MPAKA sasa hakuna taarifa zinazoeleza kwa kina mahala alipo Deogratius Kweka, ambaye alikuwa mshtakiwa mwenza wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa BoT Amatus Liyumba, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo na kuisababishia Serikali hasala ya mabilioni.
Kweka, ambaye alikuwa Meneja Miradi wa BoT, hapo awali alishtakiwa pamoja na Liyumba kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serili hasala ya zaidi ya Sh Bilioni 200.
Katika kesi hiyo ya awali, Kweka na Liyumba waliachiwa baada ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusema kuwa hati iliyotumika kuwashtaki ilikuwa na makosa ya kisheria.
Hata hivyo baada ya kuachiwa, walikamatwa tena ambapo kwa siku hiyo walilala katika kituo cha Polisi, na baadae Liyumba alipandishwa kizimbani akiwa pekee bila Kweka.
Juhudi za Globu ya Jamii kutaka kufahamu juu ya hilo kwa kuongea na wahusika mbali mbali akiwemo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova ziligonga mwamba jana baada ya maofisa hao kudai kutofahamu alipo Kweka na wengine kutotaka kuzungumzia juu swala hilo.
Yaani mpaka sasa hakuna mwenye taarifa inayotoa uthibitisho kama Kweka ameachiwa huru au mahala alipo baada ya kutoka mahakamani.
Kweka kaachiwa hana kesi ya kujibu
ReplyDeleteIla DCI Manumba kuna mhasibu wa DECI hapa Mwanza kaiba Sh zidi ya 300 milion za DECI kanunua ghorofa na magari lukuki binti wa miaka 25 mtume RCO amtingishe binti huyu arudishe fedha zetu