Mlimbwende mwenye ulemavu wa ngozi (albino)
Grace Wabani akiwa na wenzie kambini

Mkoa wa Mwanza umejipanga kuweka historia katika tasnia ya ulimbwende nchini kesho wakati wa kumpata mrembo atayewakilisha mkoa huo katika Miss Tz ya mwaka huu.
Kwanza kabisa imepania kuweka historia kwa kutetea taji la Miss Tanzania linaloshikiriwa na mrembo Nasreem Karim kutoka jijini Mwanza.
Pili ni kushirikisha mrembo mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo toka yaanze mwaka 1994, baada ya kupigwa marufuku baada ya kufanyika mara ya kwanza kabisa mwaka 1972 ambapo hayati Theresia Shayo aliibuka mshindi.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 si mwingine ila Grace Wabani ambaye ameleta msisimko wa waina yake katika kinyang'anyiro hicho, ikizingatiwa kwamba Mwanza ni mmoja wa mikoa inayoongoza kwa vitendo vya kikatili dhidi ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
Wachunguzi wa mambo wameielezea hatua ya mrembo Grace kushiriki katika mashindano ya ulimbwende ni mojawapo ya dalili za kufanikiwa kwa kampeni ya kuwajumuisha katika jamii albino ambao kutokana na imani potofu wamekuwa wakitengwa na kunyanyaswa pamoja na kufanyiwa unyama.
Wamesema Grace atazidisha mwamko kwa walemavu wenzie wa ngozi wajione kuwa na wao ni wanajumuiya na wanakubalika. Tayari hapa Dar kuna timu ya soka ya albino na pia kuna kikundi cha ngoma ambacho kilitumbuiza kwenye mashndano ya Miss Universe Tz wiki iliyopita.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Flora Entertaiment,Flora Lauwo amesema kuwa warembo wote wanaotarajia kushiriki kwenye mashindano hayo kesho ijumaa uwanja wa CCM Kirumba ni wakali na wametimia kila idara.

"Warembo wa safari hii ni wakali na wametimia kila idara,na kubwa zaidi kwa mara ya kwanza katika historia ya mshindano ya urembo hapa Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla,safari hii tunamshiriki mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) anayeitwa Grace Bani (23),ambaye naye kiukweli ana vigezo vyote vya kushiriki shindano hili,na nina imani naye atafanya vizuri",amesema Flora.

Flora amesema kuwa katika kinyang'anyiro hicho cha kumsaka kinara wa miss Mwanza 2009,washiriki wake wako jumla 15 akiwemo binti mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Grace Wabani 23,
Aidha amewataja washiriki wengine kuwa ni Warembo wengine ni Miriam Ismail (18), Roda Uyombe (22),Jacquline Msuya (20),Miliam Gerald (21),Lisa Deus (20),Eva Sitta (22),Amina Adam (20),Aika Kanenda 21,Grace Frances 21 Fiobe Samweli (22), Sheila Ismail (19),Joy Pastory (20),Emi Yachi (22) na Bulelo Tambalo (20).

Katika shindano hilo Flora amesema kuwa pia kutakuwepo na burudani mbalimbali kama vile fasheni shoo,waimbaji wa muziki wa taarab akiwemo Hammer Q, Afua Suleiman, kikundi cha muziki wa kizazi kipya cha BWV cha jijini Mwanza na burudani nyinginezo.

Flora amesema ndani ya kinyang'anyir0 hicho kiingilio kimepangwa kuwa ni kiti cha Gold (20,000/=) kiti cha Silver (10,000/=) kiti cha kawaida 5000/=

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    Kwanza napenda kumpongeza Flora lauwo kwa kuwaandaa mabinti warembo pamoja na mrembo albino kwani wote wana nafasi ya ushiriki sawa.

    Pia namwomba RCO mwanza amkamate yule binti Mhasibu wa DECI mwanza kaiba hela nyingi sana za wana DECI mwanza zaidi ya sh 300 milion asijekukimbia kanunua ghorofa huko kiloleli na magari lukuki. warembo wanajitolea kwa jasho yeye anafisadi hela za walalahoi Manumba na tume ya deci habari ndio hiyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2009

    Huyu binti atashinda - yaani hii itakuwa strategy nzuri sana ya majaji wa Ms TZ kuonyesha dunia kuwa wantanzania wanawapenda na kuwakubali na kuwapromote walemavu wa ngowi (albinos) - Nakutakia mafanikio mema.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    Huyu Grace anajichoresha tu, mlemavu na beauty pageant, wapi na wapi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    HII HABARI NI AINA MOJAWAPO YA KUNYANYAPAA. KAMA UKINIELEWA VIZURI NAMAANISHA NINI, NAFIKIRI UTABADILI KICHWA CHA HABARI HII.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    Anonymous wa June 04, 2009 11:17 AM grow up.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Kwa kweli kwa Grace ni kitu ambacho hakitawezekana kushinda kwasababu; Grace tayari ni mlemavu. Na ni mlemavu wa ngozi…..hapo Miss Tanzania wanatafuta watu warembo na tunajua mtu mrembo anavigezo vya uzuri mfano:- asiwe mlemavu sababu akiwa mlemavu tayari ameshaaribu sifa ya urembo wake, asiwe na matege, asiwe na kasoro yoyote katika mwili hata meno tabasamu liwe zuri. Sasa itakuwaje Albino awe Miss Tanzania. Wakati Albino ni mlemavu wa ngozi na hata macho.

    Sisi sio kama tunamnyanyapaa hapana ni binadamu kama sisi ila hiyo ndiyo hali halisi ya mtu kuitwa mrembo.

    Hakika tutakuwa tunajidanganya kwa Grace kushinda sababu hata Miss world hatashinda.

    Mbona tupo wengi tuu warembo lakini hatushiriki, tuna kasoro ndogo ndogo tu za miili yetu mfano matege, meno. Kushinda ngumu

    Grace dada yangu kushinda wewe ngumu. Wewe uza tu sura ujulikane

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Mbona na nyie Viongozi wa Miss Tazania mnabahatisha?? Tangu lini mlemavu akashiriki mambo ya urembo wakati kasoro ya kumfanya asiwe mrembo tayari anayo!!???
    Acheni kutuzingua.......

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    Tunajua kamati ya Miss Tanzania mnajali Maalbino lakini sio Albino kushiriki urembo tafuteni mashindano mengine muwaeke lakini sio ktk urembo. Mnachekesha sana nyinyi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    Sasa huyo ataesabika Mwafrika au mzungu???

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    Mimi ninachanganyikiwa niseme nini kwa hili, sijawahi kushiriki katika mashindano ya urembo lakini sielewi kama ngozi huwa ni kigezo, kama ni kigezo basi ninapata wasiwasi na huyu mshiriki, ila ninamtakia kila la heri

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    Wewe Anonymous June 04, 2009 10:55 AM.....Unajua maana ya BEAUTY???? Unajua sifa za BEAUTY??? hebu toa sifa za beauty then ndio utajua Albino atashinda na nisahihi kumuweka katika mashindano haya au laa....

    Hatumnyanyapai tunasema ule ukweli.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    Siyo kama Grace tunamnyanyapaa, hapana, nature ya mashindano yenyewe yalivyo hayampatii sifa ya kushiriki,Na ndiyo maana viwete nao walifanyaga mashindano yao ya u-miss, au watu wanene wana mashindano yao yaniitwa sijui, miss Bantu, nk. If that is the case siku moja tutakuja kuwa na washiriki u-miss vipofu, mbilikimo, etc, hapo ndipo maana ya mashindano ya urembo/ulimbwende itakapoondoka.Kama tunafanya kwa nia ya kuonyesha kwamba tunawajali maalibino, je Grace akishinda akaenda huko miss world, wenzetu watatuelewaje,kwamba Grace ndo mrembo kuliko watz wote, or we're not serious and we're trying to be funny? Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    Hapa kazi ipo....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...