA MTOTO HUYO AMFANYA HIVYO KUTOKANA NA UTASHI WAKE BASI MTOTO HUYO ANAYO HAKI YA KUPIGA KURA. MRADI HUO UMETEKELEZWA KUTOKANA NA WAJIBU WA SERIKALI KWA WALIPAKODI NA SI SERA ZA CCM. CCM LAZIMA IJIFUNZE KUWAHESHIMU WALIPAKODI WOTE NA SI KUONA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI KUWA NI JUHUDI ZA SERIKALI BALI NI WAJIBU WA SERIKALI KWA WANANCHI. HAPA HAKUNA SABABU YA CCM KUJIVUNA KWA HILI KWANI NI SERIKALI IMETEKELEZA WAJIBU KWA WANANCHI NA SI FADHIRA.
ReplyDeleteAkitoka tu huko shinganga huyoo Australia, China na Norway!!! hadi mkome!! bila kusafirisafiri nje nchi haiendi!!!!
ReplyDeleteNi mimi.
CCM wana matatizo ya ubongo!! sasa hapo wanataka kuwadanganya wananchi kuwa wao ndio wameleta huo mradi!!!
ReplyDeleteThanks Mr. President for giving compliments to President Mkapa.
ReplyDeleteThis show how much appreciative you are for people who deserve it.
JK bwna, kabisa mradi umejengwa na sisiemu, hhahahhahah sio walipa kodi wangonge masikini watanzania??????
ReplyDeletendugu yangu hapo juu utasisumbua kupanda ndege.tuulize sisi tuliokuwepo uchaguzi uliopita.wenzio wanajua namna ya kushinda uwapigie husiwapigie
ReplyDeletehuo mradi siyo wa sisiemu.acheni upuuzi wa kujisifia kwa kodi za wananchi.
ReplyDeleteWafipa tuna msemo "Aliyevaa kanga ya mama yako ndiye baba yako"
ReplyDeleteKubalini kwamba CCM imevaa khanga ya mama yetu na hivyo ndio baba yetu.
Ni kweli hayo yamefanywa na walipa kodi na serikali iliyochini ya chama tawala CCM
Tatizo la watanzania ni wafu wa mawazo kwamba hata ukweli ulio wazi hawahukubali kutokana na ugumu wa vichwa vyao.
na ndio maana upinzani Tanzania ni zero kwakuwa hatujui lipi la kubisha na lipi la kukubali.
Mimi si mwana CCM wala sikipendi hicho chama na viongozi wake ila tuwe na points na si kukipinga chama hata kwa lililojema
Busara finyu kelele nyingi. Mtaing'oaje CCM?
Upinzani wa kweli uko wapi kama sio kuwa wajinga na vichaa?
"Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hili yes CCM japo si chama bora.
IQ ndogo sana wabongo. Principle ni "Bisha hadi ufe" hata bila kujua unabisha nini.
Tutafute cha kupinga na kukosoa na sio mradi huu ambao wameufanya, mzuri na manufaa kwa umma
Ukidhani CCM haikufanya then jihesabu umefanya wewe.
Katika karne hii bado tunaona kuchona maji ndio maendeleo???? Jamanai raisi wetu tena anaona fahari kumtwisha mtu maji....... Kweli tutafika?
ReplyDeleteKama JK angekua kweli makini na haki/usawa kwa akina mama basi angetafuta jikaka fukani halafu amtwishe maji angalao kwa ajili ya hiyo snepu.
ReplyDeleteJK, tunataka bomba iingie ndani ya nyumba yake mama huyo siyo wewe kumtwisha.
ReplyDeleteWamama wa afrika wanachoka saana kusomba maji.