Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Nanihii,Balozi wa Nanihii, naMwenyekiti Mtendaji wa Blogu ya jamii.
Kwanza nikupongeze saana kwa kazi nzuri unayoifanyia jamii. Pili nikupongeze kwa kuendeleza libeneke tangu blogu hii ilipoanzishwa rasmi pale Chelsea Pub, Helsinki mpaka leo ambapo imefanikiwa kuwa chombo muhimu sana cha mawasilianao ya wabongo kote duniani.
Miezi kadhaa iliyopita nilianzisha blogu inayohusiana na REAL ESTATE. http://dmkrealestate-tanzaniaproperties.blogspot.com/.
Niliisambaza kwa baadhi ya watu na mashirika ilivyowezekana, na sasa, hasa baada ya kutuhamasisha kwenye post au toleo lako la juzi jumalipi june 7 kwamba tuchangamkie tasnia hii ya TEKNOHAMA, nimeona ni vyema nikaiwakilisha kwako na kwa jamii pia.
Mheshimiwa, katika toleo lako nililitaja hapo juu, ulionyesha kutoridhishwa kwako na kiwango kidogo cha matumizi ya blogu na wasiwasi walioonyesha baadhi ya watu kwamba blogu si chombo rasmi cha mawasiliano. Wengi wametoa mawazo yao kujaribu kujibu hoja zako. Mimi nitajibu kwa kifupi sana hoja zako nne kama ifuatavyo bila kuzirudia hoja zenyewe:
1. Wengi wanakataa kuzikubali globu kwasababu hatujazifahamu vizuri kama vile ambavyo tumezoea websites za kawaida. Resistance to change, au kuzuia mabadiliko kwa kutojua hali mpya inafanya watu wawe na wasiwasi.
2. Kuhusu wabongo kuamka kuchangamkia vitu kama blogu, twitter ama podcast na nyinginezo, ni kwamba hatujafika huko. Gharama bado ni kubwa sana bongo na ujuzi au “aptitude”ya kuvitumia hivyo vitu ni tofauti na wenzetu walioko nje kwa sababu kule nje ni rahisi kuvipata na pia kuvitumia na hivyo kuwa na experience navyo zaidi(fikiria umeme, bei za internet na simu/mawasiliano n.k)
3. Kwamba waandishi wachache sana kutumia teknohama mpya. Hili nadhani linahusiana na la kwanza hapo juu.
4. La mwisho ni kuhusu wizara na idara za serikali. Mimi nadhani hatuna utamaduni wa kupashana habari za mipango ya utelelezaji wa kiserikali/kijamii.
Viongozi wengi wanawajibika kwa wakubwa zao zaidi na si kwa jamii. Tumeona nchi mbalimbali unaweza kuona bango kuubwa linaelezea mradi fulani wa muda mrefu, na wananchi wanaombwa wachangie mawazo juu ya utekelezaji. Wanashirikishwa. Hapa changamoto ni ushirikishwaji wa uma. Bado tuna kazi eneo hili.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nanihii,
nihitimishe kwa kusema kwamba kama isingekuwa TEKNOHAMA ya kisasa, leo hii labda Barack Obama asingekuwa rais wa Marekani!. Na sisi tutafika huko. Kwa heshima na taadhima, naomba kuwakilisha
Karibuni m-bookmark:
Mdau David.
Huo mjina wa blog yako mrefu sana. tafuta jina zuri na fupi na rahisi kukumbukwa
ReplyDeleteDoh! Watoto wao watakuwa na mizinga ya mwanya! Best Wishes!
ReplyDeleteThis infomation could not be more timely. Asante sana mdau na ninakuandikia email sasa hivi.
ReplyDelete