Shindano la kumtafuta mrembo wa tanzania katika eneo la nchi za Shengen barani Ulaya linafanyika Jumamosi hii mjini Essen nchini Ujerumani.

Warembo wa kitanzania kutoka Norway, Holland, Ujerumani na Ufaransa wanashiriki kinyang´anyiro hicho kinachosubiriwa kwa hamu.


Mwaandaji wa shindani hilo Nashe Mvungi amethibitisha kuwa kila kitu kiko sawa, ambapo bendi ya wanamuziki wakongwe wa Afrika yenye maskani yake ijini Berlin itatumbuiza.Katika bendi hiyo yuko mpiga solo maarufu wa zaman wa orc Lipua Lipua, na Kamaley za Zaire ya wakati huo, Lusuama Aspro.


Pia mmoja wanamuziki aliyewahi kuimba na Koffi Olomide anaitwa Solei atashirikiana na kundi hilo.Soley ka sasa anaishi Paris.


Aidha Nashe amesema kundi a wanamuziki wa kizazi kipya la kitanzania lililopo hapa Ujerumani Lizchip&Gloria litatoa burudani katika shindano hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa balozi wa tanzania nchini Ujerumani HE Ahmada Ngemera.


Katika shindano hilo, Mwenyekiti na mmiliki wa bendi za African Stars Twanga Pepeta na Vibration Sound, Baraka Msilwa atakuwa mmoja wa majaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    wewe nshamba huwezi kupewa mke wa kiungwana kwa kuanza na sifa kujitangaza kama wewe ni it na kuanza kuponda wenzako wenye uhalali wa kuishi majuu kinyume na wako wewe bishoo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    Naomba pleeeeease, this time muwapige piche vizuri, mnawafanya waonekane ordinary, wakati ni warembo na wamejitahidi waonekane.
    Mjue haya mashindano si ya talenta kwanza, ni ya urembo, na mara nyingi ni first i mressions ndio zinawafanya watu waside na mmoja wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...