MFANO WA UKURASA UNAOTAKIWA KUUUTUMA BAADA YA KUUKOPI AMA KWA KUUPIGA PICHA


MDAU WA MILIONI SITA ATAPATIKANA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA WADAU KAENI MKAO WA KULA MAANA SPIDI YA HESABU ZA WADAU KAMA TARAKIMU ZINAVYOONESHA HAPO CHINI KULIA KUELEKEA KWENYE MILIONI SITA SI YA KAWAIDA.




NAMNA YA KUJISHINDIA DOLA 1,000 ZITAZOTOLEWA NA VODACOM TANZANIA KUPITIA HUDUMA YAKE BOMBA YA 'THE GRID' NI RAHISI SANA.




UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KWAMBA ENDAPO UTAFUNGUA GLOBU YA JAMII NA KUKUTA TARAKIMU PALE CHINI ZIKIONESHA 6,000,000 BASI UJUE UMEULA.




UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUKOPI UKURASA HUO WENYE TARAKIMU HIZO ZA 6,000,000 NA KUUTUMA KWA EMAIL KWENDA issamichuzi@gmail.com NA MUDA SI MREFU UTATANGAZWA MSHINDI NA UTAAMBIWA UTAPATAJE MKWANJA WAKO.




NAMNA YA KUKOPI UKURASA HUO NI AIDHA PIGA PICHA SEHEMU HUSIKA NA KUITUMA AMA BOFYA KIDUDE CHA 'Prt SC Sys Rq' AMA CHA AINA HIYO KINACHOKUWEZESHA KUKOPI UKURASA, KISHA NENDA KWENYE 'START' AMBAPO UKISHABOFYA TAFUTA 'PAINT' KUPITIA 'ACCESSORIES' NA UKISHABOFYA NENDA KWENYE 'EDIT' AMBAPO UTABOFYA 'PASTE' NA KUKUTA UKURASA ULIOKOPI UNAJAA HAPO. 'SAVE' NA KISHA TUMA KAMA ATTACHEMENT KWENDA EMAIL HIYO.




MASHARTI NI YALE YALE




1. MSHINDI NI MMOJA TU NA MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO RUKSA KUSHIRIKI


2. UJANJA UNJANJA HAURUHUSIWI NA WALA USIJISUMBUE KWANI JOPO LA WATALAMU LIKO MACHO KUNG'AMUA HILO


3. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO


4. MSHINDI ATAPATIWA MKWANJA WAKE BAADA YA KUTHIBITISHWA INGIZO LAKE NI LA HALALI. KAMA YUPO DAR ATAELEKEZWA WAPI AJE KUCHUKUA MZIGO WAKE, KAMA YUKO NJE YA DAR ANARUHUSIWA KUTUMA WAKALA KUMCHUKULIA.




-MICHUZI






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2009

    I'm not using microsoft's operating system. How can I go about to get those screenshots?

    I'm kidding. Your description is for only MS windows while others we don't use.

    I will get that award.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2009

    Michuzi unafaa kuwa mwalimu wa computer.
    I`m just say.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2009

    Michuzi and all wadau the truth is kweli sielewi jinsi ya ku-join hili shindano la mdau wa milioni za Michuzi mara sita mara tatu. Please naomba ushauri

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2009

    Juu tangazo la kifo katika mdau wa milioni sita chini tangazo la kifo. Hata mdau huyo atakufa kha!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2009

    mi sijaelewa bado hiko kitufe kiko wapi natumia.kompyuta yangu ni pc tu ya kawaida na natumia windows xp.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2009

    weweeee acha zako apa

    unamtuma mtu akuchukulie?kwani hatuna akaunti bank??

    afu acheni fix

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...